Mvua za mwaka huu sijui kama tutasalimika

Mvua za mwaka huu sijui kama tutasalimika

Tatizo hili mkuu ni kweli lipo na sio Mbeya na Dodoma tu ila,ni tatizo la Tanzania nzima na dunia kwa ujumla.Hata hivyo ukweli ni kwamba jambo hili kwa wasio wana wa Mungu wataliona kama jambo la ajabu na geni,lakini kwa wana wa Mungu,Mungu alishatuambia kwamba mambo haya yatatokea.Kama Baba wa duniani hamfichi mwanae jambo,Mungu wetu wa mbinguni ni zaidi,hajatuficha kitu.Jambo hili ameliweka wazi katika kitabu cha Mwanzo 18:17.Na katika kitabu cha Zaburi 25:14 amesema hivi,"Siri ya Bwana iko kwao wamchao,Naye atawajulisha agano lake."Kwa hiyo jambo hili liko wazi kwa wale wamchao,yaani wana wa Mungu.

Katika kitabu cha Mathayo 24:3;7 tunasoma maneno haya,3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa mizeituni,wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha,wakisema,Tuambie,mambo hayo yatakuwa lini?Nayo ni nini dalili ya kuja kwako,na ya mwisho wa dunia?Katika majibu yake,Bwana Yesu anataja dalili nyingi,lakini katika mstari wa saba anasema hivi, "7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa,na ufalme kupigana na ufalme,kutakuwa na NJAA, na matetemeko ya nchi mahali mahali." Mkuu njaa haiwezi kuwepo bila kukosekana mvua,kwa hiyo ni wazi kwamba aliyosema Bwana Yesu yanatimia sasa.Na hali bado mkuu itazidi kuwa tete.Katika mstari wa nane sura hiyo hiyo ya 24, Bwana Yesu anasema,"Hayo yote ndio mwanzo wa utungu."

Ni mjinga tu atakayepinga kwamba dunia haijafikia ukingoni,dalili zote zimeshatimia.Litakuwa tendo la busara na hekima kwa hiyo kwa kila mwanadamu aanze kujiandaa kwa ujio wa Bwana Yesu,na ambaye hajamwamini Bwana Yesu afanye hivyo sasa.Ni jioni mno,Bwana Yesu yuko karibu kabisa kuonekana mawinguni na utukufu wake na mwaliko mkuu wa malaika tayari kulichukua kanisa lake.
Mimi naishi mbeya Kusema ukweli sijawahi kupenda kulima sababu ya kunyanyaswa wakulima. Ila nimejaribu kutokana na hali ngumu. Ila mwaka huu umekuwa wa ajabu. Mwaka Jana muda kama huu mvua ilikuwa inamwagika mpaka barafu zinadondoka ila mwaka huu nimeshuhudia mvua mbili tu mpaka sasa. Dodoma mvua zimekat waliopanda mbegu zimeungua kabla hazijatokeza juu ya USO wa Ardhi. Wadau kwa halo ilivyo kutakuwa na njaaa kupita maelezo kama mvua haitanyesha. Ukweli Juma Pondamali Mensah kaja vibaya
 
Jamaa wa TMA hawapo humu watoe hata muelekeo wa miezi sita ijayo?
 
nilishangaa sana jamaa mmoja anasimama mbele za watu ana anasema mkoa utakaokutwa na NJAA ...RC,DC,DED,DAICO and the rest agricultural officers hawana kazi... bila kujua kuna agricultural production factors .
sasa MUNGU nae akajibu maombi yake...

Halafu huyo jamaa anasema watu wachape kazi huku yeye anapunguza walioajiriwa. Halafu mwenyewe hajawahi hata kujiajiri siku zote yuko kwenye ajira. Ukimuuliza kazi ziko wapi anasema kazi zipo watu hawajitumi tu. In short jamaa anamwaga nadharia za hatari lakini uhalisia haijui hata chembe.
 
Jamaa wa TMA hawapo humu watoe hata muelekeo wa miezi sita ijayo?

Hao TMA ni janga huwa wanasubiri mvua ianze kunyesha kisha waseme mvua itakuwa nyingi. kuna siku za nyuma walikuwa wanatabiri ikawa inaenda tofauti, watu wakaanza kuwachana, nakumvuka kuna wakati MCH.Kakobe aliwakebehi huo utabiri wao, naona mama Kijazi alienda ITV kumwaga.povu eti watu wasibeze utabiri ni makosa
 
Mimi naishi mbeya Kusema ukweli sijawahi kupenda kulima sababu ya kunyanyaswa wakulima. Ila nimejaribu kutokana na hali ngumu. Ila mwaka huu umekuwa wa ajabu. Mwaka Jana muda kama huu mvua ilikuwa inamwagika mpaka barafu zinadondoka ila mwaka huu nimeshuhudia mvua mbili tu mpaka sasa. Dodoma mvua zimekat waliopanda mbegu zimeungua kabla hazijatokeza juu ya USO wa Ardhi. Wadau kwa halo ilivyo kutakuwa na njaaa kupita maelezo kama mvua haitanyesha. Ukweli Juma Pondamali Mensah kaja vibaya
Weather forecast
Bussiness forecast
"Shut up forecast"
 
absolutely right mkuu..
Mbona kama unakimbizwa hebu tulia uandike kwa umakini kijana
[emoji3][emoji3]nae ni mhanga nn

Halafu huyo jamaa anasema watu wachape kazi huku yeye anapunguza walioajiriwa. Halafu mwenyewe hajawahi hata kujiajiri siku zote yuko kwenye ajira. Ukimuuliza kazi ziko wapi anasema kazi zipo watu hawajitumi tu. In short jamaa anamwaga nadharia za hatari lakini uhalisia haijui hata chembe.
 
Kilimo cha kutegemea mvua kilishapitwa na Makati dunia ya Leo.
 
Nitaendelea kuwakumbusha habari za wapelelezi 12 wa Taifa la Israel waliotumwa na Musa kukagua hali ya nchi wanayoiendea.10 waliona vitisho na hali ngumu tu,waliona mijitu, wawili tu Joshua na Kaleb walioona nchi ya maziwa na asali.Waliwaona viumbe wakawaida wakiishi nchi hiyo huku wenzao wakiona majitu.

Naiona Tanzania itakayofanikiwa na kuwashangaza watanzania wenyewe hata wale waliotucheka au kutudhania sisi tu watu wa kuomba omba daima.

Nayaona waliyoyaona Joshua na Kaleb.Kama wengine mnaona ukame ombeni kwa MUNGU neema ya mvua,serikali haileti mvua japo mliwahi kuaminishwa kuwa ipo mvua ya kununua.
MUNGU hujibu maombi hajibu malalamiko.

Ndugu yangu uliyelima Mbeya niambie umelima eneo lipi la Mbeya maana Mbeya ni kubwa.Nitajie kijiji ulicholima jina lake na Wilaya yake,nitajie na zao ulilolima naweza kukupa ushauri.

Nimetembelea baadhi ya maeneo ya Mbeya (v). Wakulima wanalalamika lakini kila zao walilopanda limeota na linaendelea vizuri,ila kiasi cha mvua kinachonyesha hakiwaridhishi maana hawajakizowea,japo mazao yanaendelea vizuri.

Nasisitiza nitajie kijiji,Wilaya na zao tushauriane hatua za kuchukua.

Acha stori zako za kitapeli
 
Mimi naishi mbeya Kusema ukweli sijawahi kupenda kulima sababu ya kunyanyaswa wakulima. Ila nimejaribu kutokana na hali ngumu. Ila mwaka huu umekuwa wa ajabu. Mwaka Jana muda kama huu mvua ilikuwa inamwagika mpaka barafu zinadondoka ila mwaka huu nimeshuhudia mvua mbili tu mpaka sasa. Dodoma mvua zimekat waliopanda mbegu zimeungua kabla hazijatokeza juu ya USO wa Ardhi. Wadau kwa halo ilivyo kutakuwa na njaaa kupita maelezo kama mvua haitanyesha. Ukweli Juma Pondamali Mensah kaja vibaya
JPM JUMA PONDAMALI MENSAH
 
Acha stori zako za kitapeli

Kwa kuwa kwako wewe ukweli ni utapeli na uongo ni ukweli endelea kusubiri na kulalamika.Utavuna malalamiko na manung'uniko,maana imeandikwa apandacho mtu ndicho atakachovuna.Unapanda kushindwa utavuna kushindwa,tunaopanda kushinda tutavuna kushinda.Nakushauri kuungana na washindi ila najua kupokea au kukataa ushauri ni hiari.

Chagua unachopenda tukutane msimu wa mavuno.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom