Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%

Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%

Kumlea kama yai ndio sababu anakuja kuwa mjinga
Mtoto mjinga chapaaaa miguu hiyo na mikono
 
Leo mnatudhihaki mnatuita viumbe wa ajabu sawa hamna shida ...mungu yupo ...kama tumekosea kiasi hicho tutalaaniwa naye..Ila kama ni tofauti ........Dunia itaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%
Fuatilia mwongozo huu: Mwalimu hakikisha umefika shule muda husika, simamia usafi na kama wanafunzi hawaonyeshi kushiriki kufanya usafi, tafadhali usishike kiboko. Mwalimu kumbuka muda wa vipindi ukifika hata kama mazingira ya shule ni machafu, wanafunzi waingie darasani tayari kwa masomo. Mwalimu fundisha kipindi chako kama mwongozo unavyoonesha, tafadhali usiwafuatilie wanafunzi wasioandika, kwani inaweza kuhamasisha hisia za kutoa adhabu ili kumjenga mwanafunzi husika. Mwalimu, daftari zikikusanywa kwa ajili ya kusahihisha, tafadhali usifuatilie kubaini wanafunzi wasiokusanya daftari kwani kubaini kwako kunaweza kupelekea kuwepo na mazingira yenye kuchochea adhabu.
Mwalimu wakati utakapoita majina, zingatia kuwa wale waliopo darasani kwa wakati huo ndiyo wanaokuhusu, hitaji lako la kutaka kujua mwanafunzi X ana tatizo gani la kutokuja shuleni linaweza kupelekea mazingira yatakayo chochea adhabu, kwani wanafunzi wenzie wakati mwingine watakupa jibu kuwa mwanafunzi X yupo maeneo ya chooni anacheza tu, hivyo jibu ili linaweza kupelekea mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu, mara upatapo kesi za mwanafunzi X kuwa amepigana darasani au kutoa lugha chafu, tafadhali tumia neno moja tu kuwa "LUGHA ZA MATUSI SI NZURI " kisha mruhusu kurudi darasani ili kuepusha mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu mzazi akikuletea kesi ya mtoto wake kuhusu tabia za nyumbani na hata mwenendo mbovu wa maendeleo yake darasani, tafadhali mueleze mzazi kuwa amalizane na mwanaye kwa namna inayofaa. Mwalimu wangu ukifuata muongozo huu, shutuma na jazba za wana wa nchi hii utaziepuka pia itakusaidia japo kurudisha mwili wako uliopukutika kwa kufuatilia watoto wasiokuhusu, nakutakia kazi njema mwalimu wangu.
Bila shaka wewe ni Mwalimu, na hukuridhishwa na kauli ya Mhe. Waziri. Naunga mkono mwongozo huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwanafunzi akirusha kondomu mbele wakati mwalimu upo darasani .........
mwanafunzi akija amelewa......
anaefanya vibaya asiadhibiwe na anaefanya vizuri je...
vip zile video za wanafunzi wanaoshindwa kusoma mbn huw zinwafuraisha au .....
vip ile ya mbeya day mnaikumbuka.....

YAJAYO YANAFURAHISHA JE MPO TAYARI
walimu wanakazi aisee
 
Kwa mtazamo wangu,mtoto aliyepigwa hadi kufa huko Kagera alionewa sana,sana sana!!

Mwalimu aliyekuwa anatoa adhabu kwa mtoto yule anastahili adhabu kabisa,kwa sababu kitendo cha mtoto kumpokea mwalimu wake mizigo kilitosha kutambua tabia ya mtoto kabla ya kumuadhibu vikali.

Jambo la pili,kwa umri wa mtoto yule,hakuwa na uwezo wa kujitetea kwa kumkuda mwalimu wake,kwa hiyo mwalimu kuendelea kumpiga ni kujitoa ufahamu,na MAKUSUDI!(MWALIMU YULE AADHIBIWE TU,UMRI WA MTOTO NA KIPIGO CHA NAMNA YA ILIVYOSIMULIWA,SI JAMBO LINALOVUMILIKA)

Kwa upande wa kanuni za namna ya kuadhibu mwanafunzi shuleni,zinaweza kutekelezeka pasipo tatizo kwa watoto wenye kujielewa (waliolelewa kwa maadili ya heshima na wazazi wao)

Kwa watoto ambao kwao heshima si kipaumbele,(kuanzia kwa wazazi wao) hizi kanuni hazitekelezeki,(hasa sekondari) ambako mtoto ukimuita anaweza akagoma kuja,ukimfuata anaokota mawe,na kukutwanga nayo!(wapo watoto wa namna hiyo).

Mwanafunzi wa kidato cha tatu,anakuja shule asubuhi akiwa amevuta bangi,amekaa darasani hana daftari hata moja,ukimwambia habari ya kwenda kwa mkuu wa shule sijui kumtoa darasani,anaanzisha varangati,muda huo anajiona yeye ni Van Dame, au John Sina!
Application ya kanuni na sheria kwenye mazingira hayo ni ngumu sana,mwisho wa siku ni hisia na hasira huchukua nafasi!

Nadhani,ili kuweka sawa mambo haya,watoto wa aina ya kuvuta bangi,na watukutu kupindukia,wafukuzwe shule mara moja,(mamlaka hayo ipewe kamati ya nidhamu shuleni),kwa sasa mwanafunzi hawezi kufukuzwa shule mpaka bodi ya shule ikae,(na sijui huwa wanakaa mara ngapi kwa mwaka).

Lakini kwa utaratibu wa sasa,ambapo nasikia mwanafunzi hafukuziki shuleni mpaka bodi ya shule ikae na kuamua,kuna watoto wataendelea kuaumbua sana walimu huko mashuleni.

Wasalaam!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
U-local wako wa kuzaliwa sehemu moja na kukulia sehemu ile ile ndiyo unakufanya ufukirie viboko ndiyo njia pekee ya kumfanya mwanafunzi awe na tabia nzuri. Ulaya watoto hawachapwi na wanapokuwa wanakuwa na heshima na ni waaminifu. Bongo mnachapa viboko na watoto wakimaliza ndiyo wanakuwa wezi, waongo na waasherati wakubwa!
Ndio hata mimi nashangaa. Tumekazana viboko tu kama suluhu. Sijui tupoje maafrika.
 
Mtaa upo utawatandika tu bakora za kutosha nyie walimu subirini salaries zenu tu
 
Naona walimu mnatafuta kila njia ili mpewe ruhusa ya kuwachapa km ng'ombe watoto, now jela inawahusu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mwanafunzi tena usiejielewa hadi viboko ndio akili yako inazinduka, Nakumbuka viboko vya mwalimu wangu Mwabukusi enzi zile pale Jangwani na Mwalim Mbasha Mlanda Sumbawanga, kwa viboko vile wala tusingekuwepo leo. Kwa tukio la Bk, mimi siamini kuwa viboko vya Mwalim ndio vimeondoa uhai wa mtoto wetu, mtoto alikuwa na shida tu lakini majibu ya viongozi ni kwa ajili ya kutuliza upepo tu. Kama waalim wataacha kabisa kuwafuatilia watoto wetu matokeo tutayaona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hata mimi nashangaa. Tumekazana viboko tu kama suluhu. Sijui tupoje maafrika.
Unajua Ulaya viboko vilisitishwa mwaka gani? Na baada ya kuondoa viboko nini kilifuata? Au mnaandika upuuzi wenu wa vijiweni?Mzazi unakaa na mtoto wako masaa mangapi kila siku hadi ujue anayoyafanya? Mwalim nfie mtu pekee anayekaa na watoto wetunmuda mrefu, ndiye anaweza kumjua mtoto msikivu na jeuri, nafikiri mjadara uwe ni vipi Mwalim amuadhibu mtoto anapokesea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom