Kwanza tufahamu kwamba:-
1. Demokrasia si kuondoka madarakani baada ya miaka mitano, kumi au kumi na tano [Helmundt Korl wa Ujerumani alikaa madarakani miaka 18].
2. Sio sahihi kuamini kuwa nchi za magharibi ndiyo zenye demokrasia na usawa! [huenda sisi Waafrika hasa Watanzania tuna usawa wa hali ya juu kulika hao wa-magharibi! tofauti yetu na wao ni kwamba wenyewe wana vyombo vya habari vinavyoeneza propaganda dunia nzima]
Menny Terry:- Mabepari wamekwisha kukuingizia propaganda zao za uongo na kukuaminisha kuwa Gadaffi ni Dikteta. Ni jambo la kusikitisha sana unapokuwa mzalendo kisha ukatekwa na utumwa wa ki-magharibi.
Hao jamaa wakishamuondoa gadaffi itakuwa ni mchezo kwamba kila kiongozi atakayepingana nao watamtishia kwa reference ya Gadaffi. Nchi za Magharibi hawana nia njema na Africa hata kidogo. Wanarudisha utumwa na Ukoloni kwa mlango wa nyuma. Hebu fikiria hili: Baada ya vita vya peninsula mwaka 1953. Marekani na Japan ilipeleka misaada Korea kusini [misaada ya technolojia]. leo hii Korea ni miongoni mwa nchi tishio kiuchumi. Afrika tangu tupate uhuru tumepokea misaada na mikopo ambayo hadi leo watoto ambao hatujazaa wanadaiwa. Mikopo hiyo yooooote haikulenga kutuendeleza bali kutuingiza Kifungoni!! Ndiyo maana mkapa alipoingia madarakani alianza kupambana nao hadharani [Kumbuka hotuba yake aliyoitoa mwaka 1996 Tokyo Japan].
Ndugu Yangu Menny Terry:- Ni kudra za mwenyezi mungu kupata viongozi wenye silka za akina Mkwawa ndiyo watatuondoa kwenye hii minyororo ya Mabepari maana hawa mabepari wameshatudumaza kwa kupandikiza rushwa miongoni mwetu hadi kwamba mambo hayaendi.
Kwa Kumalizia Tafakari haya mawazo matatu ya Gadaffi ambayo aliyatoa kwa viongozi wa Afrika:-
1. Nchi za Kiafrika zikatae kulipa madeni zinayodaiwa na nchi za Magharibi kwa sababu westerns waliiba mali asili ya Afrika
2. Afrika tuwe na setillite yetu ya mawasiliano ili kuondokana na propaganda za vyombo vya habari vya Magharibi [Wachina walifanikiwa hili kwa kupiga marufuku vyombo vya habari vya magharibi. hivi sasa wanakula matunda ya mkakati wao]
3. Gadaffi alipendekeza Afrika iungane ili tuwe na sauti moja itakayotuwezesha kujilinda. [Libya wana mafuta gas na maliasili nyingine kiasi kwamba hawahitaji msaada wa nchi yeyote ya Kiafrika. Lakini wakapendekeza tuchangie hayo yote.
NINASHAWISHIKA KUKUBALIANA NA HOJA YA ROSEMARIE!!!