Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 21,854
- 26,094
atcl ina ndege 1 inayoimiliki na wafanyakazi 300 wanaoitegemea ndege hiyo :bange:
Isijekuwa ndege za kichina, maana inasemekana ni rahisi kwa bei!Dk. Harrison Mwakyembe ameliambia Bunge punde tu kuwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) litanunua ndege mbili mpya katika mwaka ujao wa fedha.
Katika maelezo yake hajaweka wazi hadi sasa ATCL ina ndege ngapi zinazomilikiwa kwa asilimia 100 na shirika hilo mbali na kuzungumzia ndege kadhaa za kukodi.
Najua JF ina wajuvi wengi, mwenye taarifa hizi atiririke hapa tujue!
Tutanunua ndege
Tutanunua meli
Tutanunua vichwa vya treni.
Halafu wizara yake itaishia kupewa 25% ya budgeted amount for 2014/2015 fiscal year ataishia kuuchuna kimyaaa, akiulizwa mwakani ndege mbili ulizoahidi ziko wapi? Ndio ataanza blah blah zao ooh!!! Wizara ilipewa 25% ya pesa ilizoomba hivyo tukashindwa kununua ndege kama tulivyoahidi kwenye kikao cha bajeti kilichopita.
Tutanunua ndege
Tutanunua meli
Tutanunua vichwa vya treni.
Kweli Tanzania ni nchi ya ahadi. Kuahidi ni jambo la kawaida
Mkuu nasikia Lusajo ni mjomba wake kabisa na anavurunda sana ila ndo kamkabidhi shirikaMwakyembe namuheshimu sana..kuna baadhi ya mambo anajitofautisha na mawaziri wengine wa CCM,ila ktk hili huyu Mnyakyusa anapiga tu siasa hakuna uhalisia.
Mwaka jana walikuja na porojo hizo hizo,lkn mwaka umeisha bila kuwa na matokeo chanya,ATCL inamiliki ndege moja tu aina ya Bombadier DH8(?)5H-MWF,Baada ya ile moja kupata Snug kule Kigoma na wajanja wakala malipo ya bima na hawajanunua nyingine.
Baada ya kuona Bunge la Bajeti linakaribia Wizara na ATCL wakaamua kwenda kukodi(lease)ndege nchini Kenya,aina ya CRJ-200 kwa ghalama kubwa,na waliokodisha wakakataa ndege yao usiwekwe twiga wetu wala Registration ya Kibongo(Tz),walichoruhusu ni kuandikwa kwa Jina la "Air Tanzania-The Wings of Kilimanjaro",ndege imebaki na Reg ya Kenya ya 5Y-WWA,marubani wao,Air hostess wao na hata Engineer ni wao.
Juma lililopita Serikali ilipoona inakaribia kusoma bajeti ya Wizara ikaanzisha Route ya Dar-K'njaro-Znz,hii ni kuhadaa tu watu kuwa shirika lao pendwa ATCL lipo "hai";na kiukweli shirika hili linapendwa sana na Watz,hata liwe na kandege kamoja ka magumashi bado watu watakata tiketi na kupanda,kwa ndege hizo mbili moja ya kukodi na moja wanaomiliki ATCL inafanya safari za Dar to Mwanza,Dar to K'njaro,Dar to Hahaya,Dar-Kigoma-Bujumbura.
Waliingia mkataba na mwarabu wa Oman,lkn Omana akataka jengo la ATCL kwa miaka 90,wakaenda kwa Mchina napo wakashindwana,hizo tetesi za kuleta ndege mbili hazijaanza leo,toka mwaka wa jana wa pesa...waalisema wataleta Bombadier CRJ-900,lkn kimya na wamekuja na story nyingine...Usaniii mtupu.
ATCL ilikufa kifo cha membe pale "wahuni"wachache walipoihujumu,KLM ilitaka kuingia ubia na ATCL lkn wahuni wachache wapenda 10% wakapotezea dili...KLM akaamua kuingia kufanya kazi na Kenya Airways(KQ),leo hii Wakenya wapo juu sana,wanamiliki ndege aina ya E190 za kutoka Brazil za kutosha,wana B767.,B737,B738 na mpaka sasa wamevuta B777-200(?).....Pale waziri mwenye dhamana ya shirika wakati huo alipoamua kujiingiza ktk biashara ya usafiri wa anga ndipo shirika letu lilipokufa rasmi,hakuwa tayari kuona National Carrier inakua zaidi ya shirika lake na la wabia wenzake.
Leo wanataka kulifanya shirika lao binafsi kama ndio National Carrier....jawabu la kurudisha ATCL ktk hadhi yake,ni kama sbb zile zile za kuirudisha Tz ktk ramani yake.....KUIONDOA CCM NA VIBARAKA WAKE MADARAKANI
safi mwakyembe keep going
halafu wizara yake itaishia kupewa 25% ya budgeted amount for 2014/2015 fiscal year ataishia kuuchuna kimyaaa, akiulizwa mwakani ndege mbili ulizoahidi ziko wapi? Ndio ataanza blah blah zao ooh!!! Wizara ilipewa 25% ya pesa ilizoomba hivyo tukashindwa kununua ndege kama tulivyoahidi kwenye kikao cha bajeti kilichopita.
Vipi hajazungumzia wizi unaoendelea bandarini?
Alitudanganya kuwa amekomesha wizi wa mizigo,na kukwapua vitu kwenye magari ya wateja.
Lakini hivi karibuni jamaa zangu watatu wote waliopitisha magari yao bandari ya Dar es Salaam ,wamekuta sreen imenyofolewa,mmoja wamekomba jeki,mwingine wameina spare tyre na kumuwekea ambayo imesha kwisha.
Tanzania tumeoza kila kona,acha kagame atudharau.