Mwakyembe ajitoa mhanga, Mongella afyatuka

Hivi kwa nini Mwakyembe anasema wananchi waishitaki BARRICK?

Yeye si mwana sheria na wana kampuni yao kabisa ya uwakili?

Kwa nini wasijitolee kwenda kuwakusanya watu na kuipandisha Barrick mahakamani?

Kuna ile film alicheza Julia Roberts, ya kufichua kampuni inayomwaga sumu. Hiyo kweli ilitokea na mama alikuwa ni karani tu kama sikosei. Sasa hawa Wanasheria wetu na tena ni Dr na msomi kama anavyojiita/itwa, kwa nini asilivalie hili njuga?

Ninavyofahamu uwezo wa Mwakyembe ni mkubwa sana kudeal na mambo ya UBUNGE. Nafikiri hili la kugaragazana na Barrick lingelifanya kichwa chake kichemke kidogo kama si sanaa maana ninavyojua hawa nao watakuwa na wanasheria wazuri sana.

Mwakyembe usiishie hapo. Labda hii kazi inakufaa zaidi hata ya UBUNGE yaani kutetea wananchi wote wa Tanzania na si Kyela peke yake..... Nenda huko na kawasaidie wana Mara kuishitaki hii kampuni na usiishie kusema Bungeni. Kelele zako haziishitui kabisa Barrick na Serikali....
 
Hivi kwa nini Mwakyembe anasema wananchi waishitaki BARRICK?
Yeye si mwana sheria na wana kampuni yao kabisa ya uwakili?
Kwa nini wasijitolee kwenda kuwakusanya watu na kuipandisha Barrick mahakamani?

Sikonge

Nchi yetu inaangushwa na wasomi hawana uthubutu hasa pale wanapohitajika!
 
Usiwe na mawazo mafupi kiasi hicho, yeye hapo anawaonya kwamba kama ni rushwa ndo inawafanya wasione basi ni bora waache kuchukua rushwa na washighulikie tatizo, la sivyo atawasilisha hoja binafsi.

Mbona hamsomi kitu kwa makini ila kukurupuka tu!! ah... mnakera kama kitu huelewi uliza siyo una-comment ujinga.

Mara zote huwa simwelewi Dilunga ni mtu wa namna gani. Jaribu kutafuta post zake hapa utakuta ni za kupinga tu hasa yale yaliyo mazuri kwa ajili ya nchi yetu. Ni hatari sana hii.
 
Sikonge

Nchi yetu inaangushwa na wasomi hawana uthubutu hasa pale wanapohitajika!

Kibaya zaidi ni SISI wananchi. Hapa ndani tu JF kumejaa watu ambao mweleo wao uko juu sana. Pamoja na hiyo, ungelitegemea WAMBANE Mwakyembe ili huyu bwana afanye kazi katika kiwango chake cha uelewa.

Zaidi ya ile tume aliyopewa na JMK na kwenda kuchota habari kwa akina MwanaKIJIJI, kubwa zaidi ambalo hadi leo Mwakyembe amelifanya ni lipi? Tena kwenye tume hukohuko akatumia vitu alivyosoma na kuja na mbinu ya kuanzisha kampuni ya kufua umeme (nayo ilikuwa ya kitapeli - Wamepewa eneo na wananchi kwa bei chee, nasikia sijui wameuza/watauza kwa wawezekzaje wa nje /nina uhakika kwa bei juu).

Mwakyembe, acha USANII. Mwanakijiji alisema sana hadi akafikisha POST 10,000. Kaona sasa muda wa kubadilisha mapigo na kaanza mashambulizi ya aina nyingine. Je Mwakyembe ni lini atakuja kwenye mashambulizi mengine zaidi ya hayo aliyopewa na JMK?

Huwa ni MPINZANI sana wa Dillunga kwa KUCHOKONOA kwake mambo. Huyu na yule Manyerere, Game Theory unaweza wachukia ila ukweli hawa ni watu wanao demand zaidi kwa kila kinachosemwa. Dillunga kahoji maneno ya kuendekeza UFISADI ya Mwakyembe, watu wanamuijia juu. Si wenyewe tunakaribisha hii hali? Mtu kazoza bungeni mnaona kamaliza kazi. Je tofauti yake na Kibaka Mongela ni ipi? Si wote wamesema bungeni kulaani sumu ya migodi? Then what?? Mwakyembe ngoma draw na Kipanga Mongella.

Hawa Wabunge wetu wanatakiwa wafanye kazi hadi watushangaze kwa kufanya yale ambayo hatukututegemea wafanye. Wafanye hadi nje ya mipaka yao. Wapo pale kwa ajili ya Watanzania. Hili la kusema tu bungeni na akitoka anawapigia simu anasema "Don't mind what i said, it's just politics ......." Na sisi huku tumeridhika na kufurahi kuwa Mbunge "Dillunga" ni shujaa. Shujaa my ..........
 
Mara zote huwa simwelewi Dilunga ni mtu wa namna gani. Jaribu kutafuta post zake hapa utakuta ni za kupinga tu hasa yale yaliyo mazuri kwa ajili ya nchi yetu. Ni hatari sana hii.


Huwezi kumwelewa kama uwezo wako wa kuchanganua mambo ni mdogo!
 
nashukuru sana MWENYEZI MUNGU AMEMFUNGUA KIFUA MWAKYEBE KUSEMA HAYA WATANZANIA TUAMKE TUDAI UHURU WETU BADO HATUJAPATA KAMA TUNGENKUWA TUMEPATA TUSINGEFANYIWA DHURUMA HIZI TUNAJIPANGA TUMECHOKA HIPO SIKU TUTAKUWA HURU NA SERIKALI HITAJUWA UMUHIMU WETU ILA SASA WANATUPUNGUNZA NA SUMU
 
JAmani mgaieni Mwakiembe donge lake anyamaze,wako wengi kama yeye ambao hukurupuka halafu hatuwasikii tena ,maana kutoa miezi mitatu sijui wana ahadi na Mwenyezi Mungu kuwa atayasubirisha marazi yasizidi kuenea ,lakini simshangai maana huyu si ndie yule alieihifadhi siri na kumzamisha Lowasa ? Huyu si ndie yule alievaana na Rostam huyu si ni ndie yule aliewaambia wazanzibari hawana adabu ,huyu na wenzake wamezusha mtindo wa kusema wanasubiri baada ya muda au bungeni hapataeleweka huyu ni mnafiki nambari moja tu ,hebu jamani mkatieni milioni zake asizidi kutubabaisha na kutizungua ,kama kweli ahame Chama ,kama kweli aachie ngazi kama kweli ana uchungu atafute Chama kingine ,basi japo kutishia kuwa atajiuzulu uanachama na kuachana na CCM anashindwa ? Ndio nikasema kuwa anadalili za unafiki tu ,hana jipya ,kila aliekuwemo ndani ya Chama kinachofuga mafisadi basi nae ni fisadi ,hata apige makelele kama kama paka aliezingirwa ,lakini mradi yumo CCM basi hana la kutwambia ,zaidi atakuwa anapiga makelele mchana jioni wanakutana kwenye vilabu.

Hebu kama kweli mna uchungu na Nchi hii ondokeni huko CCM ,mnabaki kufanya nini kwani Chama ni hicho tu ? Viko vyama ambavyo tunaona viongozi wake wanapambana na serikali wakiwa nje ya CCM na hoja zao zinafuatwa au kuchukuliwa na kufanyiwa kazi na hatuwaoni kukonda wala kufa ,ile nyie mliomo CCM mnaogopa kitu gani ? Tena kama haitoshi nyie mtakuwa sio wa kwanza kuachia ngazi ,sasa kubwa na la ajabu ni lipi ?

Kusema kweli makelele yenu hayana tofauti na Zombe ,hayana tofauti na Mahita watu ambao walikuwa wanasifika kwa ushujaa lakini nyuma ya pazia wanafaidika na vyeo vyao na hakuna aliewagusa .

Jambo moja ni kuwa ,ambalo nawashauri msingoje mkatemwa ,ng'atukeni CCM wakati mna mshiko au mna hoja za kuwakutanisha na wananchi na sio mnapopopolewa na CCM kwa kuangushwa kura ,hapo hata soko mtakosa tunawaona akina Mang'ula na wengine.
 

Hivi kwa nini Mwakyembe anasema wananchi waishitaki BARRICK?

Yeye si mwana sheria na wana kampuni yao kabisa ya uwakili?

Imagine that!

Sikonge, you tell me, Mwakyembe anawaambia watu wakaishitaki Barrick! Huyu huwa anawaambia waandishi yeye ni mwanasheria kasoma sana! Anasema kama huna shahada ya chuo kikuu huwezi kumuelewa. Halafu anatupia mzigo wengine ndio wakashitaki.

Ndio kansa ya Watanzania hii. Hatuna "initiative and guts," alisema jaji Lugakingira kabla hajafa, kwamba tumepoteza moyo huo wakati wa chama kimoja. Mtu anakwambia, JF imejaa thread za mapenzi tu, lakini yeye kaanzisha thread ngapi za falsafa na uchumi na sayansi, na kilimo, sifuri!

Mwakyembe msanii tu. Ni kipi kipya alichokisema hapo kuhusu Barrick cha kupigiwa makofi? Tunashangilia kiiiila kitu. Kikwete alikuwa California earlier this year, akatangaza kwamba mipango ya dual citizenship kwa sasa wamei shelf. Akasema "mnataka kula kule na huku?" Watu bwa ha haa haaa! Tunashangilia kila kitu.

Mama Mongella nae eti anaongea, last time I heard of her alikuwa na soo kubwa la hela za Bunge la Africa. Mustapha Mkullo akalipa deni, Bernard Membe akazima soo, Samuel Sitta atahakikisha haliibuliwi tena bungeni. Ndio playbook ya Chama Cha Mapindufisadi. Halafu mnataka tukae hapa tunashangilia Mongela Bravo that.... Mwakyembe Bravo this...Bravo their feet!
 
Last edited:
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Mwankyembe kuilaumu serikali bungeni kwa kufumbia macho uharibifu wa mazingira ni sahihi. Wote tunaojua lililo sahihi zaidi tuendeleze. Twawezatofautiana naye katika itikadi za kisiasa lakini tutakubaliana kwamba hatupaswi kuwaacha wawekezaji (BARIKI na wenzake) kuharibia mazingira huku wakijichotea maliasili yetu tena kwa kiburi.

Kwamba eti kampuni imesema polisi walifanya uchunguzi na kubaini madai ya uharibifu wa mazingira hayakuwa keli? Mkemia mkuu wa serikali siku hizi kakasimisha madaraka yake kwa polisi? Yote tisa lakini kumi ni kwamba swala la uharibifu wa mazingira lawezavaa sura ya kimataifa wakati wowote. Hapo serikali itajikuta yenyewe inajiweka pabaya kuhusiana na mikataba ya kimataifa tuloridhia.

Nchi yanakotokea makampuni haya ukitaka kuchimba madini lazima uonyeshe mkakati wa kudhibiti uharibifu wa mazingira. Mamlaka husika huweka bayana vigezo vitavyotumika kuhakiki kiasi gani mazingira yamekarabatiwa kufuatia uchimbaji. Je mikataba yetu nayo inazingatia haya? Ukaguzi hufanyika kwa wakati?
Safari ni ndefu lakini hatuna budi kuanza hata kama kwa kuchelewa.
 
Imeandikwa na Basil Msongo;


Tarehe: 27th July 2009



Dk Mwakyembe ametoa miezi mitatu Ewura ijirekebishe, isipofanya hivyo atawasilisha hoja binafsi bungeni. "Kama ni mshiko unaofanya wafumbie macho wahakikishe hili tatizo linakwisha Tanzania" amesema


- Mnyonge mnyongeni lakini lazima apewe haki yake, Mwakyembe amewataka wabunge wa maeneo hayo kuwachukulia hatua za kisheria wahusika, meaning kwamba anajua mipaka ya kisheria on this ishu kwamba mbunge wa Kyela huwezi kukurupukia majmbo ya wengine ambao mko sawa katika level ya ubunge, kama DK angekwua na nafasi ya juu kidogo angalau hata Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya madini basi mngekuwa na hoja mnaomshambulia,

- Unless kama mnaweza kutuonyesha nyinyi mmelifanyia nini hili taifa zaidi kama sio wote hapa tunapiga kelee hizo hizo kama za DK?
pole pole wakuu, tuwe wakweli na tutathmini halihalisi kabla ya kurusha makombora. DK hapo juu ameonyesha uelewa wa kazi yake na ametoa ultimum kwamba atawasilisha hoja bungeni meaning ndio uwezo wake kama mbunge kisheria ndipo unapoishia, unless kuna mengine dhidi ya DK, lakini kwa hili tu la hii mada ninaomba ku-differ na nyinyi wakulu.

- Kwa Mongella ni sawa kabisa ninashangaa sana kwamba bado yupo bungeni mpaka leo baada ya ile aibu ya ajabu kule Adis, only in Tanzania.

Respect.

FMEs!
 
- Mnyonge mnyongeni lakini lazima apewe haki yake, Mwakyembe amewataka wabunge wa maeneo hayo kuwachukulia hatua za kisheria wahusika, meaning kwamba anajua mipaka ya kisheria on this ishu kwamba mbunge wa Kyela huwezi kukurupukia majmbo ya wengine ambao mko sawa katika level ya ubunge, kama DK angekwua na nafasi ya juu kidogo angalau hata Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya madini basi mngekuwa na hoja mnaomshambulia,



FMEs!

Mkuu FMes,

Kama sikosei, hata Mwalimu Nyerere, mipaka yake ilikuwa inaishia Pugu Secondary. Lakini kwa sababu alikuwa shujaa, aliamua kuipanua na ikaendelea kukua hadi nje ya Tanzania.

Mwakyembe anaweza kwenda huko kama RAIA wa Tanzania. Kwani haruhusiwe kwenda Mara kama Mtanzania wa kawaida? Anaweza kuiagiza kampuni yake kwenda kuwasaidia hao wananchi.

Tofauti yetu sisi na yeye au wabunge wengine ni kuwa yeye ni Dr. wa sheria na hili hata yeye hujisifu kuwa ni MSOMI. Sasa kama elimu hiyo ya Panda hadi Darini anaishia kuzoza bungeni na sisi tumuite shujaa, nashindwa ona tofauti yake na wabunge wa kawaida wa "ndugu spika, hata mimi hilo nalipinga.." Mwakyembe kwa uana sheria wake huo, na kuwa kwenye hizo kamati za nishati na madini, angeliweza kwenda pale na kuongea na mbunge wa hilo eneo. Akikataa, basi anaingia kama RAIA wa kawaida na hakuna atakayesema TOKA HAPA MARA.

Ehh, Watanzania tuanze kujenga tabia ya kuwa-treat viongozi wetu kama MALAYA. "we pay, we demand". Tumechoka na hii ya miaka 40 ya sisi tunalipa na wao wanatuona ni MABUZI ya kuchunwa.

STOP UBUZI-NISATION.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Mwankyembe kuilaumu serikali bungeni kwa kufumbia macho uharibifu wa mazingira ni sahihi. Wote tunaojua lililo sahihi zaidi tuendeleze. Twawezatofautiana naye katika itikadi za kisiasa lakini tutakubaliana kwamba hatupaswi kuwaacha wawekezaji (BARIKI na wenzake) kuharibia mazingira huku wakijichotea maliasili yetu tena kwa kiburi.

Subiri Moto atakao kuja nao Mh Mwakyembe kwenye bunge lijalo hapo Nov, stay tuned!
 
SAFI SANA MWAKYEMBE

Tatizo watu tuliowapa dhamana ya kusaini mikataba yetu hawana uchungu na nchi yetu, hata tukifa kama kuku huko maporini wao na familia zao wameshakula commission, kweli inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom