Mwakyembe, Sitta 'walisafisha' nini Bandarini?

Mkuu ahsante kwa kunielewa....
maswali hayo very valid...na wapo wana JF wanaishi nchi hizo wanaopita hapa
lakini hizi mbwembwe zina 'mvuto' zaidi kwao

Hilo hasa ndilo tatizo langu. Tunajenga mifumo au majina kama kwenye bongo movies?
 
Ndio wote hawa hawafai walikuwa wanafanya mambo kwa manufaa yao kazi yao ilikuwa ku deal na wafungua mageti tuu, ona mwenzao ana deal na ma incharge., sita na mwakyembe walikuwa wanatafuta sifa na kutaka uraisi . Watulioe tuu waonw mwenzao akifanya kazi.
 
Wasikuumize kichwa wanajua sana tofauti sema wamepotezana na viongozi wao wakuu ndio hawajui nini hasa wanapigania.
Ndugu jaribuni kutofautisha TPA iliyo wizara ya Uchukuzi na TRA iliyo wizara ya fedha ingawa zote zipo Bandarini
 
Jamani kwa kasi inayoendelea ya Dr Magufuli na PM wake ni dhahiri hao mawaziri wa zamani hawafai kurudi kwenye baraza. Naongezea;
1. Lazaro Nyarandu
2. Professor Magembe
3. Etc
 
Waanze kwanza na wale vijana pale namba 5, na washitakiwe kabisa! Wanaboa sana aisee.. mapka mlinzi wa kampuni binafsi wana nguvu sana pale gate number 5
 
Ndio wote hawa hawafai walikuwa wanafanya mambo kwa manufaa yao kazi yao ilikuwa ku deal na wafungua mageti tuu, ona mwenzao ana deal na ma incharge., sita na mwakyembe walikuwa wanatafuta sifa na kutaka uraisi . Watulioe tuu waonw mwenzao akifanya kazi.

Umelewa viroba nn
 
Huyu Bondeni ni povu tupu kweli ww bondeni kweli kweli, hujui unachoandika zaidi pumba za kuweweseka tu
 
Tulikuwa tunampa hongera na sifa nyingi humu Mwakyembe tukisema 'aliisafisha bandari' na ni 'mchapakazi' na wengine wakiomba ateuliwe kuwa Waziri mkuu ili alete Hiyo kasi na uchapakazi lakini tunakumbuka Sitta alipom replace na yeye Sitta akala 'ujiko' wa kuisafisha bandari na kuondoa madudu.

Kumbe in reality hakuna walichokifanya au walichokifanya hakikuwa na manufaa sasa tena sasa tunashingilia Magufuli na Majaliwa 'kuisafisha 'bandari na kuondoa madudu.

Maswali ya kujiuliza Sitta na Mwakyembe 'tuliwasifia' kwa nini hasa? Na kinachofanyika sasa tuna uhakika ndo soluhisho la kudumu? Kama sifa tulizowapa Mwakyembe na Sitta huko nyuma zilikuwa za makosa na hizi sifa tunazo mwaga sasa je? Hivi haiwezekani nchi hii mambo yakaenda bila kiongozi 'kutikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' na 'akamwagiwa' sifa tele?

Nchi zote zenye efficiency viongozi wao huwa 'wanatikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' Kama hapa kwetu?

usisahau pale nilipokuambia kwamba wana ccm ni watu wa ndioooo kwa kila kitu kinachofanywa na kiongozi wa ccm hata kama hakina manufaa kwao
 
Hilo hasa ndilo tatizo langu. Tunajenga mifumo au majina kama kwenye bongo movies?

Na unakuta wale ambao tunawaona ndio 'wasomi' wanashabikia hizi bongo movies pia
kwa ukali..tena...hata ukihoji mtu anakujibu tu 'wacheni watu wafanye kazi'...
as if kuhoji mbinu za ufanyaji kazi ni kumzuia mtu asifanye kazi
Msomi analipa kodi manispaa halafu anaambiwa siku fulani watu mfanye usafi
wala hataki kuhoji hizi tozo na ushuru na kodi wanazokusanya hawa manispaa za nini?
kama hata usafi tuanze kufanya watu wote nchi nzima?
 
Kama kuna watu wa kuogopa hapa Tanzania ni wale wanaojiita wasomi. Yaani wamejirahisi na kujifanya poa kuliko wale wadada wa mitaa ya Ohio.

Hebu angalia wanavyokimbizana na vyama kwa ajili ya pesa za kampeni za uchaguzi ndipo utajua aina gani ya wasomi tulio nao. Bahati mbaya hali iko hivyo kwa karibu nchi zote za Afrika
 
Ndugu jaribuni kutofautisha TPA iliyo wizara ya Uchukuzi na TRA iliyo wizara ya fedha ingawa zote zipo Bandarini
sijui atakuwa ameelewa, kwa nyakati kama hizi saada mkuya, mwigulu wanatakiwa wawe wamewekwa ndani kupisha ucgunguzi
 
Tulikuwa tunampa hongera na sifa nyingi humu Mwakyembe tukisema 'aliisafisha bandari' na ni 'mchapakazi' na wengine wakiomba ateuliwe kuwa Waziri mkuu ili alete Hiyo kasi na uchapakazi lakini tunakumbuka Sitta alipom replace na yeye Sitta akala 'ujiko' wa kuisafisha bandari na kuondoa madudu.

Kumbe in reality hakuna walichokifanya au walichokifanya hakikuwa na manufaa sasa tena sasa tunashingilia Magufuli na Majaliwa 'kuisafisha 'bandari na kuondoa madudu.

Maswali ya kujiuliza Sitta na Mwakyembe 'tuliwasifia' kwa nini hasa? Na kinachofanyika sasa tuna uhakika ndo soluhisho la kudumu? Kama sifa tulizowapa Mwakyembe na Sitta huko nyuma zilikuwa za makosa na hizi sifa tunazo mwaga sasa je? Hivi haiwezekani nchi hii mambo yakaenda bila kiongozi 'kutikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' na 'akamwagiwa' sifa tele?

Nchi zote zenye efficiency viongozi wao huwa 'wanatikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' Kama hapa kwetu?

Wewe kweli darasa la saba hujui tofauti ya mamlaka ya Waziri wa Uchukuzi na Waziri wa Fedha. Ulitegemea Waziri wa Uchukuzi aisafishe TRA? Ana mamlaka nayo? Spurious logic!
 
Bosi alikuwa nani lazima walizimwa kabisa wasitende chochote kuumbua watu hata kama hawakula bosi akisema amesema.
 
Tulikuwa tunampa hongera na sifa nyingi humu Mwakyembe tukisema 'aliisafisha bandari' na ni 'mchapakazi' na wengine wakiomba ateuliwe kuwa Waziri mkuu ili alete Hiyo kasi na uchapakazi lakini tunakumbuka Sitta alipom replace na yeye Sitta akala 'ujiko' wa kuisafisha bandari na kuondoa madudu.

Kumbe in reality hakuna walichokifanya au walichokifanya hakikuwa na manufaa sasa tena sasa tunashingilia Magufuli na Majaliwa 'kuisafisha 'bandari na kuondoa madudu.

Maswali ya kujiuliza Sitta na Mwakyembe 'tuliwasifia' kwa nini hasa? Na kinachofanyika sasa tuna uhakika ndo soluhisho la kudumu? Kama sifa tulizowapa Mwakyembe na Sitta huko nyuma zilikuwa za makosa na hizi sifa tunazo mwaga sasa je? Hivi haiwezekani nchi hii mambo yakaenda bila kiongozi 'kutikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' na 'akamwagiwa' sifa tele?

Nchi zote zenye efficiency viongozi wao huwa 'wanatikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' Kama hapa kwetu?

Ama kweli "BOSS" uelewa wako mdogo sana. Unafananisha mamlaka ya Waziri Mkuu Majaliwa na Rais wa nchi Magufuli na mamlaka aliyokuwa mayo Mwakyembe kama Waziri wa Uchukuzi? Ulitegemea Waziri wa Uchukuzi achukue hatua kama alizochukua Magufuli kumsimamisha kazi Commissioner General wa TRA au alizochukua Majaliwa kuagiza makamishna wa TRA wakamatwe na kuchunguzwa? Hata kama mna chuki binafsi na Mwakyembe (chuki za Richmond na Dowans) basi mlaumu kwa mengine si kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuondoa wizi ndani ya Bandari. Kesi ya sasa si ya wizi wa makontena bandarini, hapana! Makontena yalifika na yakarekodiwa vizuri na TPA kabla ya kukabodhiwa TRA. TATIZO HAPA NI KUWA, KUMBUKUMBU ZA MAKONTENA HAYO HAZIKO TRA, wamepotezea! Sasa Mwakyembe na Sitta wanaingiaje kwenye suala la malipo ya ushuru?
 
Mkuu walisafisha njia ya kupitisha makontena bila kulipa kodi
 
Mh Rais akimuweka Mwakyembe kwenye baraza lake ntamshangaa sana.. Huyo jamaa hana lolote, fisadi na mnafiki tu
 
Timu inapofungwa wa kwanza kubeba lawama ni kocha pamoja na kwamba hachezi acha asimamishwe tu maana hakuna namna
 
Back
Top Bottom