Mwakyembe ajitoa mhanga, Mongella afyatuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe ajitoa mhanga, Mongella afyatuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 28, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,359
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Basil Msongo;
  Tarehe: 27th July 2009

  Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ameitaka Serikali iufunge mara moja mgodi wa dhahabu wa North Mara ili sumu inayodaiwa kutoka hapo isiendelee kuwadhuru wananchi.

  Mbunge huyo pia ametaka mgodi wa dhahabu wa Geita ufungwe kwa sababu, kwa muda mrefu umekuwa ukitoa kemikali za sumu zinazowadhuru wananchi wa kijiji cha Nyakabale.

  “Kwa nini tuogope wawekezaji kama wakwe?” amehoji Mwakyembe na pia kuuuliza kwa nini vifungu vya mikataba havitumiki kuwabana wawekezaji.

  Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kuwa mgodi wa North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara umekuwa ikimwaga maji yenye sumu katika mto Tigithe.


  Kwa mujibu wa madai hayo, wananchi 21 kati ya waliyoyatumia maji hayo wamefariki dunia, wengine wamekumbwa na matatizo ya kiafya, na pia mifugo 200 imepoteza maisha.

  Kampuni inayoendesha mgodi huo, Barrick Tanzania, imekanusha taarifa hizo kwa madai kuwa polisi kwa kushirikiana na mamlaka za Wilaya ya Tarime zimefanya uchunguzi na kubaini kuwa hakuna uthibitisho wa kuwapo kwa madhara hayo.

  Dk Mwakyembe amesema, anafahamu kwamba, kampuni inayomiliki mgodi wa North Mara, Barrick, ni kubwa zaidi kwa uzalishaji wa dhahabu duniani na ina nguvu kubwa lakini hawezi kukaa kimya wakati wananchi wanaathirika na lazima hatua zichukuliwe.

  “Hii nchi ni yetu, tutaongea kwa ujasiri tu” Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2009/2010.

  Kwa mujibu wa Mbunge kampuni ya Barrick ina rekodi mbaya ya kuharibu mazingira.

  Kampuni ya Barrick Tanzania inaendesha migodi minne nchini, Bulyanhulu, North Mara, Tulawaka, na Buzwagi.

  “Pamoja na mapenzi yetu makubwa kwa wawekezaji lazima hatua zichukuliwe” amesema Dk Mwakyembe na kupendekeza kuwa wananchi waishitaki kampuni ya Barrick.

  Mbunge huyo amesema, wabunge wa maeneo ulipo mgodi huo washirikiane na wananchi, wanaharakati na wanasheria kufungua kesi mahakamani kuishitaki kampuni ya Barrick kwa kuwa maneno ya majukwaani hayawezi kuwasaidia waathirika.

  Kwa mujibu wa Mwakyembe, kuna taarifa kwamba, mgodi wa Tulawaka unafungwa kwa kuwa dhahabu imekwisha, hivyo amehoji kama Serikali imepewa fedha za kuhuisha mazingira, zipo wapi na kiasi gani.

  Dk Mwakyembe amesema, watanzania wamechoka kuachiwa mashimo yeye sumu ya zebaki.
  Mbunge wa Ukerewe, Balozi Getrude Mongella amesema, kama hatua zisipochukuliwa sumu zinazotoka kwenye mchakato wa kupata madini zitawamaliza watanzania.


  Balozi Mongella ametaka migodi inayotoa sumu ifungwe mara moja kwa kuwa zebaki inabaki mwilini na kukiharibu kizazi cha sasa na vijavyo.

  “Kwa kweli ni jambo baya, baya,…kama hatuchukui hatua mambo ya sumu it is blood money… hili la sumu it is immediate, tunafunga tujue moja” amesema Balozi Mongella.

  Dk Mwakyembe amesema, kama ubinafsishaji usipofanywa kwa makini utaligharimu taifa na ametoa mfano kuwa, madini yanawanufaisha wageni kuliko watanzania.

  Mbunge huyo amesema, ni bora madini yaachwe ardhini hadi Tanzania itakapokuwa tayari kuyachimba badala ya hali ilivyo sasa.

  “Mheshimiwa, kama uadilifu wetu una mgogoro yaachwe chini ya ardhi watachimba wengine” amesema Mbunge huyo na kusema kuna uroho katika kuzitumia rasilimali nchini.

  “Uroho umetutawala, tumeanza kutoana macho hata kabla utafiti haujafanyika” amesema na kubanisha kwamba, Baba wa Taifa, Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume hawakutaka kuchimba hata mafuta.

  Wakati huo huo, Dk Mwakyembe amesema, kama Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA) imeshindwa kazi iwaachie wengine.

  Amesema, kuna mafisadi katika sekta ya mafuta, Ewura inawafahamu kwa majina wakiwamo wanaochanganya mafuta ya taa na dizeli lakini mamlaka hiyo haichukui hatua.

  Dk Mwakyembe ametoa miezi mitatu Ewura ijirekebishe, isipofanya hivyo atawasilisha hoja binafsi bungeni. “Kama ni mshiko unaofanya wafumbie macho wahakikishe hili tatizo linakwisha Tanzania” amesema

   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I don't know why but I can't help but see Mongella as just a hypocrite. Sijui anasema hayo kwa sababu ana uchungu kweli au ni kutaka tu kujikosha na madhambi yake.
   
 3. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe anamaanisha, as long as tatizo la sumu linakwisha, ni sawa kwa wahusika kuendelea kuchukua mshiko ili wasiadhibu hizi kampuni! Na huyu ndio moja ya wabunge wanaosemwa ni mahiri, kasoma kuliko Wamisri na Wachina waliogundua karatasi, halafu kuongea hajui!
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  watu wanaweka maslahi yao binafsi mbele kuliko roho za wananchi.
   
 5. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Very strong, loud and clear. This is exactly what it means to be a mbunge. Hongera kakangu Mwakyembe, you have our moral support.
   
 6. M

  Makule Clement New Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe is right jamani!

  LAKINI........!!

  Hayo yote hayataisha bila sisi watanzania kufanya mapinduzi makubwa sana. Na ni wanahabari wenye uwezo wa kusaidia kuleta mapinduzi. Endapo nao pamoja na umasikini wasikubali kununuliwa.

  Tukiacha ubinafsi tutafika. Fikiria mjuukuu wako atakula nini na atakaa wapi, atafanya shughuli gani. Tukiweza kuwa na mawazo ya mbali kiasi hicho basi tutasonga mbele sana.
   
 7. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Kwanza tujiulize huo mgodi wakati unajengwa ulichukua tahadhari zote za kuzuia sumu isitiririke hovyo? Kama walichukua zilifikia kiwango kinachokubalika. Kama ndivyo imekuwaje maji yenye kemikali yametiririka?.

  Kwa maoni yangu tuache kujadili masuala haya kwa jazba tutafute ukweli wa mambo na kutafuta suluhisho la maana kwa manufaa yetu na kwa vizazi vijavyo. Tuache kusikiliza kelele za wanasiasa wa kibongo.

  Hawa wabunge wangekuwa kweli wanawakilisha maslahi ya wananchi wasinge fanya mambo mawili. Moja wasingejiongezea mishahara minono ambayo hailingani na mashahara wa mtanzania yeyote anyelipwa na serikali. Pili wasingetaka kuhodhi mfuko wa CDF.
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Usiwe na mawazo mafupi kiasi hicho, yeye hapo anawaonya kwamba kama ni rushwa ndo inawafanya wasione basi ni bora waache kuchukua rushwa na washighulikie tatizo, la sivyo atawasilisha hoja binafsi.

  Mbona hamsomi kitu kwa makini ila kukurupuka tu!! ah... mnakera kama kitu huelewi uliza siyo una-comment ujinga.
   
 9. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa hili naungana mkono na mh.MWAKYEMBE, KAMA mgodi unaharibu mazingira na kuwadhuru watanzania na mifugo yao,basi ufungwe ili kunusuru maisha ya watanzania.

  Zebaki ni sumu mbaya sana ,inakwenda kwa vizazi vyote vijavyo, tena hii element ni oxygen lover,inashambulia haemoglobin kwa kasi sana mwili kitu ambacho ni hatari,tutakuja pata taifa lenye idadi kubwa ya watoto walemavu,wenye mtindio wa ubungo, kwasababu ya fedha kidogo toka kwa wawekezaji ni hatari sana.
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bravo Mwakyembe!
   
 11. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu achana naye huyo ndivyo alivyo when it comes ni suala linalo mhusu Mwakyembe......!
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Mwakyeme fyatuka zaidii kileeee ulichosema utavunja kanuni...kile kile tunakisubiriaa wajuaa yale mambo yote ulioomba yatekelezwe hakuna hata moja....ni saanaa tu
   
 13. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  MWAKYEMBE ...! IN OUR HEARTS AND SOUL ...U R OUR PRESIDENT...! U SPEAK AND SOUNDS LIKE THE PIPOS PRESIDENT.....!

  PLZZZ BE OUR PHYSICAL PRESIDENT COME 2015..!
  our prayers r with u..!
   
 14. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nakupongeza Mzee mwaykembe kwa kazi yako unayoifanya Bungeni ,lakini nimeanza kuingiwa na hofu yasije kukutokea yaliyokutokea miezi michache iliyopita ,kwani shekh Yakhya amesha anza kunadi kunakiongozi atatekwa nyara ,huyu mzee ni mtabiri mkubwa wa chama sasa hata sielewe nini anakijuwa,Mungu atakulinda mzee wetu mwaykembe kwa shambulio lolote lile litakalo tokea na kama litatokea.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Dilunga,
  Nadhani hapa Mwakyembe alikuwa anazungumzia EWURA na tatizo analosema ni tatizo la kupandishwa bei ya mafuta kwa sababu ya collusion kati ya wauza mafuta na wakuu wa EWURA ambao supposedly wanakula mshiko.
   
 16. M

  Mundu JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Lakini hivi ni Mwakyembe tu anayepaswa kusema? Je ana sapoti ya nani? na wanao msapoti wako wapi na wanafanya nini?

  Maana alisema mengi mazuri na ataendelea kusema tu, haogopi kitu. Wa kuchukua hatua wa anayoyasema ni serikali au wananchi? nadhani Serikali haiwezi kuchukua hatua yoyote, tumeona kwa lile la richmond, tumebaki wanachi....
   
 17. M

  Mundu JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Lakini hivi ni Mwakyembe tu anayepaswa kusema? Je ana sapoti ya nani? na wanao msapoti wako wapi na wanafanya nini?

  Maana alisema mengi mazuri na ataendelea kusema tu, haogopi kitu. Wa kuchukua hatua wa anayoyasema ni serikali au wananchi? nadhani Serikali haiwezi kuchukua hatua yoyote, tumeona kwa lile la richmond, tumebaki wananchi....
   
 18. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni tafsiri yako wewe! Yeye mwenyewe kasema hivi:
  Kiswahili kinamsumbua huyu Mwakyembe maana sio mara ya kwanza kuchemsha chemsha. Huwezi kusema kama wanapokea mshiko wahakikishe tatizo linakwisha. Kauli hii haikemei rushwa kwa makali, inaacha tafsiri mbaya.

  Hayo matusi yako mengine, we gonna stay above the fray here, we'll bypass all that.
   
 19. Kabwela

  Kabwela Member

  #19
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Great Dr. Mwakyembe, and you show that you went to school, siasa unataka za facts.

  Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 inataka iwapo mtu au taasii ikituhumiwa kuchafua inatakiwa ijisafishe kupitia certified scientific means by its own costs. Pia precautionary principle ambayo ndio msingi wa sheria hiyo unataka kwa North Mara wangesimamisha uzalishaji mpaka ukweli halisi uwe proved scientifically (beyond reasonable doubt) ndio waendelee na uchimbaji ambayo ni tofauti na inavyofanywa kisiasa. Serikali inaweka sheria halafu inapindisha yenyewe kwa kuwa ni wawekezaji wa barrick. Hiyo pollution legacy site waliyoitengeneza wanamuachia nani? Pia polluter pay principle inataka mchafuzi asafishe kama ilivyo kwenye sheria ya mazingira, sielewi kwa nini serikali haiwawajibishi Barrick kusafisha maeneo waliyosafisha.

  Kazi kwelikweli kuwa mTZ unayefikiri kwa mantiki ukiangalia jinsi wanasiasa wetu wa mjengoni na serikali wanavyoongea na kufanya.

  Long live Tanzania
   
 20. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Okay, then, the gazeti was not clear, inabidi tudhani, tu guess.

  Lakini whether ni EWURA or what not, huwezi ku imply kwamba rushwa ni sawa as long as hatuoni matatizo. Wrong! Jasusi, viongozi lazima wazingatie kauli. Obama kataka kutolewa roho na kaneno kamoja tu, "stupidly."
   
Loading...