Mwakyembe: Hatupo tayari kuburuzwa na Kenya

Mwakyembe: Hatupo tayari kuburuzwa na Kenya

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,008
Reaction score
64,029
Dar es Salaam: SERIKALI ya Tanzania imesema haipo tayari kuburuzwa na Serikali ya Kenya kurekebisha mkataba wa mwaka 1985 unaotoa mwongozo wa ushirikiano katika sekta ya utalii kwa nchi hizo.

Kauli hiyo imekuja baada ya Kenya kuzuia magari ya kitalii yenye usajili wa Tanzania kuchukua na kushusha watalii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata (JKIA).

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema Serikali haiwezi kurekebisha mkataba huo bila kujua namna ambavyo utaleta tija kwa taifa.

"Desemba 22, mwaka jana Kenya ilitoa amri ya kuzuia magari yenye usajili wa Tanzania kuchukua na kushusha wataalii wanaotumia uwanja wa JKIA wakiwa njiani kuja kutembelea vivutio vya utalii.

"Baada ya uamuzi huo, Januari 16, mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu, alifanya majadiliano na Waziri wa Masuala ya Utalii wa Kenya ili kutafuta ufumbuzi wa jambo hilo," alisema.

Dk. Mwakyembe alisema mkataba umeelekeza maeneo mwafaka kwa ajili ya kubadilishana watalii ukizingatia kuwaondolea bughudha, hususan katika miji ya mipakani pamoja na miji rasmi iliyopendekezwa na kukubalika na pande zote mbili, ikiwamo Nairobi ambako ndipo ulipo uwanja wa JKIA.

"Kwa kuzingatia historia na uzito wa suala lenyewe, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliona kuna umuhimu wa kuhusisha wizara nyingine zikiwamo Uchukuzi, Mambo ya Nje, Viwanda na Biashara, Fedha, Ulinzi, Mambo ya Ndani, Maliasili na Mazingira, pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Uongozi wa Sekta Binafsi ili kupata msimamo wa nchi wa pamoja kabla ya mkutano wa pamoja na Serikali ya Kenya," alisema.

Alisema hata hivyo, kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili kukutana, Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii wa Kenya, Phyllis Kandie, alimwandikia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Richard Sezibera na kumnakili Waziri Nyalandu kuhusu uamuzi wake wa kurejesha amri ya awali.

Chanzo: Mtanzania
 
Najaribu kijiuliza. Hivi kwanini watalii hao wasitumie uwanja wa KIA ili kutembelea Tanzania? Kwanini washukie Nairobi? Inawezekana hatujatangaza vizuri kule Ulaya na Amerika vivutio vyetu na njia sahihi za kupita. Nadhani ndiyo kazi aliyotaka kuifanya Aunty Ezekiel, bahati mbaya au nzuri akadungwa mimba na mheshimiwa! Si vibaya kuanza upya, Promo jamani promo ndio mambo yote.
 
tuna shida nyingi lkn ya kukosa shirika la ndege imara ni kichocheo. halafu mawaziri hawa mbona hawatoi meongozo tuwafanye nn wakenya wanaoingia Tanzania kuleta watalii? au hata wanaokuja kwa shughuli za biashara maana tunawaona wengi na private cars. tukiwatikisa hawa watampelekea wazir wao salam ili ajirekebishe.
 
tuna shida nyingi lkn ya kukosa shirika la ndege imara ni kichocheo. halafu mawaziri hawa mbona hawatoi meongozo tuwafanye nn wakenya wanaoingia Tanzania kuleta watalii? au hata wanaokuja kwa shughuli za biashara maana tunawaona wengi na private cars. tukiwatikisa hawa watampelekea wazir wao salam ili ajirekebishe.

Kama Mwakeyembe ameshindwa kuifufua ATC basi hakuna kiongozi atakaeweza tena kuifufua🙁
 
Asante kwa kuzungumza kidplomasia with authority behind. Nyalandu aliingia choose cha like unaamua mkataba watu 2. Sifa ya kiongozi ni utulivu na kufanya maamuzi ya kimfumo. Kenya watch out .. Thanks pia kwa Zito kabwe..
 
Hii ndio gharama ya kuwa na jirani mnafiki! Anayetaka kila siku apate yeye tu. Ukipata wewe anaanza visa na mikasa. Tumekataa na ardhi yetu na tumegoma kutumbukizwa katika sakata la Somalia. Tumestuka! Kwa hatua ya dharura, tuzungumze na Waethiopia watuletee watalii wetu moja kwa moja Tanzania, endapo ni kupitia JNIA, KIA, Arusha au Zanzibar. Jamaa wana ndege karibu 100 hivi sasa. Kuna umuhimu wa kuimarisha uhusiano wetu na Wahabeshi hivi sasa. Wakati huo huo, hili ni fundisho kwa viongozi wetu kuona umuhimu wa kuifufua ATC, tena haraka! Majirani gani wana wivu kama nini! Hizi zote ni hasira za kuona Watz tunaanza kuwapiku kwa idadi ya watalii na uchumi kwa ujumla--The giant has awaken! Mungu anawalaani hivi sasa unafiki wao unaibuka hadharani baada ya kujificha kwa muda mrefu!! Namuunga mkono waziri wetu--hatuko tayari kuburuzwa na Wakenya!
 
For this I support Kenya 100%. Why? Hawana muda wa kuchekacheka.

Serikali ya Tanzania badala ya kuchukua hatua kali na madhubuti wanabaki kulalamika, kulaani, kunywea na kubembeleza. Poor Tanzania.
 
Asante kwa kuzungumza kidplomasia with authority behind. Nyalandu aliingia choose cha like unaamua mkataba watu 2. Sifa ya kiongozi ni utulivu na kufanya maamuzi ya kimfumo. Kenya watch out .. Thanks pia kwa Zito kabwe..

Hapa ndipo ujinga wa watanzania umejikita. Diplomasia!!! Umaskini na diplomasia wapi na wapi. Tanzania imekuwa nzito kuchukua hatua kisa inasubiri Diplomasia. Siku zote diplomasia ni dalili ya woga. Diplomasia iko kuchelewesha mambo huku busara ikingojewa na wala diplomasia hauko kuleta maendeleo.

Sasa wakenya wameshamwaga ugali, Tanzania inasubiri nini tena?
 
Hivi jirani akikuzuia usiende nyumbani kwake unamshitaki mahakamani? Jirani yako akijenga fence kuzunguka nyumba yake unampeleka polisi? Tanzania tuna uwanja wa kimataifa wa KIA, ni kwa nini watalii wang'ang'anie kushukia Nairobi. Tuna viongozi tena wasomi, tuna wachumi wazuri waliobobea, tuna wanasheria makini wameshindwa nini wote hao kutegua kitendawili wanachotegwa na Wakenya. Wahenga walikuwa na busara pengine kutuzidi hata sisi, walisema jirani usimpe samaki bali mpe nyavu. Sisi tumezoea vya bure, bajeti yetu ya kila mwaka ni tegemezi, tunapita huko na huko kuomba misaada. Namna pekee ya kutufanya tujitegemee ni kwa wafadhiri kutunyima misaada, kwa sababu ni lazima tuishi viongozi na wachumi wetu watatumia akili na usomi wao ili tuishi. Ili uwanja wa KIA uweze kufanya kazi kwa kwa kiwango cha juu na kupata faida lazima Kenya watuzuie kuingia kwao ili tujenge miundombinu kwenye viwanja vyetu itakayokubalika kimataifa. Nchi hii sasa hivi kila mtu analia na kuwalaani Wakenya kwa kukutuyzuia tusiende kwao, na sisi tuwazuie wasije kwetu kama tuna ubavu. Juzi hapa tunaambiwa pale JK Inter. Airport serikali imeamua kujenga jengo kuboresha miundombinu, Jengo lililogharimu bilioni 12 baada ya tathimini ya kina limeonekana kugharimu bilioni tatu, bilioni tisa watu wameweka mifukoni mwao serikali iko kimya lakini inalia lia kwa Kenya kutufungia milango. Kwa nchi zilizo serous na utawala wa sheria saa hizi wahusika wote kama hawajafika jela basi wako mahakamani na hakuna dhamana kwa sababu huo ni uhujumu uchumi. Serikali yetu kama ingekuwa serous ikaokoa zile bilioni tisa zilizofujwa pale JKIA na kuzitupa zote KIA sasa hivi KIA ingekuwa bora kuliko uwanja wa Nairobi na kilio hiki kisingekuwepo. Tunahitaji viongozi wenye mtizamo wa kimapinduzi
 
hivi ukishazoea kuangalia tv kwa jirani, leo akiamua anaenda kulala mapema utasema amekuonea kweli, pale ni kwake na ana uhuru wa kufanya anachotaka, hata kama mna uhusiano wa karibu kivipi. nunua ya kwako ili uwe huru nayo,
 
Najaribu kijiuliza. Hivi kwanini watalii hao wasitumie uwanja wa KIA ili kutembelea Tanzania?

Ndege ngapi zinatua KIA? Customer service ipoje pale?

Kilimanjaro Airport Passenger Reviews and Kilimanjaro Airport Customer opinion

24 June 2010 by Adam Simmons (Spain)

Compared to so many airports, a delightful experience. I was first off my arriving flight and so did not have to queue for a visa. Only one person was doling them out so I guess that stragglers had quite a wait. On departure, plenty of shops for such a small airport, with plenty of seating, both indoors and out. no problems in either direction with passport or customs.

25 May 2010 by Ravi Mene (UK)

Used Kilimanjaro as our entry point for Tanzania's northern safari circuit, KLM was the only flight arrival at the time, the airport though small had the fresh feel of yester years relaxed airports, walking to arrival area ushered by ground staff, No soulless airbridges and automatic sliding doors leading to empty spaces!! The whole ambience was relaxed, Immigration was quick and efficient, they had a green and red channel, when tried to walk through green channel, were asked (politely) to go through red, were asked a few cursory questions and waved through, total time from disembarkation from the airplane to the waiting car less than 20 minutes!! The charm of this airport is that it is not like the other mega airports, small and fresh.

28 April 2010 by Anne Linney

Another charming African airport where you can bribe your way into any area of the airport and where power cuts tend to be a problem and staff have to run to the generator to get lights back on. Surprising that KLM actually lands here, no other western airline company does such a thing.

29 September 2009 by M Ford

Small, clean, basic. One of your contributors mentions a corrupt customs official in 2007. There are now serious problems with customs officials there who take one into a room and will not be satisfied until a bribe has been paid. This is not just if one has gifts or items disallowed on the Exemption Schedule of the Customs Tariff Act. Anyone is likely to be their victim and they are very persistent and intimidating. Something should be done.

Kilimanjaro International Airport by M Ford: 29 September 2009

Small, clean, basic. One of your contributors mentions a corrupt customs official in 2007. There are now serious problems with customs officials there who take one into a room and will not be satisfied until a bribe has been paid. This is not just if one has gifts or items disallowed on the Exemption Schedule of the Customs Tariff Act. Anyone is likely to be their victim and they are very persistent and intimidating. Something should be done.


Kilimanjaro International Airport by Benjamin Arksen: 3 August 2007

A very small airport, definitely not a hub, but shops are decently-priced and have beautiful souvenirs. If you climb KiKilimanjaronjaro, then don't bother buying any souvenirs at the moutain itself, as the airport shops have basically the same shirts and etc, and the prices are unnegotiable.

Kilimanjaro International Airport by Ingvar Backéus: 5 February 2007

A lot of tourists travel nowadays through KiKilimanjaronjaro International Airport (JRO; usually called Kia). It is a fairly small airport with international flights mainly by KLM and Ethiopian. The travel from the airport to Arusha town takes nearly an hour; the smaller town of Moshi is closer. A taxi to Arusha should cost USD 50-60. KLM arrives in the evening and security along the road to Arusha has sometimes been poor. At some time passengers even travelled to Arusha in a convoy. At present situation seems to be under control. There are some decent tourist shops, both before and after immigration, actually more shops than one would expect considering the low number of flights. I have travelled through this airport many times during the last 15 years. Considerable renovation in the check-in area has taken place a few years ago and it now looks fresh. Toilets do not always work – a common phenomenon in Africa. Some years back I had at several occasions considerable problems with a corrupt customs officer who wanted something under the table for obviously no good reason, but that person has disappeared and the last few years customs checks have been quite relaxed. Getting a visa at the airport is rather straightforward but since usually a good number of people come without a visa, one has to expect some queuing; having the visa ready is recommendable.

Kilimanjaro Airport Reviews | SKYTRAX
 
Zanzibar-ASP

Chunga lugha yako bro.! Sio kweli kwamba viongozi wote na Watanzania wote ni wajinga. Lugha yako inautia shaka sana Utanzania wako!!
 
Last edited by a moderator:
Mgeni aliyechagua kuja tanzania atakuja tuu! Tukiachana na kupeleka wageni kenya mashirika ya ndege ya nchi nyingine yatafanya option muafaka! Au wageni hao watafanya option za kuwafikisha watakako. Cha msingi create a problem to solve a problem!
 
Tangu sakata la ESCROW hata sasa ndio nimegundua madhara ya kuwa tegemezi. Wazungu walipo gomea tu kutoa misaada kelele zikawa nyingi eti wanaonea wanyonge wengi!!! Hili la Kenya nalo viongozi wanapiga kelele ati Kenya inawaonea!!! hivi sisi kama nchi tumefanya jitihada gani kuhakikisha tunapunguza utegemezi???
Hakika serikali yetu ingekuwa Inafanyiwa evaluation by objectives hakika tusingekua katika aibu hizi!!! Tukianzia wizara ya maji,elimu,uchukuzi,viwanda,utalii,ardhi,viwanda nk. zooooote hizo ni usanii tupu unaofanyika huko. leo hii ukiuliza wizara hizo waliweka objectives ngapi na wametekeleza ngapi kwa 100% hutapata hata 1 hakika!!
Tuna tatizo la kimfumo na hilo halipingiki, kwani hata kiongozi mkuu hajui anataka aifikishe wapi nchii kimaendeleo. Hatujapiga hatua za kuridhisha kisiasa,kiuchumi na hata kitechnolojia tupotupo tu tunamangamanga!!!
Unless mfumo unabadilika,tutaendelea kushikwa sharubu mpaka tupate akili!!
 
ccm zile za escrow wangejenga viwanja vya ndege vya kisasa hawa wakenya wangetudharau hivi
 
hivi ukishazoea kuangalia tv kwa jirani, leo akiamua anaenda kulala mapema utasema amekuonea kweli, pale ni kwake na ana uhuru wa kufanya anachotaka, hata kama mna uhusiano wa karibu kivipi. nunua ya kwako ili uwe huru nayo,


ndio.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom