Mwaka mmoja bila Dkt. Magufuli: Falsafa ya utimilifu wa nyakati

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
MWAKA MMOJA BILA JPM;FALSAFA YA UTIMILIFU WA NYAKATI.

Leo 23:15pm 13/03/2022

Hayati Rais wa Tanzania John Magufuli alitoa ujumbe wa shukrani kwa viongozi wa dini na watanzania wote kwa kuitika wito wa kumuomba Mungu ili aliepushe taifa na janga la ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona, na kusema kuwa ana imani kuwa ugonjwa wa corona umeondolewa kwa nguvu za Mwenyezi Mungu.

''Palipo na Mungu hakuna kinachoshindikana, kwa niaba ya serikali niwashukuru watanzania wote ambao wengi walifunga, wengi walitubu, na wengi walisali na kuswali kwa ajili ya kumtanguliza Mungu mbele na mimi nina amini na nina uhakika watanzania wengi wanaamini kwamba ugonjwa wa corona katika nchi yetu umeondolewa kwa nguvu za Mwenyezi Mungu''.

''Leo humu wote tumekaa simuoni aliyevaa barakoa, hata wewe baba Paroko hujavaa chochote kufunika pua na mdomo wako hata injili isingetoka vizuri, umemtanguliza Mungu, hata wakati wa kutukomunisha hukuvaa chochote mkononi kwa sababu Mungu ni muweza wa yote''. Rais Magufuli alisema hayo alipokuwa akitoa salamu kwa waumini wa kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Chamwino jijini Dodoma,Jumapili hiyo,kauli ya Rais John Magufuli ilienda sambamba na kauli ya Nabii T.b Joshua aliposema Corona imeshaondolewa na Mwenyezi Mungu,iliyobaki ni moshi baada ya kuzima moto nao moshi utaisha,

Kwa hakika niliamini na niliomba kila mmoja aweze kuamini na iwe hivyo,Mungu ni mwema leo hii Corona tumeizoe,imeisha ama tunaishi nayo kama mafua,Leo hii watu wanaongelea mgogoro wa Urusi na Ukraine,hakuna mwenye kuongelea Corona tena,hata wale waliotuambia tufanye lockdown tusiende kanisani wala msikitini leo hii wanasema corona ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine,tutaishi nao,Jina la Mungu libarikiwe.

-Utimilifu wa Nyakati,Watu wema wataondoka (Mungu atalichukua Kanisa)ili Ufunuo uweze kutimia.

Unyakuo ni neno la teolojia ya baadhi ya madhehebu ya Ukristo yanayoamini kwamba Yesu atarudi toka mbinguni mara mbili, mojawapo ikiwa kwa ajili ya kuwatwaa wale wote waliomuamini kama Bwana na mwokozi wao.Ufunuo wa Yohana 3:4 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili,2 Wathesalonike 2:5

Je, hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? 6Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. 7Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. 8Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake,hapa tunafahamishwa kuwa wapo watu wema,kwa wema wao na uwepo wao hapa duniani wanafanya utimilifu usiweze kutimia,na sharti ufunuo utimie,hivyo basi watu hao wema Mungu atawachukua pamoja nao ili ufunuo uweze kuwa timilifu sawa sawa na ilivyotabiriwa na manabii.

-Mauti (Kifo) ni Usingizi.

Mauti au kifo sio maangamizi kamili bali ni hali ya kutokuwa na fahamu kwa muda wakati mtu anasubiri Ufufuo,Biblia kwa kurudia rudia huiita hali hiyo ni usingizi.Biblia ikielezea vifo vya Wafalme wa Israel,Agano la kale linasema kifo cha Daudi, Suleiman,na Wafalme wengine,Biblia inasema wamelala na Baba zao,( 1Wafal 2:10,11:43;14:20,31,14:8,2 Nyak 21:1,26:23, Ayubu alikiita kifo Usingizi (Ayub 14:10-12),kama Daudi (Zab 13:3) Yeremia (Yer 51:39,57) na Daniel (Dan 12:2)

Agano jipya limetumia neno Usingizi pia,tukitumia hali ya binti Yairo ambae alikuwa amekufa,Kristo alisema kuwa amelala (Mt 9:24;Mk 5:39) Alimwelezea Lazaro aliyekufa kwa namna hiyo hiyo kuwa amelala,(Yoh 11:11-14) Mathayo aliandika ,"ikainuka miili mingi ya Watakatifu waliolala" (Mt 27:52) wakitoka makaburini mwao baada ya kufufuka (Mt 27:53) akielezea kuuawa Stefano,Luka aliandika akisha kusema haya,"akalala".Matendo 7:60) Paulo na Petro pia walikiita kifo Usingizi (1 kor 15:51,52;1 Thes 4:13-17;2Pet 3:4).Bwana Yesu ametuthibitishia kuwa kifo sio nukta bali ni alama ya koma,baada ya yeye kufa na kufufuka na kupaa mbinguni kwa Baba.

Tunamshukuru Mungu kwa maisha ya Rais John Pombe Magufuli,tunashukuru kwa utumishi wa kutukuka uliouweka ndani ya Rais John Pombe Magufuli,Wewe ni Mungu,wewe ni Bwana, mapenzi yako yametimizwa,Rais John Pombe Magufuli amevipiga vita vilivyo vizuri,mwendo ameumaliza,imani ameilinda,na baada ya hayo ameweka taji ya haki ambayo Bwana,mhukumu mwenye haki,atampa siku ile ya Ufufuo,Watch and Pray Mat 26:41.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu unayemsema yupo kweli na si hadithi za watu kurahisisha mambo wasiyoyajua tu?
Ili uamini uwepo wa Mungu lazima ufikirie kama hayupo existence yako ilitoka na nini? Baada ya hapo utaelewa uzushi wa Annunaki and alike ulivyokuathiri kifikira.

JPM will remain best of the best president we have had in our state ever.
 
Ili uamini uwepo wa Mungu lazima ufikirie kama hayupo existence yako ilitoka na nini? Baada ya hapo utaelewa uzushi wa Annunaki and alike ulivyokuathiri kifikira.
Bado unaniuliza swali au ushajipa jibu unalotaka wewe swali lilikuwa la uzushi tu?

Unaweza kunipa nukuu hata moja niliyosema maisha yamefika hapa kwa kuanzishwa na Annunaki?

Nikikuita wewe mzushi, kwa sababu unanipandikizia maneno ambayo sijawahi kuandika, umeyaleta wewe na kunipandikizia mimi, nitakuwa nakosea?

Hivi hata mtu akisema hajui maisha yameanzia wapi, basi hilo maana yake ni kwamba automatically maisha yametoka kwa Mungu?

Unaelewa "logical non sequitur" ni nini?

Nimetaka uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Mpaka sasa hujatoa uthibitisho huo, umenijibia maswali uliyoniuliza wewe mwenyewe kabla sijayajibu!
 
Bado unaniuliza swali au ushajipa jibu unalotaka wewe swali lilikuwa la uzushi tu?

Unaweza kunipa nukuu hata moja niliyosema maisha yamefika hapa kwa kuanzishwa na Annunaki...
Labda nikusaidie kitu kingine... kuna aina ya majibu huwa ni maswali kwa muulizaji ili apate kujishughulisha kifikra kupata jibu sasa kuliko kumtafunia kila kitu.

Kwa sababu ni aina ya watu wanaoamini fikira zao kuliko uhalisia... pili nikujibu swali lako naelewa maana ya "Logical non sequitur" ndio naelewa. Tafsiri isiyo rasmi "Mantiki isiyo na usawa"
 
Labda nikusaidie kitu kingine... kuna aina ya majibu huwa ni maswali kwa muulizaji ili apate kujishughulisha kifikra kupata jibu sasa kuliko kumtafunia kila kitu. Kwa sababu ni aina ya watu wanaoamini fikira zao kuliko uhalisia... pili nikujibu swali lako naelewa maana ya "Logical non sequitur" ndio naelewa. Tafsiri isiyo rasmi "Mantiki isiyo na usawa"
Naomba nukuu niliposema naamini maisha yameanzishwa na Annunaki.

Ukishindwa kunipa nukuu hiyo, niombe radhi kwa kunizushia uongo.
 
Naomba nukuu niliposema naamini maisha yameanzishwa na Annunaki.

Ukishindwa kunipa nukuu hiyo, niombe radhi kwa kunizushia uongo.
Ukithibitisha nimeandika kama swali lako utaaminika... ukishindwa niombe radhi.

Pili ulitamani kupata uthibitisho wa uwepo wa Mungu labda niliweke hivi uwepo wako wewe ni uthibitisho tosha wa uwepo wa Mungu kwa sababu umeumbwa kwa kufanana nae,

wala usihangaike sana kuumiza kichwa chako jichunguze kila kitu unachotenda, ujuzi ulionao, uwezo wa kifikira, imani na ufahamu vyote ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu. Kani ya asili iliyondani yako inayokuongoza kutenda... ni ushahidi usiotia shaka na wenye usawa kimantiki.

Kwa kuwa mada ili muhusu hayati JPM nisingependa kuharibu mukitadha huo wa mleta mada na kumbukizi ya mheshimiwa.
 
Ukithibitisha nimeandika kama swali lako utaaminika... ukishindwa niombe radhi.
Pili ulitamani kupata uthibitisho wa uwepo wa Mungu labda niliweke hivi uwepo wako wewe ni uthibitisho tosha wa uwepo wa Mungu kwa sababu umeumbwa kwa kufanana nae .... wala usihangaike sana kuumiza kichwa chako jichunguze kila kitu unachotenda, ujuzi ulionao, uwezo wa kifikira, imani na ufahamu vyote ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu. Kani ya asili iliyondani yako inayokuongoza kutenda... ni ushahidi usiotia shaka na wenye usawa kimantiki.

Kwa kuwa mada ili muhusu hayati JPM nisingependa kuharibu mukitadha huo wa mleta mada na kumbukizi ya mheshimiwa.
Hujathibitisha nimeandika lolote kuhusu Annunaki.

Wewr mzushi tu.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Kusema uwepo wangu ni uthibitisho wa kuwepo Mungu ni logical non sequitur.

Hujathibitisha uwepo wangu ni uthibitisho wa kuwepo Mungu. Umezusha tu hilo.
 
Beneficiaries wa utawala dhalimu mnaumia sana.

Umeshatangulia chattle kufanya usafi kaburini MATAGA?
 
Ni wachache sana na inasemekana ni watu wenye akili na uoni wa jicho la tatu tu, walioweza kumwelewa JPM mmoja wao ni pamoja na mleta Mada,

Wengine wakija kuelewa tayari Tanzania ishazingirwa na vibaka kila kona kuliko miaka yote ya uhai wa nchi hii,

Ni wajinga pekee ambao mpaka sasa hawakumwelewa Shujaa, hii inaenda sambamba na wazungu wote walioamuru kufungia watu wao kwa sababu ya Corona! Lakini Leo, yamewashinda na JPM R.I.P kuwa Shujaa wao
 
RIP Magufuli, Chuma!
Ulifanya uliyoweza kwa moyo, akili na nguvu zako zote ili kututoa kwenye kuishi kwa mazoea na kutupeleka kwenye hamasa ya uwajibikaji kwa wote. Taasisi za umma zilibadilika kiutendaji kwa kiasi kikubwa.
 
Ni wachache sana na inasemekana ni watu wenye akili na uoni wa jicho la tatu tu, walioweza kumwelewa JPM mmoja wao ni pamoja na mleta Mada,

Wengine wakija kuelewa tayari Tanzania ishazingirwa na vibaka kila kona kuliko miaka yote ya uhai wa nchi hii,

Ni wajinga pekee ambao mpaka sasa hawakumwelewa Shujaa, hii inaenda sambamba na wazungu wote walioamuru kufungia watu wao kwa sababu ya Corona! Lakini Leo, yamewashinda na JPM R.I.P kuwa Shujaa wao
The state hawatakubali vibaka waizingire Tanzania!watafanya jambo!mageuzi yanaendelea !!
 
Ili uamini uwepo wa Mungu lazima ufikirie kama hayupo existence yako ilitoka na nini? Baada ya hapo utaelewa uzushi wa Annunaki and alike ulivyokuathiri kifikira.

JPM will remain best of the best president we have had in our state ever.

Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika.
 
Back
Top Bottom