Mvuta bangi matatani !!!

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Mvuta Bangi aliamua kujaribu kufunga "Saum" Mwenzi wa Ramadhan.

Ilipofika saa 1.30pm,,, Mambo yakamchafukia akawa anahema kama bata..

Akachukua simu akapiga Radio-FM,, Ilikua ni kipindi cha kuchagua wimbo…

Mtangazaji akamwambia: Unaitwa nani? Unapenda kupeleka salamu kwa nani? Na Chagua WIMBO uupendao!!

Mvuta Bangi: Eee bwana eehh,, Mie sitaki yoote hayo… Kwa hisani zenu ,,,
NAOMBA MNIWEKEE ;
…..." ADHANA YA MAGHRIBI"….

Karibu mwezi mtukufu wa Ramadhani ,nawatakia kila lakheri Waislamu wenzangu wote popote pale mlipo ,Inshaallah tuukamilishe mwezi huu kwa kufanya ibada na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rahema na mwingi wa kusamehe.
 
Ndugu mwiba hiyo hadithi ya mvuta Bangi umeipata wapi? na swahaba gani aliyepokea?Au wewe ndie unayefuta hiyo Bangi? jaribu basi kutufafanulia usituchanganye na mambo ya dini na mvuta bangi? kwani katika Dini ya kiislam ni haramu kuvuta bangi hukumu ya kuvuta bangi ni sawa na ya Mtu mlevi basi usitie mambo ya Dini na Madawa ya kulevya umenielewa lakini?
 
Mboni unakuwa mkali bila sababu weye? yaani unang'ang'ana kama kakijukuu ka mtume!
 
hahahaha yaani nimecheka kwa hiyo ye futari yake ni hiyo Bangi? mh haya

Jamani waislamu wote ninapenda kuwatakia mfungo mwema na pia kuwajulisheni tuko pamoja ndugu zangu. Siku moja moja nami ntakuwa nasindikiza jamani msininyime ftari.

Ramadhani njema
 
Ahsante MwanajamiiOne ,unakaribishwa tu na huku tunachinja hatunyongi :D hulaga vya kunyonga tunapopanda tireni kama unavyojua hapo katikati tireni ikisimama wanapita kuku wa kukaranga amini usiamini unaweza kukuta kuku ana mguu kama wa mbuzi . :D
 
Ndugu mwiba hiyo hadithi ya mvuta Bangi umeipata wapi? na swahaba gani aliyepokea?Au wewe ndie unayefuta hiyo Bangi? jaribu basi kutufafanulia usituchanganye na mambo ya dini na mvuta bangi? kwani katika Dini ya kiislam ni haramu kuvuta bangi hukumu ya kuvuta bangi ni sawa na ya Mtu mlevi basi usitie mambo ya Dini na Madawa ya kulevya umenielewa lakini?

Unaweza kuipata popote ila katika Uislamu hakuna umuhimu wa kuikubali hadithi kwani tunaamini kabisa kila mmoja atabeba mzigo wake sijui huko upande wa pili kama mnayo aya katika bibilia inayotoa onyo hilo ,hivyo kuifuata au kutoifuata itatokana na kipimo ulichokiona wewe mfuataji ,huku katika Uislamu hakuna kulazimishana.
 
Wewe kweli ni mwiba,tamtafuta aliekubatiza hilo jina,uislam na bangi wapi na wapi?
Uislamu na bangi haupo mbali inategemea vipimo utakayoiweka tu ,maana huku katika uislamu tunaambiwa ikiwa hujui basi angalia faida na hasara alafu kazi kwako.
 
Mwiba Ulianzia umri huu nini!?

5579d1250205088-a-smk.jpg

smk.jpg
 
Ahsante MwanajamiiOne ,unakaribishwa tu na huku tunachinja hatunyongi :D hulaga vya kunyonga tunapopanda tireni kama unavyojua hapo katikati tireni ikisimama wanapita kuku wa kukaranga amini usiamini unaweza kukuta kuku ana mguu kama wa mbuzi . :D

....... hahahah hapa lazima pawe pale Salanda sikumbuki jina vizuri maana ni siku nyingiii. Na kweli pale kama hatujawahilishwa kunguru wa Zanzibar nina wasiwasi yaani ukinunua paja la kuku pale unakula hadi unasaza!!. Na mie huwaga sibakishi kuku ila pale niliinua mikono juu..... si bure

Aksante ndugu yangu mwiba ntakuwa nakutembelea mida ya jioni jioni............ kwa maana ndiyo muda pekee foleni inakuwa imepungua barabarani lol
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom