Mwaka 47 ni mwaka upi? Na ni nini haswa kilitokea?

May 10, 2012
92
71

JUMAPILI 20.5.2012

Ilikuwa ni muda wa saa nne mchana, nikiwa nimeketi nje ya nyumba yangu nikipata Vitamin D asili kupitia Jua la asubuhi. Ghafla, akaja Rafiki yangu Tuntu niliesoma nae pale chuo kikuu cha dar-es-salaam, mara ya mwisho kuonana nae ilikua takriban miaka 3 iliyopita. Nilifurahi sana kumoana rafiki yangu Tuntu. Tulikumbushana zile adha mbalimbali tulizokuwa tunazipata pale UDSM kama Shato Pori, kubebana, RB na kadhalika, hakika ilikua ni burudani isiyo na kifani. Mara Baada ya mazungumzo ya hapa na pale nikamkaribisha ndani kwangu rafiki yangu Tuntu. Mgeni nae akaingia ndani bila hiyana. Huyu rafiki yangu Tuntu yeye ana katabia flani cha kuongea anachojisikia ( Kumuita Mropokaji itakua si sahihi) ila wazungu huwaita watu wa aina ya Tuntu as ' Ouspoken persons' sijui kwa kiswahili fasaha wanaitwa nani haswa...sasa huyu rafiki yangu Tuntu kwa sauti ya utani akaniambia na hapa na mnukuu.

" Mazingira ya chumba chako yanachosha sana, vitu viko vile vile tangu mwaka 47, jaribu kubadilisha muonekano wa chumba chako, paka rangi zenye kuleta hamasa sio za kuchusha, hamisha kitanda weka kwingine, badilisha bedlinens (mashuka, matandiko) weka zenye mvuto, yaani ilimradi kuleta utofauti"

Mimi, nkabaki nacheka tu ila mara baada ya Tuntu kuondoka, kuna swali moja bado lilikua kichani mwangu...Mwka 47 aliouzungumzia Tuntu ni mwaka gani haswaa? na kwa nini Tuntu alifananisha muonekano na rangi ya chumba changu na mwaka 47???

"As Africans our last hope is Scientific Socialism"

The Late Comrade Siad Barre
 
kulikuwa na tangazo la biashara la redio zamaani
RTD...
ambapo kuna mtu anausifia mchele baada ya kula chakula cha mkewe
anasema mchele huu...dah unanikumbusha mwaka 47......lol
nilipokuwa kijana lol

so watu wakaanza kila kitu cha zamani kukiita cha mwaka 47.....
 
mwaka 47 ni mwaka 47....ni miaka ileeeeee wengine hata wazazi wetu walikuwa hawajazaliwa.
 
1947 ni mwaka ambao Tanganyika ilikabidhiwa rasmi kwa watawala waingereza baada ya vita ya pili ya dunia.
Ukaanza utawala wa vibaraka kwa niamba ya watawala, mfumo ambao hadi leo huo unaendelea na tunaogopa kuubadili.
 
Hakuna kilichotokea, ila nakumbuka kuwahi kuwa na tangazo la biashara katika radio zetu(kama sikosei in banki ya posta) lililokuwa na maana ya kitu cha au mtu wa zamani... na wakasema mwaka huo 1947

Yeah, nalikumbuka hili tangazo.

Halafu Kijana Msomali ameuliza "outspoken person" kwa kiswahili anaitwaje, huyo anaitwa kiranga. Kiranga ni mtu mwenye kuwa mbelembele na msemaji sana hawezi kuficha kilicho mawazoni mwake.
 
Kiranga ni aina ya mtu
au tabia ya mtu?

waswahili husema 'ana kiranga yule'
na sio yule Kiranga....

au kiranga komo....

yaani kiranga kimemuisha........
 
....Mie hili neno "Kiranga" bado linanichanganya maana niliwahi kusikia mara nyingi watu wakisema "Mbona kiranga nilikiona!?" yaani ni kama wanajuta vile kwa lile walilosema/kulifanya....kwa maana hiyo wanajuta kwa kimbelembele chao.
 
mimi sitaki kuangalia ya 47. Nimeona mazingira mengine hapo. Miaka mitatu iliyopita. Graduate. Single room. Old furniture... Graduate, miaka 3 iliyopita, single room...
 
1947 ni mwaka ambao Tanganyika ilikabidhiwa rasmi kwa watawala waingereza baada ya vita ya pili ya dunia.
Ukaanza utawala wa vibaraka kwa niamba ya watawala, mfumo ambao hadi leo huo unaendelea na tunaogopa kuubadili.

mkuu huo ndo ukweli, kwani baada ya tanganyika kukabidhiwa kwa wakoloni wa kingereza walibadili mfumo baada ya 1947. Ulikuja mfumo mpya sasa kila kinachoonekana cha zamani wanakifananisha na enzi hizo.
 
Yeah, nalikumbuka hili tangazo.

Halafu Kijana Msomali ameuliza "outspoken person" kwa kiswahili anaitwaje, huyo anaitwa kiranga. Kiranga ni mtu mwenye kuwa mbelembele na msemaji sana hawezi kuficha kilicho mawazoni mwake.

Kiranga kwahiyo ww ni outspoken person kama rafiki yangu Tuntu.....nimeipenda hiyo
 
mimi sitaki kuangalia ya 47. Nimeona mazingira mengine hapo. Miaka mitatu iliyopita. Graduate. Single room. Old furniture... Graduate, miaka 3 iliyopita, single room...

Nilinunua hiki kiwanja kidogo last year so bado naendelea na ujenzi mkuu, so far nimejenga one room, wash room, kitchen na nimezungushia uzio....so mdogo mdogo mpaka nishushe kitu cha ukweli mungu akipenda...ww una nini Raia Fulani?
 
....Mie hili neno "Kiranga" bado linanichanganya maana niliwahi kusikia mara nyingi watu wakisema "Mbona kiranga nilikiona!?" yaani ni kama wanajuta vile kwa lile walilosema/kulifanya....kwa maana hiyo wanajuta kwa kimbelembele chao.

Kiranga ni mtu mwenye kupenda ngono kupita kiasi, kwa kiingereza wanamwita sexual mania.

Vilevile ni jina la mji uko Kenya na Uganda.
 
Kiranga ni aina ya mtu
au tabia ya mtu?

waswahili husema 'ana kiranga yule'
na sio yule Kiranga....

au kiranga komo....

yaani kiranga kimemuisha........

Waswahili wanasema "yule kiranga" kama wanavyosema "yule kidokozi" ki inawakilisha mtu mwenye tabia fulani, kama kibaka, kikojozi, kitindamimba, kingunge, kisirani.

Mara nyingine inaweza kutumiwa kama tabia, kwa mfano "yule mama ana kisirani kweli" na mara nyingine kama mtu, kwa mfano "yule kisirani kweli".

X-Paster naomba kujua umepata wapi hiyo habari ya uhusiano wa Kiranga na kupenda ngono.
 
Kiranga ni mtu mwenye kupenda ngono kupita kiasi, kwa kiingereza wanamwita sexual mania.

Vilevile ni jina la mji uko Kenya na Uganda.

Ghafla nimejikuta napenda jina la Kiranga. teh teh teh.

X-PASTER, Shukrani kwa u greti thinka na u greti noleji.

Kujikuta niko jukwaa la Siasa kidogo nizimie, nilipoona kontenti nilikua jukwa la Elimu.
 
Kiranga ni mtu mwenye kupenda ngono kupita kiasi, kwa kiingereza wanamwita sexual mania.

Vilevile ni jina la mji uko Kenya na Uganda.

Mie nilijua kiranga cha namna hii ni neno la Kibondei....Kwa hao jamaa kumwambia mtu ana kiranga mbele ya watu ni sawa na kutangaza vita ya msituni!!
 
Mimi, nkabaki nacheka tu ila mara baada ya Tuntu kuondoka, kuna swali moja bado lilikua kichani mwangu...Mwka 47 aliouzungumzia Tuntu ni mwaka gani haswaa? na kwa nini Tuntu alifananisha muonekano na rangi ya chumba changu na mwaka 47???

"As Africans our last hope is Scientific Socialism"

The Late Comrade Siad Barre

Mwaka 47 unatumika kuelezea maisha yetu sie tuliokula chumvi nyingi....BBC and almost died before computers!!

Babu DC!!
 
Back
Top Bottom