mpekuzifacts
Member
- Feb 12, 2015
- 60
- 10
Nchi ya maigizo hii.
Sijui kwanini sijawahi kumuelewa Mwakyembe toka asubuhi ile ya February 7 mwaka 2008
Huwezi kumuelewa. Rudi shule
Nchi ya maigizo hii.
Sijui kwanini sijawahi kumuelewa Mwakyembe toka asubuhi ile ya February 7 mwaka 2008
Swadakta !
Unaweza changia kwa kipande unachokubaliana nacho
Bade harudi tena....unaweza changia ili madudu haya yasijirudie
With great power (commissioner general-TRA) comes great responsibility. Bade hawezi kuachwa wakati makasha mengi kiasi hicho hayajalipishwa kodi. Na uzuri hajafukuzwa kazi, amewekwa pembeni ili ukweli upatikane. Kusimamishwa kwake ni kwa haki, ingawa namuonea huruma kama binadamu maana kwa nafasi yake wanasiasa wanamtumia kiasi cha kuharibu weledi wake. Ukwepaji mkubwa wa kodi kama huo hauwezi kukosa mkono wa wanasiasa.
Naungana nawe kuwa tunahitaji everlasting plans and strategies kwenye suala la kodi ili hata akija rais msela nchi isiathirike kimapato.Serikali ilichofanya so far ni cha muda mfupi na cha kujipatia umaarufu. Tunahitaji taasisi imara, sio viongozi imara. Ingawa pia taasisi imara hujengwa na viongozi imara. Tunahitaji mapinduzi ya kisera. Mfano badala ya TRA kujikadiria makusanyo, kinaweza kuundwa chombo kingine au kilichopo(mfano tume ya mipango) ili kitumike kuwakadiria makusanyo kwa mwezi,robo,nusu na mwaka mzima. Wabanwe kwa kutofikia malengo waliyopangiwa na malengo yawe ya juu kiasi kwamba hawatathubutu kupoteza mapato kizembe. Hiyo ni namna moja ya kisera na inayoweza kuzaa matunda kwa muda mrefu.
Kwa mtazamo mwingine ni kuwa TPA walifanya kazi yao, walifanya records za containers na wenye containers walilipa custom duties kama kawaida ndio maana records zipo wazi TPA...
Shida ipo huko TRA, ICT ya TPA na walinzi wa TPA Gate 5, kuna rushwa zilitembezwa hapo ili containers zipitishwe bila TRA kulipwa kodi stahiki, maana yake inawezekana wafanyakazi wa TRA walikuwa na records zilizotumwa na TPA, lakini wao kwa kupewa rushwa wakatoa release order bila kupokea malipo...
Mchezo ulichezwa na maafisa wa TRA, ICT ya TPA na walinzi...huwezi kuihusisha TPA moja kwa moja coz tayari management ilipokea containers, walitoza custom duties na kurelease docs TRA..ndivyo nilivyoelewa!
Sijui umeona ile link inayosema Masamaki aliteuliwa na bodi
huku akiwa tayari na kshafa ingine ya kupoteza makontena?
na hiyo ni mwaka 2013 Bade akiwa naibu kamishna
vitu viwili naviona hapa
1.upotevu wa makontena sio kitu kipya
2.kamishna hana mamlaka ya kuteua watendaji na wala sijui kama ana mamlaka ya kufukuza
mwakyembe ni vema sasa akaachana na siasa , hali yake mbele ya macho ya jamii hairidhishi kabisa , angeandika Erythrocyte hapa angeibuka TRUVADA au Mgirik kusakama , haya sasa watu wengine wameyaona madudu yake !
Hao walikuwa mawaziri wa uchukuzi sio wizara ya fedha.
Bandari kwenye sakata hili inaonyesha walifanya kazi yao. Sehemu iliyobaki ilikuwa TRA. Waziri mmoja hawezi kuingilia wizara nyingine ndiyo mgawanyo wa kazi.
Ndiyo ile orodha Majaliwa kaipata bandarini. Inaelekea watu wamefanya reconciliation, wakaona madudu sehemu ya TRA.
Mkuu The Boss Hii issue ya container 300+ Bandari wako safe inawezekana hata port charges zote zililipwa ndio maana yanaonekana kwenye system ya TPA.
Tatizo liko TRA Kwa kuwa hayako kwenye system yao na wala Ushuru haujalipwa. Sujui kama kuna mfanyakazo wa TPA kawajibishwa zaidi ya kuambiwa wa review walinzi wa Gate 5.
Nadhani upeo wako wa kufikiri ni mdogo. Mimi kwa mtanzamo wangu Mwakyembe alisaidia sana kusafisha Bandari na kila mtanzania analijua hilo. Kabla ya Mwakyembe kuingia Wizara ya uchukuzi hali ilikuweje bandarini na baada ya kuingia ikaweje, tuache unafiki wa kisiasa. Pia elewa kuwa makontena yaliyopotea yaliyoibuliwa na Majaliwa yapo chini ya TRA ambao ndio wanayasimamia. TRA ipo chini ya Wizara ya Fedha na siyo Wizara ya Uchukuzi, nenda shule.
Hahaa hebu jisome tena