Sn2139
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 834
- 250
Edson,hivi angeenda akapanda treni kimya kimya, akafanya utafiti wake huko njian kimya kimya..kisha akakaa chini kimya kimya na kuanza kuchambua hizo findings zake kisha kuandika report au hata kusema kile alichokiona na nini anatarajia kufanya kuboresha au kudumaza asingeweza kufika huko dodoma?!!
Usisahau kuwa huyu ni kiongozi wa watu na siyo Prof wa Chuo Kikuu anayefanya kazi yake kimya kimya. Huyu ana watu wakingoja kuona, kusikia na kutiwa moyo kuwa matatizo yao yanashughulikiwa. Maneno ya kutia moyo yanahitajika sana na wa-Tz, lakini pia yakifuatiwa na vitendo vilivyobeba dhamira ya kweli kuwatumikia na kuwathamini.
Hata wewe ukiwa kiongozi watu watataka kukuona unavyotenda na unavyozungumza pia.. Halafu baada ya muda watapima maneno yako na matendo yako kama vinafanana.
Naomba tumpe nafasi kwanza hata kama tunachuki naye kwa sababu zozote zile ....