Waafrika tungekuwa na uadilifu ingewezekana kuunda USA, lkn kwa hali ilivyo mi naona Ghadafi alikuwa anaota, kwanza huo muungano ungewasaidia raia au watawala? Maana kama serikali zetu zimejaza wezi hiyo usa ingewatoa wapi watendaji waaminifu. Kiasili kama mnigeria hawezi kuwafanyia mema watu wa kwao hawezi kuja kuwafanyia mema say watu wa Malawi na vice vesa.
Mkuu.
Gaddafi anaota..wewe hata ndoto huna?
USA au nchi za Europe hazikufika katika hali ambazo unaziona leo kwa miujiza au kama mchawi anayefunika kijiwe kitambaa cheupe na kutoka njiwa.
Wamedhulumu sana, wameua na kuuana sana,wamefanya watu watumwa na wameunda systems za kuendelea kuitawala dunia kifedha,kiuchumi na hata kutawala mawazo na fikra za watu, na yeyote anaejaribu kuzipinga au kuzipiga vita systems zao basi ataitwa mad man, dictator.
Kwa hiyo, ndugu hizi serikali zetu,jamii zetu hazitakuwa safi, hazitapata watendaji waadilifu,hazitakosa wezi kama hatutakuwa tayari kujenga check and balaces ndani ya systems zetu,ndani ya taasisi zetu, ndani ya serikali zetu lakini tuelewe haya hayafanyiki over night!! Wakati nchi zetu zina miaka 50,40,30 tokea kupata uhuru, nchi za west na US zina zaidi ya miaka 100,200 ya uhuru wao na ujenzi wa systems zao ambazo pia wanazilazimisha kwetu.Lakini hata wao wanafanya "madudu".
Ifike wakati tuamini kuwa sisi pia kama tungeamua kila kitu wenyewe basi tungechukua muda mfupi kufikia lengo la uhuru wa kweli kwa kila mwafrika, hali ya dunia na uchumi unaoendeshwa na wababe wa dunia hautupi nafasi hiyo. Tukilielewa hili, basi tutaanza kuwekana sawa na kuzi-reforms taasisi zetu ili tupate watu waadilifu, viongozi wa aina ya Gaddafi kwa yale mazuri yake.
Tanzania, Afrika bila viongozi wizi na wasio waadilifu inawezekana,tekeleza sehemu ya jukumu lako.
Unapoona tatizo na kama unaelewa dawa yake usisiste kuuamsha umma wa Afrika.
Hakuna mwananchi wa kiafrika anaetaka kiongozi mwizi au asiye muadilifu, wengine wanahitaji kufunzwa vipi watawapata viongozi waadifu na wasio wezi.
Demokrasia ya West na USA hazikuota kama uyoga ,ni matokea ya ujenzi wa taasisi za umma zenye check and balance kwa miaka mingi.
Kuna tangazo la HEDEX, maumivu ya kichwa huanza pole pole.....na hivyo hivyo, tunaweza kuzijenga Taasisi zetu hapa Afrika pole pole,iko siku zitafikia hatua tutakayoridhika nayo.
Kutokuwa na taasisi hizo ni hasara zaidi. Tuzianzishe huku tunazipiga msasa.
Wasahili husema "ukiona vyaelea, vimeundwa!"
Tafakari, mkuu.