Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe amesema kuwa hakupata kusinzia njia nzima, wakati akisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa treni, kwakuwa anafanya utafiti wake.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa hakuweza kusinzia kwakuwa alihitaji kujiridhisha na hali ya usafiri wa treni na pia kujionea hali halisi ya wananchi wa Tanzania sehemu ambapo treni linapita.
'Nimejifunza mengi sana;ya Wizara yangu na Wizara nyinginezo' alisema Dr.Mwakyembe. 'Nitatumia niliyoyaona kwa maslahi ya Taifa' aliongeza.
Chanzo: Mimi mwenyewe niliyeambatana naye kwenda Dodoma kwa treni...
Nakushukuru, nasubiri kuona matokeo. Ila kumbuka ninasukumwa na uzoefu wa vijisafari kama hivi kutokuwa na tija yoyote hasa katika kada ya viongozi wetu wa sasa, kuanzia kwa mheshimiwa Rais. Huyu amekuwa akizunguka wizara na idara nyingi za serikali matokeo yake amesababisha inefficience kubwa zaidi katika usimamizi wa serikali yetu.
Alikuwapo Lowasa, alifanya ziara nyingi na kutoa maelekezo na maamuzi ya papo kwa papo ambayo hatuoni mwangwi wake ukirindima mpaka sasa. Lowasa alikuwa akifuta leseni za mainginia kutokana na ujenzi mbovu wa maghorofa akiwa site, ujenzi wa maghorofa yenye viwangu vya chini ndio umeshamiri mara dufu sasa.
Huyu Mwakyembe huyu, majuzi kasema hajaenda Bandarini sababu bado anawapa muda wa kujipanga, how many times mr president went there? not less than three times since 2005, nini kimetokea? Nini Mwakyembe Jamani.
Both,Mwakyembe and CCM have to go kama kweli tunataka kuanza kuamini mategemeo ya ufanisi baada ya vijisafari vya namna hii kufanyika.
Nitasubiri Matokeo. Nashukuru.
Sijaona ubaya wa Mwakyembe kusafiri kwa treni.
Hivi utawezaje kuhubiri ubaya wa pombe wakati hujawahi hata kuionja? tusubiri matokeo ya utafiti wake ndipo tuje na kejeri za namna hii.
Achana na Mwakyembe, wewe binafsi hauelewi matatizo wanayokabiriana nayo wasifiri wanaotumia treni? haya, ufahamu wa matatizo hayo unaweza kukusaidi vipi kulikwamua shirika la reli kutoka kwenye mning'inio lililokuwa nao.
Kwa mfano, kuna tatizo la wafanyakazi kutokulipwa mishahara yao, unatatuaje tatizo hili kwa kusafiri kwa treni? miundombinu ya reli imezeeka na haiwezi kuimili safari za mara kwa mara na shehena nzito, unatatuaje na hili kwa kusafiri? kuna tatizo la wafanyakazi kurusha ticketi, unalitatuaje hili kwa kusafiri na treni?
Hii ndiyo bongo bwana; ukifanya ubaya unalaumiwa na ukifanya wema unalaumiwa pia tena kwa maneno ya kebehi.Hapa ndipo nashindwa kuwaelewa watu. Hivi hata mtu akifanya jambo jema kwa kuwa itikadi yako ni tofauti na ya kwake linabadilika na kuwa baya???? Hapa Mwakyembe kakosea nini? Hivi yeye kufuatilia utendaji wa Shirika hili ambalo limekuwa kama ndoo mbovu ambayo kila jitihada za kujaza maji zimeshindikana kutokana na kuvuja nalo limekuwa kosa!!!!!!!!!! You are not serious. Kutokana na kupitia physically masuala yaliyo chini ya Wizara yake anajiweka katika nafasi nzuri ya kutoa maamuzi au ushauri sahihi tofauti na kukaa kwenye kiyoyozi na kungojea kila siku apokee taarifa za walio chini yake ambazo sometimes zinakuwa sugar quoted. Kwa kusafiri na wananchi ni sehemu mojawapo ya kupata mawazo raw from horses mouth. Maana mawazo aliyoyapata hayajachakachuliwa kwa maslahi ya yeyote maana ameyapata live kutoka kwa wadau wa usafiri huo. Hivyo nina hakika amejifunza jambo jipya.
Hongera bro. Mwakyembe keep it up lakini uyafanyie kazi na uyaweke bayana uliyoyaona na jinsi unavyokusudia kuyafanyia kazi.
Mkuu ifikie wakati tujadili hoja na wala sio hizi typing error.Ni wizara mpya nini?? maana zumbukuku hakawii kulala na kuamka na kuanzisha wizara mpya..
Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe amesema kuwa hakupata kusinzia njia nzima, wakati akisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa treni, kwakuwa anafanya utafiti wake.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa hakuweza kusinzia kwakuwa alihitaji kujiridhisha na hali ya usafiri wa treni na pia kujionea hali halisi ya wananchi wa Tanzania sehemu ambapo treni linapita.
'Nimejifunza mengi sana;ya Wizara yangu na Wizara nyinginezo' alisema Dr.Mwakyembe. 'Nitatumia niliyoyaona kwa maslahi ya Taifa' aliongeza.
Chanzo: Mimi mwenyewe niliyeambatana naye kwenda Dodoma kwa treni...
shut up!
Mbona anafanya kazi kwa kutaka coverage kubwa sana ya media? anamaanisha nini