Nitaendelea kuwakumbusha habari za wapelelezi 12 wa Taifa la Israel waliotumwa na Musa kukagua hali ya nchi wanayoiendea.10 waliona vitisho na hali ngumu tu,waliona mijitu, wawili tu Joshua na Kaleb walioona nchi ya maziwa na asali.Waliwaona viumbe wakawaida wakiishi nchi hiyo huku wenzao wakiona majitu.
Naiona Tanzania itakayofanikiwa na kuwashangaza watanzania wenyewe hata wale waliotucheka au kutudhania sisi tu watu wa kuomba omba daima.
Nayaona waliyoyaona Joshua na Kaleb.Kama wengine mnaona ukame ombeni kwa MUNGU neema ya mvua,serikali haileti mvua japo mliwahi kuaminishwa kuwa ipo mvua ya kununua.
MUNGU hujibu maombi hajibu malalamiko.
Ndugu yangu uliyelima Mbeya niambie umelima eneo lipi la Mbeya maana Mbeya ni kubwa.Nitajie kijiji ulicholima jina lake na Wilaya yake,nitajie na zao ulilolima naweza kukupa ushauri.
Nimetembelea baadhi ya maeneo ya Mbeya (v). Wakulima wanalalamika lakini kila zao walilopanda limeota na linaendelea vizuri,ila kiasi cha mvua kinachonyesha hakiwaridhishi maana hawajakizowea,japo mazao yanaendelea vizuri.
Nasisitiza nitajie kijiji,Wilaya na zao tushauriane hatua za kuchukua.