Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
- Thread starter
- #21
Ni habari nzuri hii CS.
Kinadharia inatakiwa ieleweke kwamba kwa abiria kulipa nauli ya mabasi na zingine za vituoni humo mabasi yanakuwa yamekwishalipia gharama za kutumia vituo hivyo.
Mheshimiwa Mwakyembe anatakiwa atume wasomi watembelee nchi za wenzetu na waangalie namna vituo na viwanja vya ndege vinavyoendeshwa bila mizengwe wala husda.
Kwa wale walio nchi kama za UK kunavituo vingine vya mabasi ni vidogo sana kama kituo kimoja kinaitwa Golders Green kilichopo kaskazini mwa jiji la London. Kituo hiki ni kidogo sanalakini kinachukuamabasi mengi sana yanayosafari mbali pia lakini pana mfumo unaoeleweka.
Lakini tatizo kuna watu wanafika kutembea nchi za wenzetu wakiwa na nafasi ya kujifunza lakini wakirudi nyumbani hakuna kitu.
Hivi ile ziara ya Askari wa Usalama barabarani kule Ujerumani imewafundisha nini askari wetu? maana Ujerumani inaongoza kwa mfumo bora wa barabara Ulaya.
We vipi? Wenzako ni mashindano ya kuvaa suti waendapo nje ya nchi. Karibuni hivi nilipata kuvunjika mbavu ndani ya ndege jamaa anavyojipitisha na suti kutoka isle hii hadi nyingine huku inaonekana kama kaipachika kwenye mkwaju vile. Anaonekana ilikuwa awamu yake ya kwanza kukwea pipa kwenda huko ughaibuni. Hawanaga ile kitu kujifunza kwa wayaonayo bali kushangaashangaa tu.
Wewe na wengine wengi wamejitahidi kuwapa hapa darasa lakini hawafunguki, tatizo ndio hili elimu imewapiga kumbo. Wenyewe wanachofikiria ni kutundika shahada majumbani hata zilizo feki kumbe elimu si shahada. Wengi wameelimika kwa kufungua akili na mioyo yao kujifunza kwa kuona na wamefanya makubwa kuiga waliyoyaona. Wao wanafikiri ni vyeti. ndio haya sasa ya kupeleka sekondari wanafunzi wasiojua kusoma na kuandia na walimu kuanza kuwafundisha madarasa ya chekechea.