Mvutano Wizara ya fedh@ kuhusu kumpokea JK

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Mda huu inasemekana JK anatembelea wizara ya fedh@ kuna tetesi kwamba watumishi woote wanalazimishwa waende wakajipange mstari ili kumlaki, inasemekana hata kama kulikuwa na ishu nyeti inaendelea ofisini kwako lazima uende ukajipange msitari. "nilikuwa ninashida hapo hazina lakini wanadai eti shughuli zote zimesimama wafanyakazi wote lazime wakae nje kumlaki Rais" mwisho wa kumnukuu muathirika wa huduma Hazina. Nimepita maeneo hayo mda si mrefu kweli hakuna hata gari moja la mtu binafsi maeneo yamesafishwa vizuri na watu wapo smart kumsubili kumpokea Jk. Kumbe rais anapotembelea sehemu kuna ghalama zake?.
 
Mambo ya miaka ya 1984!..Ni kupoteza ufanisi tu wa kazi!...Zaidi sana wakubwa hapo wanazalisha bili ya matumizi, msalaba kwa walipa kodi!
 
Ezan hiyo font inatukwaza bana
 
Pole sana ndio maana tunatakiwa kuwaondoa maofisini hawa wazee wana mambo ya kliong mno na hawasomi alama za nyakati.

Utakuta maboss wote ni wale wa miaka ya 49
 
Sucker.... Inasikitisha kuona nchi ilivyo ya kijuha, kisa tu mtu analinda ugali. Ifike kipindi hizi nafasi za kuteuliwa zipunguzwe sasa. Alikuja Mizengo Pinda pale UDSM, hakuna hata mfagizi aliyelazimishwa kwenda Nkrumah.. na mapindi yaliendelea kama kawa, hata madenti wengine hawakujua kama Chakulialia alikuwa in da house. Tuwe watu huru sasa...... Aaaaaaaaagh!
 
shida zenu msitushirikishe hata kidogo na hiyo laana ya hazina
 
halafu watu wakiandamana wanasema ooooh watu wanakosa muda wa kufanya kazi wanaenda kwenye maandamano,sasa na haya wanayofanya ni nini ya kusimamisha kazi?
 
Mambo ya miaka ya 1984!..Ni kupoteza ufanisi tu wa kazi!...Zaidi sana wakubwa hapo wanazalisha bili ya matumizi, msalaba kwa walipa kodi!

....vipi, hawajamtungia nyimbo???!!!! Nasikia akitoka hapo anaelekea bandarini na TRA, mheshimiwa mwenzie makamu alikuwa huko juma lililopita tu!!!
 
hivi JK kwenda hazina/wizara ya fedha si kama kwenda kumtembelea jirani tu? maana hata malango yanatazamana, ni lazima kusababisha usumbufu wote huo? bila hazina rais/uongozi wa kazi gani? ina maana anaingia hazina kukagua mara moja kwa miaka mitano, ndiyo maana ujio wake unakuwa very special? do he real have any idea what is going on kwenye hazina yake yeye mwenyewe kwa hali hii?
 
Leo ameenda kukagua majengo na mazingira ya pale.
 
hivi JK kwenda hazina/wizara ya fedha si kama kwenda kumtembelea jirani tu? maana hata malango yanatazamana, ni lazima kusababisha usumbufu wote huo? bila hazina rais/uongozi wa kazi gani? ina maana anaingia hazina kukagua mara moja kwa miaka mitano, ndiyo maana ujio wake unakuwa very special? do he real have any idea what is going on kwenye hazina yake yeye mwenyewe kwa hali hii?
Jamani huo ndiyo ujirani!!! Ikulu na hazina mjumbe wao wa nyumba kumi ni mmoja, hivyo kujuliana hali ndio ujirani. siku nyingine atoke kupitia geti la nyuma la Ikulu asalimie mateja ya Feri pale labda vyombo vya usalama vitaona namna ya kuwatimua eneo hilo
 
Back
Top Bottom