Mwaka 2018 mwanasayansi Elon Musk aliamua kupeleka angani gari yake binafsi

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Gari hiyo aliyokuwa akiitumia kwa muda sana huku duniani , ambapo alipanga kufanya hivyo kama majaribisho ya rocket yake kubwa ya falcon heavy ambayo ndio ilikuwa inaruka kwa mara ya kwanza kabisa

Gari ya aina ya Tesla Roadster ndio aina ya gari iliyopelekwa anga za mbali mpaka sasa inatimiza miaka 4 huku ikiendelea kuzunguka jua kutokea umbali wa zaidi ya kilomita millioni 150 kutokea katika jua

Ndani ya gari kulikuwa na sanamu " Starman " lenye mfano wa mwanaanga katika kiti cha mbele cha dereva ambalo limeshikishwa usukani kwa muda wote huo huku akiwa anasikiliza miziki ya kila aina ambayo imewekwa katika mfumo wa auto repeat

Kwanini Elon Musk akiamua kupeleka gari anga za mbali

Swali hili lilikuwa ni moja swali lililokuwa linawasumbua watu wengi ila alipoulizwa bwana Elon Musk alijibu kuwa alipeleka gari ili kuwatamanisha viumbe wengine walioko katika maeneo mengine ya ulimwengu wetu katika sayari zengine ili wafahamu kuwa kuna uwepo wa viumbe vinavyoitwa binadamu katika sayari hii

Jambo hili lilionekana ni jambo la hatari sana kwakuwa huenda likaja kusababisha hatari kwa dunia yetu kutoka kwa viumbe wengine kama wapo ambapo huenda wakaja kufanya huaribifu

Watu wengine walihisi kuwa kupelekwa kwa gari anga za mbali ni moja wapo ya ufanyaji wa promotion tu ya magari hayo ya tesla kwa maana tukio hilo liligusa hisia za watu wengi sana kwa maana lilikuw tukio la kwanza na kila mtu alifahamu kuhusu aina ya magari hayo ya Tesla

Gari linaweza vipi kuendelea kuwepo huko anga za mbali

Kitu chochote kitakacho pelekwa angani kwa kiasi cha mwendo kinachohitajika katika moja wapo ya orbit basi kitu hicho kitafanikiwa kuingia katika orbit na kuendelea kubaki katika orbit mpaka pale nguvu nyengine kutokea sehemu nyengine itakapo vuta kile chombo kuelekea kwake

Kwahiyo gari litaendelea kubaki huko anga za mbali kwakuwa tu kasi yake bado inaendelea kubaki vile vile sasa kama kasi itapungua basi huenda gari likavutwa na nguvu nyengine kuelekea kwake

geraldchristopher1@gmail.com
Gerald
FB_IMG_1666785555971.jpg
 
Video za hilo tukio mpaka leo uwa nazitazama napata same feeling nlipotazama tukio siku hiyo.
Yani zile engines zilivyorudu na kutua duniani zikiwa vertical aisee ila watu wapewe heshima kwakweli watu ni vichwa.
Wenzetu wanaumiza sana vichwa kufikiria vitu vingi nje ya Dunia yetu
 
Video za hilo tukio mpaka leo uwa nazitazama napata same feeling nlipotazama tukio siku hiyo.

Yani zile engines zilivyorudi na kutua duniani zikiwa vertical aisee ila watu wapewe heshima kwakweli watu ni vichwa.
Na hiyo video hapo juu ya bujibuji mtu anapuliziwa dawa...haikusisimui?
 
Video za hilo tukio mpaka leo uwa nazitazama napata same feeling nlipotazama tukio siku hiyo.

Yani zile engines zilivyorudi na kutua duniani zikiwa vertical aisee ila watu wapewe heshima kwakweli watu ni vichwa.
Hizo video nazipateje mkuu zipo youbtube siyo ,je ni niandike vip nipelekwe ili kupata hbr hzo
 
Weka ushahidi wapi imeandikwa kwenye hiyo quran kwamba Elon Musk atapeleka gari lake binafsi anga za mbali?
(55:33) O company of jinn and men, if you have the power to go beyond the bounds of the heavens and the earth, go beyond them!

Hapa kumbuka enzi hizo hata baiskeli haijagunduliwa ila Allah alijua ipo siku tutatoka nje ya dunya.
watu walikuwa hawaamini hiki kitu kitakuja kuwezekana, wangejuaje pasi Mungu kufunua kupitia Quran?
Allahu akbar
 
Back
Top Bottom