Mwaka 2024 watu watabambikiwa kesi nyingi kulinganisha na mwaka 2023 kutokana na presha za uchaguzi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
887
4,131
Zipo dalili kwamba wanasiasa wenye misuli watatumia sana mbinu chafu kupunguza kasi wapinzania wao. Zipo dalili zote kwamba watu wenye fedha hasa wafanyabiashara watasumbuliwa na kulazimika kutumia fedha zao nyingi kuwapa wanasiasa kwa mgongo wa kusaidia jamii.

Zipo dalili kwamba haki katika mazingira ya kisiasa haitakuwepo badala yake vitisho na mkandamizo wa fikra vitachukua nafasi kwenye jamii. Zipo dalili zote kwamba maridhiano yatakufa na badala yake mamluki kadhaa watazaliwa kutetea uovu

Zipo dalili kwamba mwaka 2024 utakuwa mwaka wakutapanya mali na fedha za umma kwa misingi ya kisiasa. Wasiokubalika na wanaokubalika wanakwenda kuongeza kasi ya kurejea majimboni na hivyo watahitaji mtaji wakuaandaa mazingira makanisani kupitia machangizo, kwenye pombe, kwenye huduma na shughuli za kijamii

2024 ni mwaka mgumu kwa wafanyabiashara na wanasiasa wenye mrengo wa kushoto. Anza kujipanga
 
Source?
 
Back
Top Bottom