trachomatis
JF-Expert Member
- Jun 7, 2011
- 3,758
- 746
Hivi kwenye hiyo tume alikuwa peke yake mpaka aandamwe yeye tu?? Binafsi cant buy that unless kuna kitu kingine ambacho hakisemwi. Yeye alikuwa Mwenyekiti tu wa hiyo kamati ambayo ilikuwa na wajumbe wengine. Sasa inakuwaje wajumbe wengine hawajui kile anachokijua Mwakyembe?? Labda mseme kuna uchunguzi aliokuwa anafanya bila kuwashirikisha wenzake!!
jamaa hali yake ni tata sana maana ngozi inatoa vumbi mzee..
acha uongo ulienda India kumwona!?
Ndugu wana jf, heshima kwenu. Siku chache zilizopita tumesikia ujio wa Mwandosya, sasa naomba mwenye updates kuhusu Mwakyembe. Hali yake kwa sasa iko vp? Je, ugonjwa gani unaomsibu na nini chanzo chake? Natanguliza shukrani.
anaendelea vizuri sana katoka hospitali yupo hoteli kwa uangalizi zaidi na karibuni atarudi na akirudi anaziujuli ubunge na uwaziri! anarudi kwenye fani yake ya kufundisha na uwakili na huko huko ataendelea kuwasema mpaka kieleweke
Nimetokwa machozi nilipoona picha ya Mh Mwakyembe gazeti la mwananchi ya leo akizungumza na Sitta akiwa bado hosipitalini. Mwli wake umekuwa kama nyoka. Kama ni watu walimpa sumu ili watu wapate madaraka walaaniwe
Picha kubwa: https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=41762&d=1321869350
Ni kweli kabisa tunatakiwa tumsemee mazuri hasa wakati huu anapougua lakini mimi watu wanafiki huwa siwasemei mazuri aslani, mtu anawajua waliohusika lakini akirudi utamsikia anawasifia kama Mwandosya anavyofanya, kama mtu ameamua kufa na tai shingoni mwacheni mwenyewe na Mungu wake.......issue ya Mwakyembe ni tata, tunatakiwa tumsemee mazuri kwa vile anaumwa, vinginevyo waliohusika na yeye, walijipanga, huo ndio ukweli.
Si muumini wa hicho kitabu, lakini kusoma kwa dhati ya moyo na Mungu alietajwa humo ndani ya kitabu basi inategemea na usafi wa mtu alietendewa hayo! sasa inategemea na Ndugu Mwakyembe ni msafi kiasi gani ili Mungu nae amsikie, ispokuwa ninachojua, Mungu ni mlipaji, yeyote alofanya hivi basi kama hili halikumkuta yeye basi ni wazi vizazi vyake vitalipizwa, hakika wajue wote walofanya hivi wamejitengenezea dhimma kwa Mungu alie juu na ipo siku atalipiza japo wale walotenda watasahau, kwenye Quraan Mwenye Ez Mungu Sub-hana wa Taala anasema kuwa "MWENYE EZ MUNGU HATOBADILISHA KAULI YAKE MPAKA MBADILISHE YALE MLOTANGULIZA KUYAFANYA KWA MIKONO YENU" sasa hata yasipowakuta wao basi jua wazi waoto wao yatawafika tu....Kweli inauma sana, ila kama kuna wanafamilia wa Mwakyembe anasoma hii comment naomba muwe mnasoma zaburi 35 kila siku mpaka atakapopona, zaburi ya 46, na 109, hii ni kwa ajili ya mgonjwa na pia ni njia nzuri ya kuwashughulikia maadui zenu.
Ingekuwa vizuri kama mke wake angekuwa anasoma. Mgonjwa mwenyewe awe anasema haya maneno kila siku Maombolezo 3:22-23, Yakobo 5:15-16, Zaburi 20 yote.
Awe na moyo wa kusamehe yote, hakika Mungu atauokoa uhai wake na kaburi. Maana imeandikwa katika Marko 16:18b hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa.
I hope anybody who is closer to this family will take this very seriouse. Hulituma neno lake lipate kutuponya na kututoa katika maangamizi. I will keep praying for him