Kwanza kabisa hakuna shule inayofundisha busara, alafu pia kigezo cha mtu kuongoza watu sio elimu bali ni hekima. Hivi kati ya sugu na mwakyembe nani anayewaongoza wajinga?
Msomi wa sheria asiyejua kuwa Uchaguzi wa marudio Zenj haukuwa halali kisheria!!
.........mtu akificha ukweli anaoujuwa na watu wakajuwa kuwa kauficha na anajuwa watu wamejuwa kuwa anaujuwa lakini kauficha na bado akaendelea kuficha kinachojulikana, hataaminika hata pindi akinena lililo la kweli. na hapo ndipo hata mfalme huanguka.
Mwakyembe yupi, au ni Harrison huyu waziri wa sheria aliyeomba mwongozo wa hovyo juzi kuhusu wabunge wa upinzani kunyimwa posho? Kama ni yeye afadhali hata ya Sugu ana uwezo wa kujenga hoja. Mawaziri walio wengi wa CCM ni mizigo.
Mwalimu wa sheria asiye jua sheria,
rejea posho za wabunge wa UKAWA
Atakumbushwa suala la vichwa vya treni na madai yake CCM walitaka kumkolimba
Jamaa feki
Hana lolote huyo kasoma nini Yeye? Usomi huo wa kifisadi una faida gani kwa Taifa? Kule Airport alipiga 10% Ujenzi wa majengo mapya na Treni toka mjini hadi Airport, Bandarini alipiga Dili kibao akapenyeza Ukabla akawaajili ndugu zake kibao, PhD za kununua mabehewa Feki, kuchakachua reports ya Richmond hizo zina manufaa gani? Mbona Dr Slaa na prof Lipumba ni Wasomi lakini walirubuniwa na Div four Nape Nnauye pia Div zerooo form six January Makamba, Wanaojiita Wasomi CCM wote ni Mafisadi angalia tabia za Chenge, werema, Tibaijuka, Kapuya, mbilinyi, ngereja na wenzao zinafanana na Tabia za Ally kessy?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.