Naomba nikusahihishe ili kuondoa upotoshaji. Mwakyembe hajatamka: "Ndiyo tatizo la kuchukua data kwenye JamiiForums", bali ametamka:
"...hilo ndio tatizo la kutegemea sana JamiiForums"; binafsi sioni ubaya wa kauli hii kwani mbali ya kupata habari JF au chanzo kingine chochote, ni vizuri to verify na vyanzo vingine kabla haujawa na uhakika na unachokisema. Vinginevyo Dr. Mwakyembe ni dhahiri anaheshimu sana JF kama chombo cha habari na hii ilidhihirika wakati ule anaugua.
Nimeisikia hiyo... sema Ngoja wadau wapite kwanza..Akijibu swali la Wenje, Mwakembe amesema kwamba taarifa zake si za kweli, "Ndiyo tatizo la kuchukua data kwenye JamiiForums."
Ni mara ngapi?na ni data zipi ziliwekwa jamii forum ni za uongo??
mh mwakyembe ameikejeli JF wakati akijibu swali la Wenje.
Amesema ukitegemea sana JF unaweza kuwa na hbr ambazo uhakika ni mushikeri
wengine walisha jifia kiakili...Maadui wa JF wanazidi kuongezeka.
Hajui atendalo, angejua kuwa kupona kwake kuna mkono wa JF angeishukuru na kuichangia mara dufu!
Jf ndio iliyofichua njama zote za jaribio la yeye kuuawa na kila aina ya hila dhidi yake lakini leo anaiona si chochote?
Aje ajiunge huko tumpige msasa huyo!