Mzee DC, Mie sio mtaalam wa Taarab but the little I know I Love and appreciate... hii ni moja ya Music hapa JF inakua rarely listed to or discussed, hopefully hii thread itaendelea na Music ya taarabu Worthwhile zitazidi miminika....
Chumvi ninaipa pole, hakika inaonewa
Sijasikia milele, chumvi pongezi kupewa
Chumvi tangu hapo kale, katu haijasifiwa
Chumvi tusiisahau, kuisifu ni wajibu
Chumvi tusiidharau, inaishinda dhahabu
CHUMVI TUSIIDHARAU - YouTube
Mwanaume mzima anaongea pumbaaaaaaa
At na yeye anaweza kujiita baba! au mume!! lol
sijui kama maisha atayaweza kwa mtazamo alonao
Ndio maana Malkia wa taarabu alishaimbaga kwamba.......
"........Wengine si wanaume......ila magumegume......." - hadija kopa
Afadhali umerudi Gee,
Naamini hiyo chumvi ni NaCl....Lol!!!!
Hapo sijajua kama ni Sodium Chloride kweli au chenginecho ........ila mie nimeamua kuitafsiri kwa chenginecho 😛
I used to love one song by Babloom Modern Taarab- HAWARA HANA TALAKA
Kukupenda sana, ndilo kosa langu
Sitofanya tena, naapa kwa Mungu
Niliyoyaona, yanatosha kwangu
Nikikumbukia, naona uchungu
Nimekupokea, kwa khiari yangu
Kumenichongea, kukupenda kwangu
kukupenda sana ndio kosa langu - YouTube
Kweli Gee,
Ni kosa kubwa kumpenda sana mtu naye akalijua hilo...Mara nyingi utajuta kumpenda!
Ni ukweli unaoumiza sana!
Apendwaye akajua haachi kujizuzua. Lazima u-make sure anakupenda yeye sana kuliko unavyompenda wewe 😛
Kwa unapendekeza mchezo wa kutegeana???
Ila kuna watu wanakuwa malimbukeni kiasi kwamba wanapoteza akili, busara na hekima wapojidai wanapenda!
Sijui ndiyo hayo mambo ya Zumbukuku???
Sijui ndo tuseme binaadamu binaadamu tumeumbwa tofauti! Maana kuna wengine wakipenda kama wagonjwa!
Atafikia hadi kupigwa, lakini humuelezi kitu.......
Mungu asituonyeshe huuuh