Mwakyembe: Hatupo tayari kuburuzwa na Kenya

Mwakyembe: Hatupo tayari kuburuzwa na Kenya

Umesema bahati mbaya akafanywaje eti??????
Najaribu kijiuliza. Hivi kwanini watalii hao wasitumie uwanja wa KIA ili kutembelea Tanzania? Kwanini washukie Nairobi? Inawezekana hatujatangaza vizuri kule Ulaya na Amerika vivutio vyetu na njia sahihi za kupita. Nadhani ndiyo kazi aliyotaka kuifanya Aunty Ezekiel, bahati mbaya au nzuri akadungwa mimba na mheshimiwa! Si vibaya kuanza upya, Promo jamani promo ndio mambo yote.
 
Huku barabarani mbona tunawaona mko bize sana na Ma V8 yenu mpaka sheria mlizoziweka hawazifuati na mahumps mnapanda tu na 140km/h kumbe mnafanya safari raly tu na sio kazi.. JAKAYA KIKWETE HEBU KUWA IDI AMIN AU SADAAM HUSSEIN KWA MIEZI MIWILI TU...
 
halafu huo mkataba jamaa walitakiwa wawe wanalipa usd 1'000, ndio dola za kimarekani elfu moja, kwa mwezi.
sijui kama huo mkataba bado unaendelea


Ule "mkataba wa siri" bado unaendelea for the next 25 years mkuu.
 
Ngoja nikupe mfano: umepewa shoka uangusha mti wa mpingo, wakati unaendelea akaja mtu akakunyang'anya shoka akakupa kisu, je mpingo utaanguka kweli?

Hauwezi anguka mkuu,yaani hii nchi hii sijui viongozi wakubwa wanatumia fikra gani kufanya maamuzi,
 
Kama hizi ndizo akili za watanzania wakenya watatuburuza sanaa...

-Sanaaa...watuburuze mara ngapi mkuu? Mpaka leo hii Kenya zinajengwa barabara za kisasa flyovers nyingi kweli, wana connection kubwa na Marketshare kubwa na mataifa ya nje,angalia viwanda vyao kulinganisha na vyetu,karibu vyakula vyote ambavyo ni processed huku Tz vinatoka kwao.

-Angalia seriousness katika suala la uwajibikaji katika sekta zote.

In deed,we need changes we Tanzanians...japo hatupendi kuukubali ukweli.
 
Leo hii tungekuwa na shirika imara la ndege yote haya yasingelikuwepo...

Kwanini hatuna mpaka leo wakati tulikuwa na vivutio vya utalii vingi sana kuliko Kenya kabla hata ya kupata uhuru? Na fortunately tukapata uhuru kabla ya wakenya lakini leo hii tunawategemea kwa uwanja wa ndege?

Tujiulize.
 
Unachosema ni sawa, ila ukiwa huko nje km amerika,asia, na kwingineko, si rahisi kupata ndege ya moja kwa moja tanzania ,lazima upitie nairobi ,na hatuna hata ndege moja ya tz kwenye viwanja vya huko nje, ni KQ tu zinazotamba, yaani kwa ujumla tumelala kuanzia ndege, kiwanja cha kia, mahotel, yaani tupotupo tu mkuu.

Duh...AIBU KUBWA HII.
 
Najaribu kijiuliza. Hivi kwanini watalii hao wasitumie uwanja wa KIA ili kutembelea Tanzania? Kwanini washukie Nairobi? Inawezekana hatujatangaza vizuri kule Ulaya na Amerika vivutio vyetu na njia sahihi za kupita. Nadhani ndiyo kazi aliyotaka kuifanya Aunty Ezekiel, bahati mbaya au nzuri akadungwa mimba na mheshimiwa! Si vibaya kuanza upya, Promo jamani promo ndio mambo yote.

Ndege wanazokuja nazo hazifiki KIA
 
Hatuko tayari kivipi wakati WAKENYA wanatupelekesha kuanzia kwenye mauzo ya Tanzanite hadi sekta ya Utalii?... Sera Mbovu za CCM ndo MAJANGA kwa Watanzania... ONDOA CCM then Heshma ya Watanzania itarejea kwa kasi .
 
Najaribu kijiuliza. Hivi kwanini watalii hao wasitumie uwanja wa KIA ili kutembelea Tanzania? Kwanini washukie Nairobi? .
ndugu yangu KIA pale kuna connection yoyote ya international flight???hebu lets try to think beyond our capacity
 
Dar es Salaam: SERIKALI ya Tanzania imesema haipo tayari kuburuzwa na Serikali ya Kenya kurekebisha mkataba wa mwaka 1985 unaotoa mwongozo wa ushirikiano katika sekta ya utalii kwa nchi hizo.

Kauli hiyo imekuja baada ya Kenya kuzuia magari ya kitalii yenye usajili wa Tanzania kuchukua na kushusha watalii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata (JKIA).

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema Serikali haiwezi kurekebisha mkataba huo bila kujua namna ambavyo utaleta tija kwa taifa.

“Desemba 22, mwaka jana Kenya ilitoa amri ya kuzuia magari yenye usajili wa Tanzania kuchukua na kushusha wataalii wanaotumia uwanja wa JKIA wakiwa njiani kuja kutembelea vivutio vya utalii.

“Baada ya uamuzi huo, Januari 16, mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu, alifanya majadiliano na Waziri wa Masuala ya Utalii wa Kenya ili kutafuta ufumbuzi wa jambo hilo,” alisema.

Dk. Mwakyembe alisema mkataba umeelekeza maeneo mwafaka kwa ajili ya kubadilishana watalii ukizingatia kuwaondolea bughudha, hususan katika miji ya mipakani pamoja na miji rasmi iliyopendekezwa na kukubalika na pande zote mbili, ikiwamo Nairobi ambako ndipo ulipo uwanja wa JKIA.

“Kwa kuzingatia historia na uzito wa suala lenyewe, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliona kuna umuhimu wa kuhusisha wizara nyingine zikiwamo Uchukuzi, Mambo ya Nje, Viwanda na Biashara, Fedha, Ulinzi, Mambo ya Ndani, Maliasili na Mazingira, pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Uongozi wa Sekta Binafsi ili kupata msimamo wa nchi wa pamoja kabla ya mkutano wa pamoja na Serikali ya Kenya,” alisema.

Alisema hata hivyo, kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili kukutana, Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii wa Kenya, Phyllis Kandie, alimwandikia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Richard Sezibera na kumnakili Waziri Nyalandu kuhusu uamuzi wake wa kurejesha amri ya awali.

Chanzo: Mtanzania

Nimesoma hapa nikajiuliza kama Mwakyembe alikuwa anapiga siasa kama kawaida yetu ni sawa lakini kama aliongea kama mwanasheria na waziri wetu wa EAC ambaye anatakiwa kujenga hoja shawishi ili nchi yetu inufaike na jumuiya hii basi hii kichwa tupu!

Mkataba ulizuia gari zetu kuingia uwanja wa Jomo Kenyatta na mbuga za Kenya. Wakenya walizuiwa kuingia Tanzania na mbuga zetu! Mpaka miaka ya karibuni nakumbuka vizuri gari zetu zikipokea wageni mpakani Namanga. Sijui utaratibu wa kuanza kupeleka wageni mpaka Jomo Kenyatta ulianzishwa kwa misingi gani.

Wanao kumbuka gari pekee kutoka Tanzania zikipokea na kushusha abiria Jomo Kenyatta zilikuwa ni Shuttles za akina Riverside na wengine. Nimesoma juzi ktk gazeti moja hapa,aliye kuwa Mkuu wa Bodi/Shirika letu la Utalii ndugu Richard Rugimbana akisema Wakenya ni kweli wanasimamia sheria inavyo sema,lakini muhimu ni kuwepo mazungumzo pande zote mbili. Na wengine walihojiwa wamekiri gari zetu hazikuruhusiwa kuingia JKIA. Sasa Mwakyembe anasema tunasimamia sheria zipi kama sisi ndiyo tumekuwa tunavunja?

Katika hali hii ya sintofahamu ktk suhala hili napenda kuwalaumu Kambi ya Upinzani. Hakuna mtu anafahamu hii sekta na siasa zake kama Mbunge Mustapha Akunay wa Mbulu,CDM. Ajitokeze asaidie,hawa wakurupukaji akina Mwakyembe ni debe tupu. Mzee Ndesamburo huko wapi? Vyama vya Mawakala wa Utalii mmekaa kimya. Wasaidie hawa wanasiasa wanao fanya siasa za uchaguzi ktk maslahi ya nchi.
 
Undugu tulio nao kati yetu na Kenya ni zaidi ya matakwa ya wazungu.
Hakuna haja ya kumtafuta mchawi katika hili suala bali ni kwa nchi washirika hasa Tanzania kuanza mkakati maalum na endelevu wa kuboresha miundombinu na kutangaza utalii ili hatimaye tuibadilishe hali iliyozoeleka sasa.
Hatubuluzwi bali tunafundishwa njia iliyo bora ya kujidhatiti na mikiki mikiki ya Kibepari katika kukuza uchumi wetu.
 
Mh. Mwakyembe usikubali kusaini mkataba visa ya pamoja ya jumuia ya EA kwani wakenya na wanyarwanda wanataka kutumia resource zetu ambazo wao hawana ili kuendeleza nchi zao. Rwanda hawana vivutio vya utalii ila wanang'ang'ania hiyo visa ya pamoja ili nchi yao inufaike kupitia rasilimali zetu.
 
Mh. Mwakyembe usikubali kusaini mkataba visa ya pamoja ya jumuia ya EA kwani wakenya na wanyarwanda wanataka kutumia resource zetu ambazo wao hawana ili kuendeleza nchi zao. Rwanda hawana vivutio vya utalii ila wanang'ang'ania hiyo visa ya pamoja ili nchi yao inufaike kupitia rasilimali zetu.

Tatizo lako ni elimu ndogo na uelewa mdogo wa dunia na utalii ni nini!! Wenzetu kupitia vitu vidogo ambavyo kwa akili yako ndogo inadharau wameweza jitangaza na kutengeneza pesa! Wanyarwanda kupitia makumbusho za mauaji ya kimbari ni mgodi wa dhahabu utakaoendelea kutema kuliko uwezo wako unavyo weza kuwaza!
 
Obama na wamarekani wenzake watatununulia mashirika yetu ya ndege, hapo ndipo wakenya wataufyata.
Wamarekani wanamkubali sana JK.
 
Hawa wote wamekuwa marais wa Kenya kwa Nyakati tofauti zilizoongozana. Huyo mdogo ndiye wa sasa.
 

Attachments

  • 1423800604907.jpg
    1423800604907.jpg
    42.3 KB · Views: 74

Similar Discussions

Back
Top Bottom