Mwaka unaisha, umefanikiwa kufanya nini?

Mwaka unaisha, umefanikiwa kufanya nini?

Mpauko

R.I.P
Joined
Jan 19, 2019
Posts
2,323
Reaction score
3,451
Wasalaam.

Zimesalia siku 20 tu mwaka 2019 uishe. Ni siku chache kweli kweli na zinakwenda kasi haswa.

Wengi watakuwa wanatafakari namna miezi 12 ilivyokwisha na huku wangali:

- Hawajatimiza malengo waliyojiwekea.

- Maisha yameharibika na kuvurugika.

- Familia zimesambaratika.

- Kupoteza ndugu jamaa na marafiki (misiba)

- Kuachwa/kusalitiwa ama kuachana.

- Kutimiza malengo ya kiuchumi na kifamilia.

- Kununua gari/kiwanja.

- Kujiwekea akiba.

- Kupata ulemavu.

- Kupoteza ajira nk.

Bila shaka kwa namna moja ama nyingine wengi tunaweza kuangukia katika masuala kama haya na mengine mengi.

Kwa kuanza na wale waliofanikisha malengo ya hapa na pale hongereni sana, haitoshi juhudu ziongezwe angalau mwaka ujao muwe pazuri zaidi.

Na wale kina wenzangu tuliofanikiwa kusajili kitambulisho cha NIDA, tupeane pole, maisha ndivyo yalivyo tusikate tamaa kwani kitambulisho nacho si mafanikio pia.

Mwenzangu umefanikisha nini mwaka 2019?

images.jpeg
 
Mwaka ulikua na changamoto sana lakini zilinifanya niamini kuwa zinaniandaa zaidi kuwa mshindi! Nilipitia mengi makubwa but MKONO WA BWANA ULIKUA JUU YANGU! Nawashukuru ndugu zangu, jamaa na marafiki waliokua upande wangu! Hata kesho ni siku. Marehemu Mama alikua akiniambia kila Mara "This too shall pass".
images%20(10).jpeg
best-health-and-fitness-quotes-every-test-in-our-life%20(1).jpeg
images%20(2).jpeg
 
Mwaka huu:

1. Nimeongeza ujuzi kwenye forex.

2. Nimejifunza website development (Hii nataka niitumie sana mwakani, infact mpaka sasa nimetengeneza websites mbili).

3. Nimesoma vitabu vinne vya kuongeza maarifa.

4. Nimeboresha ujuzi katika kazi yangu.

5. Nimejifunza kwamba "Bila pesa furaha hakuna".

6. Nimejifunza social media marketing hasa kwenye facebook na instagram.

MWaka huu sehemu kubwa nimetumia katika kuongeza ujuzi hasa maeneo yasiyo ya fani yangu!

The idea ni kuwa na wigo mpana kiuchumi! Kuanzia mwaka natarajia kuanza kuona matunda kwa uwekezaji wa elimu/ujuzi nilioufanywa mwaka huu.

Kwa sasa nakumbuka hayo.
 
Niliweka lengo la kupanga chumba...na limetimizwa

Niliweka lengo la kukuza biashara na limetimia kwa asilimia 80

Nilipanga kujaza vitu vyote vya muhim chumban na limetimia

Kiufupi namshukuru Mungu huu mwaka nmetimiza mengi

2020 naomba lile lengo kuu nlopanga litimie
 
Back
Top Bottom