Mvutano Mirathi ya Mengi wapamba moto. Abdiel & Benjamin wapinga kutupwa maombi yao na Mahakama ya Rufani

Kuna mdau alianzisha uzi humu akasema wale wadada wapo watano wote wapo kimkakati wamejilengesha na kuolewa na wenye pesa yaani,

JACQUELINE
FARAJA
NANSI

wengine wawili nimewasahau mmoja ishatimia bado hao wengine na ukichunguza ni kweli kwa kinachoendelea sasa hivi ila wachaga sio wakuoa wale.
Jackie Mengi sio mchaga Ni Muha mwenye asili ya kitusi anatokea kigoma sehemu inaitwa Manyovu
 
Wale wanarithisha watoto kabla hawajafa. Baba yao gsm kafa jana ila urithi katoa zamani

Mo dewji baba yake yupo hai ila urithi ameshatoa ndio maana mo anatamba

Sisi weusi urithi ni mpaka ufe na tena seke seke lianze
Ila kuna yule mhindi wa maji ya Afya na Sayona Tunda kama sikosei alizinguana na mwanawe mpaka kumfuta katika watoto wake kwa tangazo magazetini. Kwamba mtoto alikuwa anataka kumuua baba yake
 
Kesi ya kutengua huyo mama iko mahakamani,hukumu ya mauaji ikitoka inamtupa mariam nje ya kusimamia..lini ulisikia mali ya inasimamiwa na ndgu wa mke
Ila watakuwa wameshafuja sana mali kwa kipindi walichokuwa wakisimamia mali hizo kisheria.
 
Jackie Mengi sio mchaga Ni Muha mwenye asili ya kitusi anatokea kigoma sehemu inaitwa Manyovu
Wilaya ya Manyovu ni mpakani kabisa na Burundi, kijiji cha mwisho ni Mnanila - Manyovu ndio kwa makamu wa Rais, Mhe. Mpango, jimbo la uchaguzi linaitwa Buhigwe
 
Ila watakuwa wameshafuja sana mali kwa kipindi walichokuwa wakisimamia mali hizo kisheria.
Huyo wa kiume amenunua nyumba jirani yangu,pia kajenga za wapangaji yeye ndio anamjaza huyo mtoto chuki ili mtoto awe upande wake achume mali,fununu mirathi ikitenguliwa watafanya mahesabu kujua zilizopigwa
 
Waafriica Ni umaskini ndio inaleta matatizo yote haya.. ..

Hao wengine wengi wao Wana pesa kwa hiyo hawahangaiki Sana na Mali za marehemu.. ...

Na ukikuta familia za wahindi na waarabu maskini ujue vitta ipo ..nimeona mifano mingi...

Hii ya Mengi Ni kwamba toka na hapo watoto wakubwa walikuwa hawaivi na bi mdogo.. ...sasa Pana vingi ikiwemo kuko Moana pia!

Wangeweza kukaa pamoja na kuweka sawa.. lkn...
 
Ila kuna yule mhindi wa maji ya Afya na Sayona Tunda kama sikosei alizinguana na mwanawe mpaka kumfuta katika watoto wake kwa tangazo magazetini. Kwamba mtoto alikuwa anataka kumuua baba yake
... dah; hivi hii inawezekana? Unaachaje kuwa mzazi wake labda?
 
Ni sawa na wa wachaga wa zamani, warishirikisha watoto wakiwa wadogo Dr.Mengi na Mama Mercy walianza kutengeneza Kalamu na watoto wao nyumbani mikono imechafuka na wino sana leo mjinga mmoja aje awatoe aseme anataka kurithi vyote .Damu ingemwagika
Akili yake ni SAwa na mke wa Erasto msuya
 
Hilo jambo unalosema liliweza na linaweza kutekelezeka kupitia WOSIA, sasa shida ni kuwa Sheria inaruhusu kutikisa (challenge) uhalali wa huo wosia na kupitia hapo ndio meza zinapopinduliwa.

Ama watu wanaghushi wosia ( wanatengeneza wa kwao na kuusema ni wa marehemu) ama wosia halali uliotolewa na marehemu unapigwa na sababu za kisheria na kuonekana ni batili.
Hivi wewe leo ukipewa wosia uusaini wakati upo kati kati ya tendo la ndoa na unakaribia kumwaga bao zito sana, na unaambiwa saini vinginevyo unachomolewa kwenye K ili bao lako liishie katikati, utasaini au hausaini?!!! Lazima utasaini tu ili upate ile raha ya mida mfupi, ila je, wosia huo utakuwa halali kisa tu umesaini mwenyewe tene kwa hiari bila kushikiwa bunduki?!! Sasa alichofanya huyu mdangaji kwa mwengi kinatofauti gani na hii scenario niliyoieleza?! Ukizingatia mtu alikuwa amepatwa na kiharusi, ni mgonjwa na hafikirii vizuri?! Sasa huo wosia usitenguliwe kwa nini?! Tutumie akili zetu vizuri jamani, sio kubishana na kujaza server tu...

Inshort, atafute mali zake, aache kung’ang’ania walizochuma wengine
 
kwenye hili sakata bado namlaumu mzee mengi kwa kushindwa kuzisimamia vizuri hizi familia zake 2 za bi mkubwa na bi-mdogo, yaani mzee kaziachia matatizo hizi familia ambayo yalikuwa yana epukika kabisaa…...

Matajiri wengi hawaamini kama watakufa mkuu!! Ndo sababu wakifa wanakuwa Hakuna walichoandaa....!!! Ndo wanaacha misala kama ivi....” Mzee alikuwa tu anaita kikao wote wakiwepo watoto ndugu na mke wake anatoa maagizo Incase nikifa utaratibu ni huu na msimamizi ni Fulani imeisha
 
Ila kuna yule mhindi wa maji ya Afya na Sayona Tunda kama sikosei alizinguana na mwanawe mpaka kumfuta katika watoto wake kwa tangazo magazetini. Kwamba mtoto alikuwa anataka kumuua baba yake
Na alikufa na mtoto akaendelea kuwa ceo
 
Kuweka wosia wazi ni hatari mno...
Jaribu uwaishwe mbele za haki
Kuna Channel moja inatwa ID (Investigation Discovery), asilimia kubwa ya mauaji wanayotengenezea Documentary yanahusu kitu kinaitwa ‘Life insurance’ au ‘Bima ya maisha’, ambapo mtu anajikatia bima kwa endapo akifa basi mke / mume wake alipwe pesa kiasi kadhaa kulingana na ukubwa wa bima. Sasa unakuta yule mnufaika akigundua tu, anakutengenezew tukio ili ufariki alipwe bima, japo wengi hukamatwa ila wengine hafanikiwa. Ni hatari sana haya mambo ya mirathi
 
Yule Mzee alichoharibu kama kweli ni yeye mwenyewe ndiye kaandika ule wosia ni kuwabagua wale watoto wake wakubwa kwamba wasipate chochote kwenye urithi wake, yeye kama alitaka kuwanyima angeweza kusema tu warithi nguo au kitu kingine chochote kisichokuwa na thamani kubwa basi.

Lakini kuwanyima kabisa ndipo alipokosea.

Hii wewe ungekuwa baba inawezekana kufanya ivyo mkuu?? Aka kadada katapeli niamini!! Mimi ninachojifunza nikukomaa na mama Chanja mpaka dakika ya mwisho.... hii mambo yakuzaa ovyo ovyo ndo mashida Haya sasa
 
Kuna mdau alianzisha uzi humu akasema wale wadada wapo watano wote wapo kimkakati wamejilengesha na kuolewa na wenye pesa yaani,

JACQUELINE
FARAJA
NANSI

wengine wawili nimewasahau mmoja ishatimia bado hao wengine na ukichunguza ni kweli kwa kinachoendelea sasa hivi ila wachaga sio wakuoa wale.
Naomba nitag kwenye huo uzi niufanyie reference
 
Kuna mdau alianzisha uzi humu akasema wale wadada wapo watano wote wapo kimkakati wamejilengesha na kuolewa na wenye pesa yaani,

JACQUELINE
FARAJA
NANSI

wengine wawili nimewasahau mmoja ishatimia bado hao wengine na ukichunguza ni kweli kwa kinachoendelea sasa hivi ila wachaga sio wakuoa wale.
Hata katika hao wote uliowaoredhesha hakuna mchaga hata mmoja
 
Mzee alifuata uzuri kwa binti mrembo(Alikua na uwezo wa kuoa wazee wenzake), na Jacky alifuata PESA. Sielewi mnaomuandama, mnadhani mzee hakujua pesa ndio imemuwezesha kumpata mtoto mzuri? aliacha type zake akaenda kupambana na mzee miaka yote iyo na watoto ukampa halafu asipate kitu. Ah aisee Jacky pambana.
 
Back
Top Bottom