Ukiwa unaulizwa maswali uwe unajibu, kinyume na hapo huu mjadala unakuwa hauna maana.
Kuhusu uthibitisho wa kuwa kuna Muumbaji na hakuna nguvu ya uumbaji, nakuthibitishia kwa njia mbili, nazo ni :
1. Self-Evident Truth
Kitu chochote unachokiona ambacho kipo katika umbile fulani, ujue yupo aliye kisanifu, mwenye maarifa, mwenye uwezo, mwenye malengo na hekima juu ya kitu hicho.
Ulimwengu na vyote vilivyomo, haujatokana pasi na chochote au ulimwengu wenyewe umejitengeneza, hili haliwezekani, ni sawa na leo hii utuambie "Simu" hii aidha imejitengeneza au imetokana pasi na chochote, ila uwepo wa simu unatoa ishara hizo nilizo zitaja apo juu, na hili ndivyo lipo katika upande wa Ulimwengu.
2. Ufunuo yaani Qur'aan
Anasema Allah mtukufu :
38. Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu. (Qaf : 38 )
Angalizo, usipo jibu maswali niliyo kuuliza, nasitisha mjadala mpaka utakapo jibu maswali niliyo kuuliza.
Ahsante.