Ahaa, sasa hapo kwenye red inaonyesha ndio kwanza umeanza kuzinduka kidogo. Lakini hapo kwenye blue bado unajichanganya! Mfano wako ulioutoa ni sahihi kabisa kwani nyie mnaoamini kuwa Mt. Kilimanjaro uko SINGIDA na sisi tunaosema uko RUKWA kumbe wote TUKO WRONG, and therefore based on this, no one can claim to be right maana kiukweli huo Mlima hauko Singida wala Rukwa! Sasa ubishi na madai ya ushahidi kutoka pande hizi mbili unaanzia pale nyie mnaoamini kuwa huwa Mlima uko Singida (mungu wenu) mlipoanza kutuzuga eti kwa ushahidi kuwa kwa vile Singida kuna baridi sana basi ndio maana mna kila sababu ya kuamini kuwa huo mlima uko Singida! Ushahidi wa namna hii hutolewa na -------- tu kwani hata Makambako ambako huwa kuna baridi kali kuliko Singida hakuna mlima mkubwa kama Kilimanjaro. Sasa nyie mliotumia mfano wa kijana mlemavu wa mkono kuweza kusukuma mkokoteni na kusema huo ndio ushahidi wa kuwa Mungu yupo (hence kauli yenu Mwacheni Mungu Aitwe Mungu) ni sawa kabisa na mjinga anayeamini kuwa palipo na baridi kali basi ni lazima kuna Mlima mkubwa sana mahali hapo! SNa ndio maana sisi tukawa tunapinga maana tuna ushahidi thabiti kuwa si kila palipo na baridi kali (in this analogy: kiumbe kilemavu) eti maana yake imesababishwa na uwepo wa Mlima Mkubwa sana (in this analogy: huyo Mungu wenu). Sasa kati ya pande hizi mbili, ni upi una hoja za kijinga kama sio uendawazimu kama unavyodai wewe? Eti
Kiranga, kweli huyu
Eiyer anaelewa anachokisema au anasema asichokielewa?