Mvua yaanza kunyesha Morogoro

Mvua yaanza kunyesha Morogoro

Mvua inakuja kwa wakati wake hakuna cha maombi ya viongozi wa dini. Mungu hufanya yake kwa ratiba yake na hao viongozi wa dini hutuambia hivyo. Huu ni wakati wa BWANA.
 
Ya kutuliza joto hii imenyesha dk 2 tena baadhi ya maeneo labda kwenye lami inaonekana kwa kuwa haiendi chini inaishia kwenye mitaro huku shamba hakuna hata kidimwi kimoja ni vumbi tu.
😀😀😀hahaaaaaa
 
Mbegu amekula!
🙁🙁Duh! mkuu kama ndio hivyo mbona yupo kwenye hali mbaya, ok! kale kanyongeza ka mshahara bado sijakatumia ninge mchukulia hapa mjini alafu angekuja kuzichukua au angetuma mtu aliyeko huku angemchukulia.
 
Iringa mjini jana imenyesha yakutosha na sasa kuna dalili yaweza nyesha na leo.
Mkuu vipi huko Iringa na leo imenyesha ili huku tuanze kuandaa majaruba au ndio hiyo iliyo kuja kwetu asubuhi.
 
mlime kwa wingi mpunga uko..
Mkuu tutalima kwa wingi tu ila si unajua thamani ya mpunga ni tofauti na maindi kwa hiyo mujiandae kuthaminisha gunia kwa ng'ombe sita au thamani ya pesa ya ng'ombe sita 😀😀😀😀
 
Kutakuwa na kelele za mafuriko na mazao kuharibiwa na mvua...
 
Yaani leo imepiga balaa, naamini kunasehemu kutakuwa na mafuriko.
kwahiyo mkuu mkayaacha maji yaende mabondeni? alafu wiki ijayo mtaanza kuilalamikia njaa serikali wakati mmeshindwa kutumia baraka mulizozipata!
 
Mkuu tutalima kwa wingi tu ila si unajua thamani ya mpunga ni tofauti na maindi kwa hiyo mujiandae kuthaminisha gunia kwa ng'ombe sita au thamani ya pesa ya ng'ombe sita 😀😀😀😀
ah.. nmekusom mkuu.

mx_nature
 
kwahiyo mkuu mkayaacha maji yaende mabondeni? alafu wiki ijayo mtaanza kuilalamikia njaa serikali wakati mmeshindwa kutumia baraka mulizozipata!
Mahindi, maharage na karanga tulizopanda zina yatumia maji sasa, maana hali ilikuwa mbaya.
 
Kutakuwa na kelele za mafuriko na mazao kuharibiwa na mvua...
Hapo ndipo unapoona tofauti kati ya mwafrika na mzungu, ndiomaana huwa wanatushangaa sana tunapo lalamika ukame wakati nchi imezungukwa na maji pande zote nne wakati Israeli walipo pata uhuru nchi yao ilikuwa jangwa tupu ila ndani ya miaka sita wakaibadilisha sasa hivi wanalima mabustani ya matunda makubwa. Huwa najiulizaga maswali sipati jibu ninapo ambiwa toka uhuru Mkoa wa singida unashida ya maji kwa sababu ardhi yake ina asili ya ukame ila swali la kujiuliza kama ni kweli ni hivyo mbona kuna watu wa mission wamechimba kisima na wanatumia maji safi tu ina maana hata hao viongozi wa huko miaka zaidi ya hamsini hawalijuhi hili? au na lenyewe lipo kwa sababu za kisiasa.
 
Mahindi, maharage na karanga tulizopanda zina yatumia maji sasa, maana hali ilikuwa mbaya.
Ila mkuu mjitahidi kutafuta njia mbadala ya kuhifadhi maji kwa muda mrefu inatubidi tuanze kubadili mfumo wa kulima kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani tunapaswa kuacha kilimo cha kutegemea mvua, kuna siku niliangalia clip moja ya video ya waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyau alikuwa anazungumzia kuhusu mafanikio ya Israeli alisema "waisraeli mpaka walipo fika sasa nchi yao walipigania kwa jasho na damu ila matatizo waliyo yapata na vikwazo vingi kutoka kwa maadui wao walio wazunguka kila upande ndio walio sababisha Israeli iwe jinsi ilivyo sasa hivi" kwahiyo mkuu siku zote matatizo ni kipimo cha akili, na waswahili wanasema kukosa ndio kujifunza au mtenda kosa haja kosa, kosa ni kurudia kosa.
 
Back
Top Bottom