Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,902
- 145,986
Inawezekana wewe na wenzako huwa hamsomi ninachoandika au mnasoma halafu hamuelewi
Don't flatter yourself, hatuwezi kuelewa kitu ambacho hakieleweki to begin with, you put garbage in, you get garbage out, tutaelewaje?
Wewe mtu signature yako mwenyewe inakusuta, inasema "Sane people doubts" (sic), and I might add "insane people believe with no doubt".
Watu sane wakija ku doubt na kuuliza maswali relevant wewe unawakejeli?
Kama nyie mngekuwa mnasema hamjui kama Mungu yupo au hayupo hapo ningewaelewa
Nyani Ngabu as an agnostic is of this position, umeshindwa kumjibu maswali hayahaya.
Lakini huyo Nyani Ngabu,wewe, na wengine mmekuwa mkisema Mungu hayupo
You don't understand the meaning of "for arguments sake". Let's say mimi nakuja kama agnostic, sijui kama mungu yupo au hayupo, wewe unasema mungu yupo, nakwambia nipe ushahidi kama yupo ili na mimi niamini hivyo, utasemaje?
Hapa ndipo nilipowauliza mna ushahidi gani kuwa hayupo?
Kitu ambacho hakipo hakina ushahidi kwamba hakipo. Kwa sababu hakipo.
Nikikuambia unipe ushahidi kwamba juu ya mlima Kilimanjaro hakuna ukoo wa Wachagga wenye miguu mitatu na macho matatu utaweza kunipa ushahidi huo?
Hamjanijibu hadi leo!
Umejibiwa mara lukuki, umejibiwa Kiingereza, ukasema wewe Maimuna huelewi Kiingereza, ukaomba tafsiri, ukatafsiriwa Kiswahili, sasa unataka nini? ujibiwe kilugha cha kabila lenu?
Mtu anaposema jambo fulani au kitu fulani kipo
Anakuwa na mzigo wa kukithibitisha kwamba kipo
halafu wewe ukaja na kusema hakipo utaulizwa ni kwanini unadai hakipo
Kwa sababu hakijathibitishwa kuwepo.
Mtu akiniambia kuna Ukoo wa Wachagga wenye miguu mitatu na macho matatu wanakaa juu ya mlima Kilimanjaro, yeye ndiye mwenye mzigo wa kunionyesha ushahidi, mimi kama siamini, kazi yangu ya kukamilisha kubisha ni ndogo tu, ni kumwambia "nioneshe uthibitisho". Kama hajanionesha uthibitisho kwa nini niamini kwamba ukoo huu upo?
Kama vile watu nyakati za nyuma walivyokuwa wanadai kuwa dunia ni flat
Ambao walikuwa na sababu zao kusema hivyo.
halafu wakaja wengine kudai kuwa dunia sio flat,
Hawakusema kwamba dunia hai exist, walisema dunia si flat ni round. Big difference. Unachanganya madawa.
Sisi hatusemi kwamba mungu wako flat si wa kweli, mungu wetu mviringo ndiye wa kweli.
Tukisema hivyo utatudai uthibitisho wa mungu mviringo na itabidi tuuoneshe.
Sisi tunasema mungu hayupo. Tutatoaje uthibitisho kwamba kitu hakipo ilhali hakipo?
Wewe unaweza kutoa uthibitisho kwamba ukoo wa Wachagga wenye miguu mitatu na macho matatu haupo juu ya mlima Kilimanjaro?
Ndiyo kazi unayotupa hapa. Anayesema huu ukoo upo ndiye anatakiwa kuthibitisha hilo, anayesema haupo hahitaji kuthibitisha chochote, anahitaji ku challenge tu apewe uthibitisho.
ilibidi waseme ni kwanini sio flat sio kudai tu kuwa sio flat bila kuwa na sababu!
Once again you are proving to be the undisputed king of bad analogies.