Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakiembe
Waziri Mwakiembe amepiga marufuku magari ya abiria kulazimishwa kuingia vituoni kwa lengo la kulipa ushuru kwenye vituo vilivyoandaliwa na halmashauri za miji. Amesema njia hiyo husaidia kukuza rushwa na pengine kuchelewesha safari za mikoani.
Waziri Mwakiembe alifanya safari ya kushtukiza kituo cha mabasi cha Ubungo. Alisema malalamiko ni pamoja na kwamba hata mabasi kama hayateremshi au kupakia abiria hulazimishwa kupitia vituo hivyo na hivyo kuchelewesha safari za abira na pengine kusababisha kushimiri kwa rushwa.
Moja ya vituo vinavyoleta usumbufu huo ni Ubungo, Mbezi, Kibaha, Morogoro, Iringa, Mafinga, Nzega, nk.
- Binafsi nilishuhudia mara kadhaa nilipotumia usafiri wa basi niliposafiri kwenda mikoa ya Kusini Nyanda za juu ucheleweshaji na usumbufu wa kupitia vituo ambavyo nilishuhudia hakuna abiria aliyeteremka au kupanda ni Kibaha, Iringa, na Mafinga.