Mafanikio ya Elon Musk katika mfumo wa utuaji wa rocket duniani

Mafanikio ya Elon Musk katika mfumo wa utuaji wa rocket duniani

Mzawa_G

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
669
Reaction score
1,479
Ngoja nikwambie Kama utapata bahati ya kumfufua Neil Amstrong kwa sasa na umwambie Elon Musk ameshafanikiwa kutuisha takribani rocket 50 basi anaweza akafikiria kwamba bado yupo usingizini Kwasababu Amstrong na wanasayansi wengine walifikiria kuwa swala hili haliwezekani kamwe na ikabaki kuwa Science Fiction ( Yaani ni Mambo ya kisayansi ya kufikirika tu kipindi Chao )

Kipindi Cha Miaka ya 2015 kurudi huko nyuma watu wengi hawakuamini Kama Rockot boosters zinaweza kutua bila ya kupata na matatizo yoyote yale na pia unaweza Tena kutumika kwa matumizi mengine Ila Mara baada ya mwanasayansi Elon musk alivyokuja na mawazo haya ambayo yalikuja kubadilisha taswira mzima na mafikirio ya wengi sana ambapo mpaka Sasa Jambo Hilo kimekuwa la kawaida kabisa ambapo hapo mwanzo lilionekana ni Jambo zito sana

Mwanasayansi Elon na Musk na Jopo lake waliweza kuongezea calculations kadhaa kwenye zile calculations za Uundwaji wa Rocket ambapo hapa waliweza kuongezea mahesabu ambayo yatafanya rocket boosters ziweze kuwasha thrusters zitakazoweza kusukuma boosters hizo hadi kwenye eneo lake maalumu tena kwa mahesabu yatakayofanya Landing Legs kuweza kuhumili uzito wa booster yote

Japo hapo mwanzo lilikuwa Jambo gumu hata kwa mwanasayansi Musk Ila baada ya kuharibu Mara nyingi zaidi hatimaye zoezi Hilo liliweza kufanikiwa na kubadilisha maono ya watu wengi Juu ya Jambo hili , Hadi Sasa shirika la uchunguzi wa anga za mbali NASA limependa kutumia ideas hizi katika mission mbalimbali za mwezini na sayari ya Mars Mara baada ya ujio wa Mwanasayansi musk kwa asilimia kubwa ameweza kumfufua matumaini ya siku moja wanaanga wa NASA kuweza kutua katika sayari ya Mars

Picha moja wapo za hapo chini zinaonyesha Rocket boosters za Space shuttle zikiwa zinaelea baharini Mara baada ya kutua huko kwenye bahari ya Atlantic Ocean 2011 ( kumbuka huu ndio ulikuwa Utuaji wa Rocket nyingi back then huko . Risking ilikuwa ni kubwa sana kwa maana vyombo vingi na mifumo mingi ilikuwa inapata hitilafu Mara baada ya kutua )

Rais Putin aliomba kampuni ya space x iweze kufundisha namna ya mfumo huu unavyoweza kufanya kazi katika mojawapo ya vyuo vya nchini Russia vinavyotoa elimu hii ya Rocket science engineering kwakuwa alipenda siku moja mfumo huu uje kutumika katika mojawapo ya Rocket zinazotengenezwa na Roscosmos siku moja

Starship Super Heavy inakwenda kuwa Rocket kubwa zaidi na Nzito itakayoweza kutumia mfumo huu wa kutua salama kwenye eneo lolote la surface ya gimba ambapo kwa Mara ya kwanza tutaona ikifanya kazi katika mwezi wa 6 au 7 mwaka huu

Main Point

Hapa suala la kutua salama kwa Rocket ilikuwa ni Science Fiction hapo mwanzo Ila Elon Musk alikuja akabadilisha na kuwa Reality , Huenda Kuna Fictions nyingi zitakazokuja kuwa Reality Ila ni kiasi Cha Muda tu

[emoji419]AstronomyKiswahili

FB_IMG_1689443233293.jpg
FB_IMG_1689443230024.jpg
FB_IMG_1689443225302.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1689443233293.jpg
    FB_IMG_1689443233293.jpg
    50.3 KB · Views: 21
Wazungu wametuacha mbali sana.

Afrika tuna ishi miaka 100 nyuma ya Ulimwengu unavyo kwenda, Sisi tumebaki wasindikizaji, watazamaji, na washangaaji.

Bado tuko kwenye Elimu za kuchora panzi[emoji3074] na kupasua Panya [emoji232][emoji242]
 
Mkiwa Mafisadi ,walaghai Wezi wa Mali ya Umma Waonevu Watu wanajipenda Wenyewe (wabinafsi) Kamwe hamuwezi Kusonga Mbele Mafanikio Ya Wenzetu Weupe Ni Juhudi Zao na Kuheshimu sheria walizoweka Wao Ili Ziwatoe Kwenye Lindi la Umaskini na Kufika Mahali Pengine Zaidi ndo Matokeo Yake ndo Tunayaona Leo
 
Wazungu wametuacha mbali sana.

Afrika tuna ishi miaka 100 nyuma ya Ulimwengu unavyo kwenda, Sisi tumebaki wasindikizaji, watazamaji, na washangaaji.

Bado tuko kwenye Elimu za kuchora panzi[emoji3074] na kupasua Panya [emoji232][emoji242]
meli ya tiutanic kama ilitenngenezwa mwaka 1800 naa jiulize tulikuwaje kipindi hicho huku afrika
 
Back
Top Bottom