Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 169
- 287
Urafiki kati ya China na Afrika una historia ndefu, ambapo mzizi wake ni maelewano kati ya watu wa pande hizo. Kuanzia amani na urafiki ulioletwa na meli ya Zheng He zaidi ya miaka 600 iliyopita, hadi juhudi za pamoja katika mapambano dhidi ya ukoloni na ubeberu, na maendeleo ya pamoja chini ya FOCAC na pendekzo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” katika karne mpya, kiwango cha uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika kimeinuliwa kwa mfululizo. Mawasiliano kati ya watu wa pande hizo mbili ndio kiini cha uhusiano huo.
Mwaka wa 2026 wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika una kauli mbiu ya “Kuimarisha urafiki wa siku zote na kufuatilia ndoto ya mambo ya kisasa”, na kuonesha sifa maalum ya kizama na mpangilio wa kimkakati.
Kupitia mawasiliano ya watu, shughuli hizo zitazidisha kuelewana na kuheshimiana kati ya China na Afrika. Ustaarabu wa China na wa Afrika una sifa ya kipekee. Mwaka huu, takriban shughuli 600 za mawasiliano zikiwemo mazungumzo, maonesho ya filamu na tamthilia, na mawasiliano ya watu mashuhuri mtandaoni zitafanyika, ili kukuza maelewano ya kina kati ya watu wa China na Afrika.
Kwa kuzingatia ustawi wa watu na ujenzi wa uwezo, shughuli hizo zitahimiza ushirikiano wenye faida halisi. Lengo kuu la ushirikiano wa China na Afrika ni kuwanufaisha watu. Shughuli za Mwaka wa 2026 wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika zitazingatia ushirikiano wa elimu, mafunzo ya ujuzi, kuongeza uwezo wa wanawake, teknolojia ya kidijitali, na akili bandia, ili kusaidia nchi za Afrika kuongeza uwezo wa kupata maendeleo endelevu.
Shughuli za Mwaka wa 2026 wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika zitakusanya maoni ya pamoja kuhusu utawala bora unaoweza kutimiza maendeleo. China na Afrika ni “wasafiri wenzi” katika mchakato wa maendeleo ya nchi na ustawi wa watu. Chini ya jukwaa la Mwaka wa 2026 wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika, pande hizo zitabadilishana maoni kuhusu namna ya kuhimiza utawala bora na maendeleo endelevu, na kuboresha maisha ya watu.
Mwaka wa 2026 wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Afrika ni kama daraja imara, linalovuka bahari na mabara, kupitia historia na mustakabali, na kuunganisha ndoto za watu. Kupitia shughuli hizo, moyo wa watu wa China na Afrika utakuwa karibu zaidi, na msingi wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili utaimarishwa zaid