Mwakyembe: Joshua Nassari akamatwa akiwa anataka kuingia bungeni na Chupa ya kilevi akiwa amelewa

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
539
644
Leo Bungeni Dodoma, Joshua Nasari(Mb) Arumeru Mashariki amekamatwa na Watu wa Usalama akiwa amelewa huku akiwa na chupa akitaka kuingia nayo Bungeni.

Mb Joshua alipoanza kuchangia alisema kuwa kamati iliyoundwa na Bunge wakati ule wa Rais Kikwete, kumchunguza Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa juu ya tuhuma za Richmond haikutenda haki kabisa.

Akijibu tuhuma hizo kwa kujiamini kabisa, Mh. Harrison Mwakyembe alisema yafuatayo:

"Kwanza niwashukuru vijana wa Usalama kwa kutekeleza majukumu yao hasa ya kumshika Mh. Nasari na chupa hiyo ya kilevi, maana angeweza kutapikia bendera ya Taifa hivyo kulidhalilisha Bunge lote kwa ujumla...

Kuhusu Edward Lowassa na tuhuma hiyo ya Richmond hawezi kusafishika kamwe kwa hali yoyote ile...Tumeshawachoka sana na hatuwezi kuwavumilia tena....

Kamati yangu iliwahoji zaidi ya mashahidi 75,huku kabla ya kuhojiwa kwake na kamati hiyo Edward Lowassa alikimbilia kujiuzuru ghafla...Sasa bhasi kama kuna mtu yeyote hapa Bungeni anayejiamini alete hoja ya kurudisha tuhuma hizo za Richmond kuhusu Edward Lowassa tuanze kuijadili upya..

Na siku tukianza kuijadili upya tuhuma hizo, ntamwomba Mh. Rais JPM anipumzishe Uwaziri ili nilishughulikie hili suala kikamilifu.

 
Hana lolote Mwakyembe ni njaa tu inamsumbua. Hapo ajibu hoja aache kulalama, eti ibueni tena hoja ya Richmond, kwani yeye hawezi kuibu? Mnataibuaje wakatai hela mshawalipa akina PAP aache kutishia watu nyau.

Gullam Bhai aliyeibua hoja ni Nassari, kuwa Lowasa Alionewa, basi alete ushahidi na suala la Richmond lifuatiliwe kwa umakini na asiye na dhambi asafishwe na alipwe fidia ya kuharibiwa Jina.

Mwakembe amezungumza kwa kujiamini, NA vyama vya upinzani viliunga mkono ripoti ya mkwembe NA kwa kujiamini waliiweka kwenye tovuti Yao NA kumtaja Lowasa kama Fisadi No 1. Sasa kipi kilichobadilika, yaani imewachukua miaka 7 kujua alionewa???
 
Gullam Bhai aliyeibua hoja ni Nassari, kuwa Lowasa Alionewa, basi alete ushahidi na suala la Richmond lifuatiliwe kwa umakini na asiye na dhambi asafishwe na alipwe fidia ya kuharibiwa Jina.

Mwakembe amezungumza kwa kujiamini, NA vyama vya upinzani viliunga mkono ripoti ya mkwembe NA kwa kujiamini waliiweka kwenye tovuti Yao NA kumtaja Lowasa kama Fisadi No 1. Sasa kipi kilichobadilika, yaani imewachukua miaka 7 kujua alionewa???
Nadhani unachanganya madesa, Chadema walimtuhumu Lowassa before Richmond SAGA na Richmond ilipokuja ni kama ili finalize the excise
 
Sasa kilichomshinda kumshughulikia that time ni kipi!!?

Yaani, ilitakiwa tuanzae na yeye Mwakyembe kwa kushindwa kufanya kazi yake sawasawa!! Rais ameshasikia .... kama yuko serious basi amuondoe huyu mtu kwenye hayo madaraka. Kama alishindwa kulishughulikia Richmind miaka 10 iliyopita na leo anaadmit tutawezaje kumuamini kuwa anafanya kazi zake sawasawa!! Ten years down the line atakuja kutwambia tuyalete mambo ya Bashite na Nape Bungeni kuyajadili!
 
Swala la ulevi kwa wabunge wetu limekuwa tatizo sugu. Hii ni aibu kwa Taifa kuwa na wabunge wasiotambua wajibu wao kwa wananchi. Kuingia Bungeni akiwa amelewa muda wa kazi ni dharau kwa wana arumeru mashariki ambao wamemwamini na kumpa jukumu la kuwawakilisha bungeni. Sioni kama ni sahihi kwa wabunge wa aina hii , wasioheshimu wajibu wao kurudi tena bungeni bunge lijalo.

Mh. Spika tunakuomba uwe unaweka waangalizi kwa wabunge kabla ya kuingia bungeni, ili kuepusha aibu kama hii, na kuligeuza bunge letu kijiwe cha wahuni.
 
Back
Top Bottom