Si kwa Mwanafunzi wa Dar, ninamifano mingi ya Shule za Kata Dar ambazo wakuu hawakuwa na mchezo, mtoto akikosea kidogo ni bakola na wakawa safi hadi Darasani na matokeo yao ya mwisho yalikuwa mazuri. Kuna tofauti kubwa kati ya shule binafsi na za kata, binafsi mwalim analipwa vizuri.na anatumika vizuri, binafsi darasa halizidi watoto 45, kata wanafika 100, binafsi mtoto mtovu wa nidhamu hurudishwa nyumbani hapo mzazi huumia na kumuadhibu mwanae kwa sababu ya ada anazolipa, huku upande wa pili hamna hilo. Ndugu yangu, Wazo lako si baya lakini kwa Tanzania bado ssna maana sehemu kubwa ya watoto hawajui kwa nini wanaenda shule, baadhi ya wazazi pia hawajui umuhimu wa Elimu kwa watoto wao.Tunapaswa kuwa na mjadala mpana wa kuwasaidia watoto wetu.
Sent using
Jamii Forums mobile app