Mwaka Mmoja Ndani ya Jamii Forums!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,246
2,000
N Leo nimemaliza mwaka mmoja tangu nijiunge na JF. Nawashukuru wanaJF wote kwa maandishi yao kwenye majukwaa mbalimbali yaliyonielimisha, kuniburudisha na kunipunguzia stress za maisha.Jukwaa la JF Doctor kwa mfano, limenifundisha mengi sana, mwalimu wangu mkubwa akiwa Dr. Mzizimkavu. Hongera sana MziziMkavu kwa kazi yako ya kuelimisha.

Jukwaa jingine ninalopendelea kutembeleai ni Jukwaa la Siasa. Jukwaa hili ni kama ulingo wa ndondi katika siasa za ushindani hapa Tanzania. Washabiki wa vyama viwili vikuu hapa nchini hutoana jasho kwenye jukwaa hili. Mapema kabisa kwenye mwezi wa pili na wa tatu mwaka huu, nikagundua kwamba Jukwaa hili huponza wengi kupigwa Ban. Nikajifunza namna ya kuvumilia cheche zinazowashwa dhidi ya chama ninachoshabikia cha chadema, cheche nyingi zikiwashwa na wadau wawili waitwao@Ritz na chama wa Gongo la Mboto. Nikijisikia kujibu chochote nafanya hivyo kwa uangalifu mkubwa kwa kutotumia jazba yenye lugha ya kuudhi/kukashifu. Namshukuru Mungu nimefaulu kwa hilo katika mjukwaa yote na mpaka leo Mods hawajanikunjia uso

.Kuna msemo: raha ya kitu huwezi kuifahamu mpaka pale hicho kitu kitakapokosekana. Hiyo kwangu ilidhihirika katikati ya mwezi wa tano mwaka huu pale uongozi wa JF ulipofanya marekebisho kwenye mtandao huu. Kwa muda wote ule wa wiki mbili za marekebisho nilipata shida sana na ndipo nilipogundua kwamba JF ni sehemu ya mwili wangu kama yalivyo macho au masikio yangu.JF is highly addictive! JF ni kila kitu bwana

!Nikimaliza Jukwaa la siasa naingia Habari na Hoja Mchanganyiko. Huko nako watu hutoa habari na mambo mengi ya kuelimisha. Kuna thread moja ilinieleza maisha ya watu katika visiwa vidogo zaidi hapa duniani. Niliipenda sana. Nikimaliza huko naenda mmu na cc.

Nikiingia mmu naangalia kama kuna thread ya wadau waitwao Mtambuzi Bishanga au Preta.Nikiikuta naisoma na kutafuta michango ya The Boss au Kongosho. Michango ya hawa, kwangu ni burudani tosha. Cc nako kulinipendeza kipindi Lizzy alipokuwepo. Baada ya Lizzy kupotea, cc imeendelea kung'aa kwa ujio wa mama moto @Lara1.

Stress zangu za maisha nazitibu kwenye jukwaa la jokes! Huko watu wanatoa utani na vimbwanga vya kuharibu mbavu zilizokaa vibaya. Mdau mmoja(simkumbuki jina) sitomsahau kwa thread yake iliyoniacha mdomo wazi kwa mshangao. Alikuwa anawaeleza watu walokuwa wanalalamika eti jina la Magufuli ni libaya! Mdau huyu akaenda nchi nyingine akatuletea majina ya mawaziri wa nchi hizo . Nukuu ya hiyo thread naiweka hapa chini:"

watanzania mnadai Magufuli ndie waziri mwenye jina baya angalia haya sasa;


Jacqueline Natombeka (Utamaduni Sauzi)
Kazakuku Firafisi (Mipango,Japan) ,
David Kinembe (miundo mbinu Kenya)
James Kakuma (Biashara Zambia)
Akaja Akatombeka (Nishati Ghana)
Nalia Namboo (Sheria Botswana)
Antonie Chipumbu (fedha Msumbiji)
Chirambo Kafirwa (Mazingira Malawi)
Rozia Kamkundu (Kilimo ZimbabwJapan)


Naomba nikiri hapa kwamba hayo majina ya mawaziri wa nchi mbalimbali sikupata nafasi ya ku -cross check kama ni ya kweli au ya kubuni.

Pia sikosekani jukwaa la Jamii Photos. Wajuzi wa kupakua picha hutoa picha zenye mafundisho na burudani. Wanaonifurahisha kwenye jukwaa hili ni: Mzizimkavu, Mbuzi Mzee, Boflo, SILENT WHISPER na Ndallo. Ndallo ni maalum kwa picha za kucheza(motion).

Nilichogundua baada ya kujiunga ni kwamba ukimsifia mtu kwenye jukwaa lolote utaandamwa sana.Hilo lilinitokea pale nilipovutiwa na aina ya uchangiaji wa mdau mmoja aitwaye THK DJAYZ.Huyu,akiona thread ni ngumu au haieleweki anachangia kwa kuandika: "Searching……… No Network…" Staili hii ilinivutia kwa sababu haina maudhi au kashfa kama vile kuandika: ‘kichwa chako kina ubongo au matope? Nilipomsifia THK kwa staili ya uchangiaji wake nilihukumiwa hivi: multiple id @work! Na maneno mengi ya kudhihaki kuvutwa kwangu na staili ya uchangiaji ya THK. Nikajifunza kuwa kusifia mtu hapa JF ni ngumu. Jaribu uone.

Kingine kinachoambatana na ugumu wa kusifia ni huu mtazamo wa baadhi ya wadau kupenda sana kuponda thread za wengine kiasi kwamba wanaomba kitufe cha ‘dislike' kiwepo! Salaleh! Kama thread imekuudhi na huipendi iache hivyohivyo au changia kiungwana kwa kusema kwamba hiyo thread hukuipenda na utoe sababu. Wengi hushindwa kuvaa uungwana na huishia kukashifu na Mods wanatoa ban.

Ule msemo wa busara wa: ‘Hakuna swali la kijinga ila kuna majibu ya kijinga' bahati mbaya sana una ukweli hapa JF.Tazama hili swali lililoulizwa hapa Jf kwenye mmu na majibu yaliyotolewa!

SWALI: Wajameni,naombeni mnijuze hasara na faida za kuangalia picha za ngono Huyu anataka kujua ukweli wa mambo yanayohusu picha za ngono.Anataka aelimishwe. Lakini ebu tazama majibu ya hilo swali
JIBU1. Uko darasa la ngapi vile??
JIBU2. Nenda fecebook hapa sio mahala pake jinga sana wewe naukome kutuchafua humu ni thegreat pekee kwendraa

I think Great thinkers should be great teachers! Let's educate these young men who can't tell branches from roots!

Najisikia kupungukiwa sana pale wadau niliowazoea kwa michango yao kutoonekana hapa jamvini kwa muda mrefu.Wadau hao ni: keren Happuch, e2themiza, @Senetor miss Judith na @Excellent. I really miss them.Nawapongeza Mods wote kwa kazi nzuri ya kusimamia jamvi letu na ninawaomba watuletee vitu vipya mwaka ujao wa 2013!

MAISHA BILA JAMII FORUMS HAIWEZEKANI! ASANTENI SANA NA HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA!
 

Arushaone

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
15,036
2,000
HYGEIA pamoja na kukupongeza kwa kufikisha mwaka mmoja, (mimi bado sijafikisha) hakika thread hii imeniongezea kitu! Kwa dhati kabisa nakupongeza kwa kuwa wewe ni kati ya wachangiaji ninaopenda kusoma posts zao kwani huwa mjanja sana kukwepa BAN.
 
Last edited by a moderator:

Erickb52

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
18,515
2,000
Hongera sana HYGEIA
JF inatuweka pamoja km ndugu! Tuendelee kuwa pamoja!
 
Last edited by a moderator:

Otorong'ong'o

JF-Expert Member
Aug 17, 2011
36,233
2,000
Hongera sana mkuu(Happy birthday)...Mi nna mwaka na miezi mitatu... Kwahiyo mm ni kaka yako naomba unipe shkamoo yangu fasta...


Mi nilikuwa mdau wa jukwaa la siasa lakini nilipata ban ya miezi miwili nilivyorudi niliamua kuamia CC...Ninamiezi kaa mitano huku Cc...Ila mjasiri haachi asili huwa nachunguliaga kule siasani ila ndo hivyo niko makini sana...

Sasa hivi narudi huko huko Siasani kwani kuna Masumbwi zinaendelea huko na kiingilio nilishalipa..
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,246
2,000
Hongera sana mkuu(Happy birthday)...Mi nna mwaka na miezi mitatu... Kwahiyo mm ni kaka yako naomba unipe shkamoo yangu fasta...Mi nilikuwa mdau wa jukwaa la siasa lakini nilipata ban ya miezi miwili nilivyorudi niliamua kuamia CC...Ninamiezi kaa mitano huku Cc...Ila mjasiri haachi asili huwa nachunguliaga kule siasani ila ndo hivyo niko makini sana...Sasa hivi narudi huko huko Siasani kwani kuna Masumbwi zinaendelea huko na kiingilio nilishalipa..
Shikamoo kwa sababu ya kukaa JF mwaka na miezi mitatu? Na akina Invisible na Maxence Melo nitawapa nini?
 
Last edited by a moderator:

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,246
2,000
Hongera sana mkuu(Happy birthday)...Mi nna mwaka na miezi mitatu... Kwahiyo mm ni kaka yako naomba unipe shkamoo yangu fasta...


Mi nilikuwa mdau wa jukwaa la siasa lakini nilipata ban ya miezi miwili nilivyorudi niliamua kuamia CC...Ninamiezi kaa mitano huku Cc...Ila mjasiri haachi asili huwa nachunguliaga kule siasani ila ndo hivyo niko makini sana...

Sasa hivi narudi huko huko Siasani kwani kuna Masumbwi zinaendelea huko na kiingilio nilishalipa..

Shikamoo kwa sababu ya kukaa JF mwaka na miezi mitatu? Na akina Invisible na Maxence Melo nitawapa nini?
 
Last edited by a moderator:

chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
0
Mkuu HYGEIA
Hongera sana kwa mwaka kutimiza mwaka mmoja JF; ban ni sehemu ya maisha ya JF si kitu cha kuogopa hata kidogo; mtu akitumia silaha na wewe unaziwasha mpaka kieleweke; hilo halivunji mahusiano yetu ya utanzania; mkuu ila haya majina ya mawaziri wako yameniacha hoi bado wapo madarakani?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:

stevoh

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
2,921
1,195
Yani ntajipanga nisome hii siredi ni ndefu mno. Alafu ujanitaja wakati wewe nimekupita naniliu... siku 10s
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,246
2,000
Mkuu HYGEIA
Hongera sana kwa mwaka kutimiza mwaka mmoja JF; ban ni sehemu ya maisha ya JF si kitu cha kuogopa hata kidogo; mtu akitumia silaha na wewe unaziwasha mpaka kieleweke; hilo halivunji mahusiano yetu ya utanzania; mkuu ila haya majina ya mawaziri wako yameniacha hoi bado wapo madarakani?

Chama
Gongo la mboto DSM
chama! Umetoka wapi huku? Unatakiwa kule Jukwaa la Siasa ukatoe misimamo!. Sasa ni hivi: Hayo majina ya mawaziri sikuyatoa mimi ila ni mdau mmoja hapa JF aliyatoa. Kama bado wapo au hawapo kwa kweli sijui hilo, na nashukuru kwa kunipa hongera.
 
Last edited by a moderator:

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,246
2,000
Ahaaaa HYGEIA mbona nililuwa na joke tuu...Naona kama umechukulia siriazi...

Najua sana ilikuwa ni joke, Nami nikaweka joke vile vile kwa,mba shikamoo sikupi ng'o ila utapata hongera kwa huo mwaka mmoja na miezi kadhaa. Kama umeshakula ban nirudishie hongera yangu!
 

chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
0
chama! Umetoka wapi huku? Unatakiwa kule Jukwaa la Siasa ukatoe misimamo!. Sasa ni hivi: Hayo majina ya mawaziri sikuyatoa mimi ila ni mdau mmoja hapa JF aliyatoa. Kama bado wapo au hawapo kwa kweli sijui hilo, na nashukuru kwa kunipa hongera.

Mkuu huwa napita kila kona jukwaa la siasa wanatoana roho kwa njaa; mimi na akili zangu siwezi hata siku moja kumshiriki wala kumsikiliza mganga njaa kama Ben Saanane na Exaud Mamuya

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,246
2,000
Aante @FP. Nami nitangulize honera kwako kwa kudumu humu miaka mitatu plus!
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,246
2,000
Mkuu huwa napita kila kona jukwaa la siasa wanatoana roho kwa njaa; mimi na akili zangu siwezi hata siku moja kumshiriki wala kumsikiliza mganga njaa kama Ben Saanane na Exaud Mamuya

Chama
Gongo la mboto DSM

Hapana chama. Kwa nini unataja majina ya wadau wa siasa hapa chit-chat? Hata wewe njaa unayo.Au huna tumbo?
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom