Sugu na Mwakyembe wote wanatoka mbeya, ila mbunge wa mbeya wa mwnanchi wote ni Sugu.
Mwakyembe kibaraka cha ikulu, sugu ni kibaraka cha wana mbeya,
PHD za Tanzania hazina maana maana kila phd holder hajiamini, kulia lialia tuu walau maisha yaende
Ukitaka ujue Phd ya Mwakyembe ni ziro kabisa kabisa akose ubunge na uwaziri. Hata vimiradi vyake vitakufa kifo cha mende.
Sijawahi kuona msomi mwenye majivuno kama Mwakyembe japo kwa kweli hajalitendea chochote taifa hili zaidi ya kununua Mabehewa feki.
Sijawahi kuona Msomi mwenye jaziba na chuki kama Mwakyembe.
Msomi asiyejua kuzuia jazba,hasira na chuki ni mpumbavu. Kudhibiti jaziba ni kipaji na hekima toka kwa Mungu.
Ukiangalia serikali hii ya awamu hii imejipanga kitaaluma lakini karibu wate hawana busara ,hekima ,uvumilivu na uvumilivu.
Tanzania tuna amani kwa sababu ya kuwa na uvumilivu na hekima sio kwa sababu ya elimu.
Tena Mwakyembe na wengine wenye dharau na kila maneno ya ushuzi kama hayo wafahamu tu kuwa kama hii nchi kila mtu angekua msomi kwa kiwango cha Form four tu basi huu utawala waajabu ajabu wa CCM kwa miaka 50 ungekua umeshaondolewa kwa nguvu ya umma.
Mwakyembe amesahau kuwa ujinga wa watanzania na kukosa kwao elimu ndio mtaji wake na Chama chake.
Sijawahi kumuona Mwakyembe kama msomi muhimu kwa taifa hili zaidi ya mtu aliyeranikiwa tu kibinafsi na familia yake,jambo ambalo lipo kwa kila binadamu anayehangaikia maisha yake.
Kupigania jamii ni kazi ngumu sana.
Mandela hakuwa Phd holda ,hata Sokoine aliishia form two lakini alikua ni muhimu zaidi kwenye taifa hili kuliko maprofesa wengi waliosoma kwa lengo la kuongezewa tu mishahara makazini mwao.