Mwakyembe: Joshua Nassari akamatwa akiwa anataka kuingia bungeni na Chupa ya kilevi akiwa amelewa

Sasa kilichomshinda kumshughulikia that time ni kipi!!?

Yaani, ilitakiwa tuanzae na yeye Mwakyembe kwa kushindwa kufanya kazi yake sawasawa!! Rais ameshasikia .... kama yuko serious basi amuondoe huyu mtu kwenye hayo madaraka. Kama alishindwa kulishughulikia Richmind miaka 10 iliyopita na leo anaadmit tutawezaje kumuamini kuwa anafanya kazi zake sawasawa!! Ten years down the line atakuja kutwambia tuyalete mambo ya Bashite na Nape Bungeni kuyajadili!
Vipi kuhusu hawa vijana wanaoingia wamelewa pombe na bangi, washughulikiwe vipi ?
Kwa Kitwanga Magu alionyesha mfano, je CDM wanavumilia mbunge kwenda bungeni amelewa pombe na bangi ?
 
Mwakyembe ajibu hoja na siyo kukimbilia kwenye konyagi. Kwanini hakumhoji Lowassa wakati yeye anahoji kwanini Tume ya Nape haikumhoji Bashite. Tujuavyo Nassari ni mtoto wa mchungaji, amelelewa katika malezi ya kiroho sana! Nassari aombwe radhi. Au ile sumu iliingia hadi ubongoni?
 
Mwakyembe hebu mshughulikie na yule waziri aliyetuletea mabehewa feki pamoja na kumleta mwekezaji hewa wa treni kutoka Marekani.

Screenshot_2014-10-05-22-27-32-1.png

PG4A2808.JPG
 
Mwakyembe bado kidoogooo ataishiwa kabisa maneno..... Wahenga wanasema, weka akiba ya maneno ili na kesho upate cha kuzungumza.... Sasa huyu yameisha
 
Hahahaahahaha huu uzi utaondolewa soon na mods maana kumsema bashite ni sawa ila kutaja kashfa za wanachadema ni dhambi kubwa. Jana nilianzisha uzi kuhusu joshua nasari na chupa ilitajwa kuwa aliingia nayo, baada ya wanajamvi kuanza kutoa majibu ghafla uzi ukaondolewa....
 
Hivi ni kweli Lowassa alijiuzuru kabla ya ripoti ya Mwakyembe kuwasilishwa bungeni? Kwa hiyo Mwakyembe anataka kutuaminisha kwamba wakati anasoma ripoti ya Richmond bungeni Lowassa alikuwa tayari ameshajiuzuru? Mwakyembe kapoteza kumbukumbu. Ndio maana aliikana hata PhD yake.
 
Mwakyembe ajibu hoja na siyo kukimbilia kwenye konyagi. Kwanini hakumhoji Lowassa wakati yeye anahoji kwanini Tume ya Nape haikumhoji Bashite. Tujuavyo Nassari ni mtoto wa mchungaji, amelelewa katika malezi ya kiroho sana! Nassari aombwe radhi. Au ile sumu iliingia hadi ubongoni?
Nyie watu wanafiki sana, 2020 Mungu atawajibu tu, yaani Nasari anaingia amelewa na bapa pembeni mnaona sawa, Halima anaingia bungeni akiwa amevuta tayari bange zake nyie kwenu huu ndio ufahari ?
 
Kwa hiyo CDM walikuwa wanaamini Richmond ni uonevu ? Huu unafiki unapatikana Tz tu.
Soma vizuri bila hasira na please uwe na kumbukumbu kwenye hili SAGA la Richmond; hakuna sehemu niliposema kwamba Chadema waliona Lowassa kaonewa kuhusu Richmond, rudia kunisoma tena, ni mistari 2 tu wala usiwe mvivu. Mtu wa kwanza kuonesha kwamba Lowassa alionewa wala sio mwingine, ni huyo huyo Mwakyembe; kwa maneno yake mwenyewe na tena ni baada ya yule aliyekua mbunge wa Kigoma mjini bwana Selukamba kumtuhumu yeye na tume yake kwamba ilimuonea, ni Mwakyembe aliyesimama bungeni na kusema yafuatayo, "Waheshimiwa wabunge, lirudisheni suala la Richmond humu bungeni halafu na sisi tuliokua kwenye tume, tutasema hata yale tulioyaficha ili kuokoa serikali yote isianguke" Selukamba alifanya kama alivyo fanya Nasari juzi. Narudia, sijasema popote kwamba Chadema walimtetea Lowassa kwa issue ya Richmond, what I said is, Chadema walimtuhumu Lowasa kwa ufisadi kabla ya sakata la Richomnd halijajadiriwa bungeni. Well, sakata la Richmond bungeni lilikua mwezi February 2008 na Chadema walimtuhumu Lowassa na wengineo (list of shame) mwaka 2007; can't you see that brother?
 
Hahahaahahaha huu uzi utaondolewa soon na mods maana kumsema bashite ni sawa ila kutaja kashfa za wanachadema ni dhambi kubwa. Jana nilianzisha uzi kuhusu joshua nasari na chupa ilitajwa kuwa aliingia nayo, baada ya wanajamvi kuanza kutoa majibu ghafla uzi ukaondolewa....
Haishangazi hilo, mods wenyewe si ndio kina marehemu Isango, ila hili lazima tulishupalie tu, haiwezekana mbunge kwenda bungeni akiwa amelewa pombe, ndio maana wengine wanaishia kutukana matusi ya nguoni kabisa kumbe akili za pombe na bangi.
 
Swala la ulevi kwa wabunge wetu limekuwa tatizo sugu. Hii ni aibu kwa Taifa kuwa na wabunge wasiotambua wajibu wao kwa wananchi. Kuingia Bungeni akiwa amelewa muda wa kazi ni dharau kwa wana arumeru mashariki ambao wamemwamini na kumpa jukumu la kuwawakilisha bungeni. Sioni kama ni sahihi kwa wabunge wa aina hii , wasioheshimu wajibu wao kurudi tena bungeni bunge lijalo.

Mh. Spika tunakuomba uwe unaweka waangalizi kwa wabunge kabla ya kuingia bungeni, ili kuepusha aibu kama hii, na kuligeuza bunge letu kijiwe cha wahuni.
Makonda alikuwa SAHIHI
 
Kama mambo yakienda hivi, hatufiki mbali. Huo ulevi wa Nassari hadi kuliweka bapa kubwa mfukoni na kuingia nalo mjengoni, naona ni utaalam mpya wa kuwafedhehesha watu. Wapinzani, kuweni macho kama sivyo mwaweza kujidhalilisha huko mjengoni. Ona jinsi mlivyonyimwa hata taarifa zenyu. Jueni kuna jambo limefichwa hapo na tulio nje tulitakiwa tusilisikie.
 
Leo Bungeni Dodoma,Joshua Nasari(Mb)Arumeru Mashariki amekatwa na Usalama wa Taifa(TISS)akiwa amelewa huku akiwa na mzinga wa konyagi akitaka kuingia nao Bungeni huku akitokwa na mapovu ya kusema kuwa kamati iliyoundwa na Bunge wakati ule wa Rais Kikwete,kumchunguza Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa juu ya tuhuma za Richmond haikutenda haki kabisa.

Akijibu tuhuma hizo kwa kujiamini kabisa,Mh. Harrison Mwakyembe alisema yafuatayo:

"Kwanza niwashukuru vijana wa Usalama wa Taifa(TISS)kutekeleza majukumu yao hasa ya kumshika Mh.Nasari na chupa hiyo ya Konyagi,maana angeweza kutapikia bendera ya Taifa hivyo kulidhalilisha Bunge lote kwa ujumla...

Kuhusu Edward Lowassa na tuhuma hiyo ya Richmond hawezi kusafishika kamwe kwa hali yoyote ile...Tumeshawachoka sana na hatuwezi kuwavumilia tena....

Kamati yangu iliwahoji zaidi ya mashahidi 75,huku kabla ya kuhojiwa kwake na kamati hiyo Edward Lowassa alikimbilia kujiuzuru ghafla...Sasa bhasi kama kuna mtu yeyote hapa Bungeni anayejiamini alete hoja ya kurudisha tuhuma hizo za Richmond kuhusu Edward Lowassa tuanze kuijadili upya.....

Na siku tukianza kuijadili upya tuhuma hizo,ntamwomba Mh. Rais JPM anipumzishe Uwaziri kwanza ili nimshughulikie kisawasawa Edward Lowassa kisheria zaidi maana wakati ule tuliamua kumwachia tu pasipo kushtakiwa.

Inaumiza sana,waziri mzima na.msomi wa sheria kuongea siasa za kitoto namna hii.
Anasema Lowasa alikimbilia kujiudhuru kabla ya kuhojiwa.....
Huyu ndo mwanasheria wetu na ni waziri alipewa wizara ya katiba na sheria....Lowasa alijihuzuru kabla ya ripoti kusomwa au baada ya ripoti kusomwa?
Huyu mtu ni mwanasheria na ni waziri,kipi kimemshinda miaka yote hiyo kumaliza suala la Lowasa wakati ushahidi anao? Huyu Lowasa ni nani Tanzania mpaka atuingize kwenye matatizo yote hayo na ushahidi upo tena kwa mwanasheria mwenye ngazi ya PHD na anashindwa kumshitaki?
Mh Mwakyembe anatufundisha nn,ni waziri lakini hana uwezo wa kusimamia anachokiamini?
Mwakyembe analeta maswali mengi zaidi ya majibu.
 
Hakuna mtu mnafiki nchi kumzidi huyu mzee, haki ya nani hii political prostitution.
 
mtanzania1989: Kwa kumbukumbu zako, ni kweli kwamba Lowassa alijiuzuru kabla tume ya Mwakyembe haijatoa ripoti yake bungeni? Ni kweli kwamba Lowassa alijiuzuru kabla tume ya mwakyembe haijamaliza kazi yake? Naomba jibu kama unaakili zilizotimia.
 
Soma vizuri bila hasira na please uwe na kumbukumbu kwenye hili SAGA la Richmond; hakuna sehemu niliposema kwamba Chadema waliona Lowassa kaonewa kuhusu Richmond, rudia kunisoma tena, ni mistari 2 tu wala usiwe mvivu. Mtu wa kwanza kuonesha kwamba Lowassa alionewa wala sio mwingine, ni huyo huyo Mwakyembe; kwa maneno yake mwenyewe na tena ni baada ya yule aliyekua mbunge wa Kigoma mjini bwana Selukamba kumtuhumu yeye na tume yake kwamba ilimuonea, ni Mwakyembe aliyesimama bungeni na kusema yafuatayo, "Waheshimiwa wabunge, lirudisheni suala la Richmond humu bungeni halafu na sisi tuliokua kwenye tume, tutasema hata yale tulioyaficha ili kuokoa serikali yote isianguke" Selukamba alifanya kama alivyo fanya Nasari juzi. Narudia, sijasema popote kwamba Chadema walimtetea Lowassa kwa issue ya Richmond, what I said is, Chadema walimtuhumu Lowasa kwa ufisadi kabla ya sakata la Richomnd halijajadiriwa bungeni. Well, sakata la Richmond bungeni lilikua mwezi February 2008 na Chadema walimtuhumu Lowassa na wengineo (list of shame) mwaka 2007; can't you see that brother?
Usicheze na maneno, Mwakyembe hajawahi sema Lowasa ameonewa, Dr Mwakyembe si mnafiki kama baadhi ya CDM. Maelezo ya Mwakyembe yapo very clear, tume yao ilikuwa ni kuchunguza tu na sio kuhukumu, natural justice ipo kwenye kuhukumiwa na sio kwenye kuchunguzwa.

Dr Mwakyembe amerudia mara kadhaa kuwa kama kuna yoyote anayeamini mamvi alionewa walirudisha tena hilo suala bungeni, ni nini kinawashinda hawa wanafiki wa CDM, maelezo ya Mwakyembe ni bunge ndio lilitakiwa limuadhibu EL na Lowasa alikuwa apate haki yake ya kusikilizwa bungeni ila badala ya kutoa utetezi wake akakimbilia kujiuzuru. ACHENI UNAFIKI.
 
Hivi ni kweli Lowassa alijiuzuru kabla ya ripoti ya Mwakyembe kuwasilishwa bungeni? Kwa hiyo Mwakyembe anataka kutuaminisha kwamba wakati anasoma ripoti ya Richmond bungeni Lowassa alikuwa tayari ameshajiuzuru? Mwakyembe kapoteza kumbukumbu. Ndio maana aliikana hata PhD yake.
Nani kasema Lowasa alijiuzuru kabla ?
Lowasa alikuwa na haki yake ya kujieleza kabla ya kuhukumiwa, alitakiwa ajitetee mbele ya bunge ila alishindwa kufanya hivyo badala yake akaamua kujiuzuru, natural justice ipo sehemu ya kuhukumu na sio uchunguzi. Mahakamani lazima upate natural justice ila polisi si lazima na vivyo hivyo kwa tume za kibunge, si lazima wakupe natural justice ila wakishawasilisha bungeni lazima bunge likupe nafasi ya kujieleza.
 
kandawe: Mwakyembe ni mbabaishaji ndio maana alikimbia kuendelea kufundisha pale UDSM inasemekana baada ya kuona wanafunzi wanalalamika kutomwelewa. Kumbuka alifikia hatua ya kuikana kazi yake ya PhD. Yaani hakumbuki hata aliandika nini kwenye tasnifu yake ya PhD. Eti Lowassa alijiuzuru kabla ya kuhojiwa! Wakati sote tunajua kwamba alijiuzuru baada ya Mwakyembe kusoma ripoti yake bungeni. Ina maana alisoma ripoti ambayo ilikuwa haijakamilika? Sasa kwanini alisoma ripoti bungeni kabla hawajaikamilisha?
 
ina maana Nassari anakunywa muda wote kama mheshimiwa Waziri Mkuu wetu Mstaafu wa miaka hiyooo ambaye muda mwingi anapenda konyagi na sigara?!!!
 
Back
Top Bottom