Mwaka 2014 utaukumbuka kwa lipi?

Mwaka 2014 utaukumbuka kwa lipi?

scatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
1,671
Reaction score
940
Zimebaki siku chache kukamilisha mwaka 2014 ambao kuna mengi yametokea ..mazuri na mabaya yote tumepitia
Maisha bado yanaendelea na muda si mrefu tutaanza mwaka mwingine wa 2015
Je ni jambo gani unalikumbuka na kamwe hautolisahau katika mwaka huu 2014..karibu tufahamishane wakuu
Kwangu mimi sitasahau nilivyo achana na mke wangu baada ya kumfumania na mwanajeshi..
 
Dah.! Kwaupande wangu sitausahau huu mwaka wa 2014 kwa kuondokewa na baba mdogo wangu baada ya kuangukiwa na chuma kizito kichwani na kufariki akiwa kazini ktk kiwanda cha A TO Z kilichopo arusha. R.I.P baba mdogo wangu.
 
Mimi nakumbuka esikirowo na na kichwa cha mwendawazimu kuongoza nchi
 
Boko haramu kuteka wasichana na kuwa wake zao.
 
Ebola,Isis,boko haram,Escro,Obama kutoa executive order on immagration, mengi mno nnayo kwasasa ni hayo tu
 
dah pole kwa kumfumania mkeo inauma sana.kwangu ni escrow scandal
 
mapunguvu makubwa nilio wahi kuyaona ktk utawara uliopo madarakani.na kusababisha ugumu wa maisha kwa umma wa watanzania.
 
Miss Temeke Sitti bint Zubeir kuzaliwa miaka tofauti lakini tarehe na mwezi kafanana
 
Waziri mwanamke kufukuzwa kazi Tanganyika, na zanzibar.


SWISSME
 
Dah.! Kwaupande wangu sitausahau huu mwaka wa 2014 kwa kuondokewa na baba mdogo wangu baada ya kuangukiwa na chuma kizito kichwani na kufariki akiwa kazini ktk kiwanda cha A TO Z kilichopo arusha. R.I.P baba mdogo wangu.

Pole sana mkuu mungu amlaze pema peponi.amen
 
Wakuu, huu mwaka umevunja rekodi kuwa mbaya kwa dunia nzima, ni mwaka ambao tumeshuhudia kikundi kikatili cha ISIS kikifanya mauaji na kuwa kikundi chenye uwezo mkubwa kiuchumi ie US 2B,ni mwaka ambao ndege yenye abiria imepotelea kusikojulikana mpaka leo, ni mwaka ambao watoto wa kike wa Nigeria wamepotea na hawajulikani walipo japo wanafahamika waliowachukua, ni mwaka ambao Boko Haram wameuwa watu wengi na kupata nguvu zaidi, ni mwaka ambao Alshabab wamewapiga wakenya kwa ukatili wa hali ya juu, ni mwaka ambao Israel ilirushuwa makombora elfu 3 ndani ya anga lake, ni mwaka ambao vita kati ya Israel na Palestina imepelekea vifo vya wapalestini zaidi ya elfu mbili, ni mwaka ambao USA imeshuhudia dalili za mgawanyiko kati ya black and white, ni mwaka ambao vita baridi kati ya Rusia na Western vimekua juu sana, ni mwaka ambao dunia imeshtushwa na sakata la Tegeta Escrow Tanzania, ni mwaka ambao tatizo la ajira limekua kubwa zaidi, ni mwaka ambao tumeshuhudia Ebola ikisababisha vifo na yatima ktk West Afrika. Wadau tuendeleze zaidi matukio yaliyovunja rekodi na kufanya kua mwaka wa kipekee.... Karibuni!
 
Prophet Tb Joshua alishatabiri toka mwanzoni kuwa 2014 is the year of crossing the bridge.
 
kweli aise ata ile meli ya china ilizama na kuuwa wanafunzi na raia wengi sana 2014
pia kuna wale wanafunzi waliouwawa kwa kupigwa risasi na magaidi sijui ni wapi kule lkn 2014
 
Kwngu mm sinto sahau nipale ambapontulizama na bot katika ziwa tanganyika tulikuwa tumetoka kuowa tukapona watu wa3 kati ya watu 80 sinto sahau
 
Back
Top Bottom