Mwaka 47 ni mwaka upi? Na ni nini haswa kilitokea?

prof J aliimba;
Bongo ya sasa siyo ya mwaka 47, hadi bibi kizee anafanya ukahaba.
vichochoro vya mwananyamala wanakaba roba za mbao....
 

JUMAPILI 20.5.2012

Ilikuwa ni muda wa saa nne mchana, nikiwa nimeketi nje ya nyumba yangu nikipata Vitamin D asili kupitia Jua la asubuhi. Ghafla, akaja Rafiki yangu Tuntu niliesoma nae pale chuo kikuu cha dar-es-salaam, mara ya mwisho kuonana nae ilikua takriban miaka 3 iliyopita. Nilifurahi sana kumoana rafiki yangu Tuntu. Tulikumbushana zile adha mbalimbali tulizokuwa tunazipata pale UDSM kama Shato Pori, kubebana, RB na kadhalika, hakika ilikua ni burudani isiyo na kifani. Mara Baada ya mazungumzo ya hapa na pale nikamkaribisha ndani kwangu rafiki yangu Tuntu. Mgeni nae akaingia ndani bila hiyana. Huyu rafiki yangu Tuntu yeye ana katabia flani cha kuongea anachojisikia ( Kumuita Mropokaji itakua si sahihi) ila wazungu huwaita watu wa aina ya Tuntu as ' Ouspoken persons' sijui kwa kiswahili fasaha wanaitwa nani haswa...sasa huyu rafiki yangu Tuntu kwa sauti ya utani akaniambia na hapa na mnukuu.

" Mazingira ya chumba chako yanachosha sana, vitu viko vile vile tangu mwaka 47, jaribu kubadilisha muonekano wa chumba chako, paka rangi zenye kuleta hamasa sio za kuchusha, hamisha kitanda weka kwingine, badilisha bedlinens (mashuka, matandiko) weka zenye mvuto, yaani ilimradi kuleta utofauti"


Mimi, nkabaki nacheka tu ila mara baada ya Tuntu kuondoka, kuna swali moja bado lilikua kichani mwangu...Mwka 47 aliouzungumzia Tuntu ni mwaka gani haswaa? na kwa nini Tuntu alifananisha muonekano na rangi ya chumba changu na mwaka 47???







"As Africans our last hope is Scientific Socialism"

The Late Comrade Siad Barre

1947
 
Back
Top Bottom