MV Butiama imezimika ni msaa 4 sasa hakuna msaada

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Habari za Uhakika toka Mwanza zinasema Mv.Butiama ikiwa abiria kutoka Mwanza kwenda Ukerewe imezimika katikati ya Ziwa Victoria na yapata masaa 4 sasa hakuna msaada . Naambiwa watu wameanza kusali na kukata tamaa maana kuna hofu sasa kwamba Meli yaweza kuzama . Tafadhali mwenye habari zaidi azidi kutu habarisha hapa.
 
Hakika habari hizi ni za kusikitisha sana maana kama ni kweli basi Mungu asaidie kuona kama ndio hivyo. Hivi ofisi ya Maafa ya waziri Mkuu wanafanya nini??
 
Lets hope kuna process zinaendelea, kwa ajili ya kuwaokoa watu hao.
 
Lets hope kuna process zinaendelea, kwa ajili ya kuwaokoa watu hao.
yaani nnchi hii aacha tu, napiga simu pale kitengo cha maafa kutoa taarifa hizi zaidi ya nusu saa simu hazipokelewi, napiga Wizara ya miundo mbinu hapa mwanza na ofisi za ujenzi wanadai wanashughulikia swala hilo, ngoja niende kule bandarini nijue japo juhudi gani zinachukuliwa kuokoa hili janga lilikua jirani nasi.
 
The God of Abraham,

The God Isaac, and

The God of Jacob, please help these fellows. look, they are in trouble...May you Send the holly spirit to them to soothe their souls and to courage them up!

Rather to enable the captains and techical men to come up with the solution on the snag!

In the name of Jesus i pray, Amen!
 
yaani nnchi hii aacha tu, napiga simu pale kitengo cha maafa kutoa taarifa hizi zaidi ya nusu saa simu hazipokelewi, napiga Wizara ya miundo mbinu hapa mwanza na ofisi za ujenzi wanadai wanashughulikia swala hilo, ngoja niende kule bandarini nijue japo juhudi gani zinachukuliwa kuokoa hili janga lilikua jirani nasi.

Watanzania tuko wajinga sana. Hapo watu wanasubiri baada ya matatizo waanze kutoa ripoti ya maafa na wengine kutubeza kuwa hawatajiuzulu ng'o kama alivyotuambia Kusila baada ya MV Bukoba.

Kwa wale mlio karibu jaribuni hata kuomba msaada kwa watu binafsi. Pia ikiwezekana jaribu kupiga simu kwenye redio na TV ambazo zinaweza kurusha hiyo habari mara moja. Wakubwa wa bongo wanaogopa media kuliko jehanamu! Watafukuzana kama swala waliongiliwa na Simba. Plse try to help.
 
kwa neema za Mungu hakuna kitu kibaya kitakachowapata....
tuweni na imani.....
 
Watanzania tuko wajinga sana. Hapo watu wanasubiri baada ya matatizo waanze kutoa ripoti ya maafa na wengine kutubeza kuwa hawatajiuzulu ng'o kama alivyotuambia Kusila baada ya MV Bukoba.

Kwa wale mlio karibu jaribuni hata kuomba msaada kwa watu binafsi. Pia ikiwezekana jaribu kupiga simu kwenye redio na TV ambazo zinaweza kurusha hiyo habari mara moja. Wakubwa wa bongo wanaogopa media kuliko jehanamu! Watafukuzana kama swala waliongiliwa na Simba. Plse try to help.
rekebisha kauli yako hiyo (bolded)
 
Inakuwaje atu wakae ziwani kwa saa nne bila msaada wowote? Hii ndio response yetu kwa majanga. Mungu saidia watu hawa wasiaptwe na baya lolote
 
Wajameni, hebu tuliangalie hili suala kama watanzania tuliokubali utendaji "slow wa serikali yetu na sisi wenyewe", ni lini tuliwahi kurespond kwenye emergency na desired speed???

Huu upungufu tumejitakia wenyewe kwa kukalia kimya kila matatizo, ukiuliza kwa nguvu kuhusu "slowness" ya huduma utashangaa kuona wateja wenzako wanakwambia acha kujifanya mzungu etc.

Ni mpaka yafike chumbani ndio upige kelele, utashangaa hata waliokwama wengine ni mabingwa wa kuwa slow kwenye sehemu zao za kazi

POLENI SANA WAHANGA LAKINI TUANZE KUPAMBANA NA UZEMBE NA "U-SLOW" KILA SEHEMU WATANZANIA

Hivi ina maana serikali bado haijaact mpaka saa hii?
 
Radio one wametangaza uhalisia na sasa sijui kuna kitu gani ila naambiwa Meli ilikuwa inaelekea kubaya .Sababu za kuzima kwa engine haijulikani na watu wako maofisini bize for nothing . Mwenye habari endelevu please share I am being cut off na mawasiliano sasa
 
Na ndio meli inayotegemea sana kwa safali za Mwanza kwenda Ukerewe mbali na MV Clariaus, kwakweli huo ni uzembe wa hali ya juu huwezi acha meli kwenda safari bira kuchunguzwa jamani pale mwanza South port wanafanya madudu gani haya ndiyo yalipelekea MV Victoria kuzama ikiwa yatokea Bukoba sasa wanataka kuahakikisha meli ya pili ina zama???

Masha Uko wapi please go back home and deal with them (TR L/C) perpendicular wameanza kuleta mzaaaaa tena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom