Mvua yaanza kunyesha Morogoro

chrissleon

Senior Member
Jul 22, 2015
147
89
Habari za asubuhi wakuu! hatimaye Morogoro mjini tuna anza kuona matokeo ya dua na maombi ya viongozi wa dini, mvua imeanza kunyesha kuanzia saa 5:30 mpaka sasa hivi bado inaendelea sijajua ndugu zetu wa Mahenge na sehemu nyingine kama wamebahatika kupata hizi baraka, mda si mrefu Morogoro hatuta kuwa na kelele za njaa.
 
Habari za hasubuhi wakuu! hatimaye Morogoro mjini tuna anza kuona matokeo ya dua na maombi ya viongozi wa dini, mvua imeanza kunyesha kuanzia saa 5:30 mpaka sasa hivi bado inaendelea sijajua ndugu zetu wa Mahenge na sehemu nyingine kama wamebahatika kupata hizi baraka, mda si mrefu Morogoro hatuta kuwa na kelele za njaa.
Sio Hasubuhi ni Asubuhi

Mjin hapa kwenyewe imenyesha kwa mafungu. Itakuwa Mahenge?
 
Sio Hasubuhi ni Asubuhi

Mjin hapa kwenyewe imenyesha kwa mafungu. Itakuwa Mahenge?
Mkuu bora sisi huku imenyesha kuna sehemu toka mwaka uanze hawajawahi hata kusikia tone la mvua likidondoka kwenye mabati yao.
 
Ya kutuliza joto hii imenyesha dk 2 tena baadhi ya maeneo labda kwenye lami inaonekana kwa kuwa haiendi chini inaishia kwenye mitaro huku shamba hakuna hata kidimwi kimoja ni vumbi tu.
 
Iringa mjini jana imenyesha yakutosha na sasa kuna dalili yaweza nyesha na leo.
 
Duh kweli huu mwaka wa mapicha picha, nadhani siku nyingine usiandike uzi jumuishi mkuu pasipo kuwa na taarifa za kutosha kuhusu eneo unalolizungumzia mathalani mimi nipo hapa Kihonda kwa mkomola hiyo mvua unayoizungumzia kunyesha morogoro, mitaa hii haijanyesha mkuu.
 
Mtulize akili Mlime na mtunze Mazao yenu, mkijishaua hakuna Chakula cha Bure
 
Habari za asubuhi wakuu! hatimaye Morogoro mjini tuna anza kuona matokeo ya dua na maombi ya viongozi wa dini, mvua imeanza kunyesha kuanzia saa 5:30 mpaka sasa hivi bado inaendelea sijajua ndugu zetu wa Mahenge na sehemu nyingine kama wamebahatika kupata hizi baraka, mda si mrefu Morogoro hatuta kuwa na kelele za njaa.

Uchochezi huo,nani kasema kuna njaa.

Wenzako wameshiba,kwao kuna nyasi za kijani,wanaenda shopping mlimani city na hawauliZi bei,wewe unasemaje kuna njaa,mvua peleka mtera,mwenzio hata shati lake linaashiria shibe ndo maana la rangi kijani.

U
 
Back
Top Bottom