Wadau, amani iwe kwenu.
Sipati picha hali ambayo hawa vijana wa CHADEMA waliyonayo hivi sasa.
1. Benard Rabiu Saanane aka Ben Rabiu wa Saanane
2. Nusrat Hanje
3. Asia Msangi
4. Peter Kibatala
5. Kumbusho Downson Kagine
6. Bob Chacha Wangwe
7. Christopher Cyrilo na wengineo wengi.
Hawa vijana walikuwa wanaanzisha mijadala kwenye mitandao ya kijamii wakimsifu, kumpamba na kumtukuza Mgombea wa Chama cha Democrat, Bi Hilary Clinton na kusema kuwa ndiye mgombea atakayeshinda Uchaguzi wa Marekani. Tena walienda mbali wakajimaliza kuwa Donald Trump hawezi kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani kwa sababu ni dikteta tena wakimfananisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.
Walichokuwa wanafanya vijana hawa ni sawa na walichofanya kwa Edward Lowasa kwenye uchaguzi wa Oktoba 2015. Walimpamba sana Lowasa kupitia mitandao ya kijamii wakasahau kuwa wapiga kura wengi hawapo humu na wala hawafuatilii mijadala inayoanzishwa.
Kwa sasa hawa vijana wapo kwenye hali mbaya sana hasa kutokana na matokeo yanayoendelea kutangazwa kuonesha kuwa Donald Trump anaongoza. Kwa hakika huu nao ni mwaka wa hasara kwao.
Najua walikuwa wanamkumbatia sana Bi Hilary Clinton kwa sababu ni Moderate hasa kutokana na utawala wa Rais Obama kulifanya taifa la Marekani kuwa maficho ya vijana wengi wa Tanzania wanaoendelea kuwatukana viongozi wetu. Unaweza kurejea mijadala inayoanzishwa na Mange Kimambi anayeishi California ambaye sina hakika yupo hali gani mpaka sasa. Pia wapo akina Kalley Pandukizi ambao wameingia Marekani kwa njia za panya na hivyo Trump akitekeleza alichonadi kwenye kampeni, naona ishara za vijana hao kuikimbia Marekani.
Niwakumbushe tu ndugu zangu wa CHADEMA, siasa zina misingi yake. Si kila mnachokipenda mtakipata. Vingine mtaishia kula kwa macho tu.