Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,581
- 46,170
CHADEMA jipangeni kuingia uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 bila hata Katiba mpya. Ni wazi kwamba uwezekano wa kupatikana katiba mpya ni kuanzia mwaka 2026, hii ni kwa kuangalia mahesabu ya kisiasa ya chama tawala.
Hata hivyo mazingira ya kisiasa yamebadilika sana katika kipindi hiki cha miaka miwili. Jipangeni vizuri kuingia katika chaguzi zinazofuata, dalili zote zinaonyesha refa wa mchezo hatapendelea sana timu moja.
Kwa sasa pazeni sauti tu mabadiliko ya kisheria yafanyike katika tume ya uchaguzi.
Nyie ndio chama kinachotegemewa sana kutoa upinzani kwa chama tawala, mkikosekana mtawanyima raia wengi fursa ya kushiriki kuamua uongozi wa nchi yao hasa katika mhimili wa bunge.
Kuna nchi pia wapinzani waliwahi kushinda katika aina ya mazingira mliyopo nyie kwa sasa.