Muziki wa Injili umeingiliwa

Muziki wa Injili umeingiliwa

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2014
Posts
3,098
Reaction score
5,470
Shalom wana wa Mungu

Jumapili ya leo nimeamua niitumie kuyatoa ya moyoni juu ya muziki wa injili hapa Tanzania.

Ki ukweli hawa waimbaji wa siku hizi wa injili wamakera sana na nachelea kusema ninapata mashaka na Mungu wanayemwabudu.

Dressing code yao ni hovyo sana, yani wanavaa kisharobaro, yaani ni mavazi ambayo hayaleti utukufu kwa Mungu, sijui kama kuna watu wanawashauri katika hili. Nawazungumzia hawahawa wakina Gooddluck Gozbert, Akina Paul Clement na hao wengine mnaowakubali wa type hiyo. Yani ukifungua TV alaf uka mute sauti unaweza ukamaliza wimbo bila kujua kama ni Bongo fleva au ni injili.

Ee Mungu tusamehe turudishie waimbaji wetu wenye adabu na staha kwenye ramani. Akina Ambwene Mwasongwe, Mchungaji Abihudi, Christina Shusho na wengine wa type hyo...

Hawa wa sasa wanaondoa kabisa utukufu wako
 
Utkufu wa Mungu ni Individual feeling, kunawanaopenda hiyo melegezo maana wanajiona wapo sehemu ambayo ni sahihi wao kuwapo wakiona wanakwaya wamevaa kama wao.
Nadhani nilipaswa kutoa precaution kwamba wanaopaswa kuchangia ni wale wanaojua umuhimu wa kuvaa vizuri katika ibada. Lakini nimekusamehe bure
 
Nadhani nilipaswa kutoa precaution kwamba wanaopaswa kuchangia ni wale wanaojua umuhimu wa kuvaa vizuri katika ibada. Lakini nimekusamehe bure
Usihukumu Kaka, hata hao waliotuletea Injili ni wavaa hovyo wakuu tena huke huke kanisani, Labda sisi kama Wa Africa turudie inada za ki Africa hapo tutaweza kuelewana. Lakini kama tutaendelea na tizi dini za Mkoloni basi utayaona Mengi sana.
 
Huwezi kumfananisha Mungu na uchafu
Wanataja Mungu lakini bado wanaipenda dunia
unakuta kiongozi wa dini amevaa mlegezo
kwasasa kwakuwa tunaishi kwa neema ya Yesu kristo
ndo maana unaweza kutenda uovu
ukaendelea kuishi kwakuwa hukumu ya mwisho kwa wadhambi wote inakuja.
Mungu ni mtakatifu sana sana

Zamani ilikuwa ukitaja tu jina Mungu bila sababu ya msingi unakufa hapohapo.



'Gear yourself to solutions in every problem'
 
Ibada kwwa njia iliingiliwa na shetani kitambo baada ya mason akiwamo marehemu Bill Graham kuanzisha bendi za muziki kanisani ili kuwafanya waabuduo wawe na concept ya eintertainment zaidi kuliko ibada kwa hiyo unaposema tu muziki wa injili unaongelea maburudisho ya mioyo sio ibada . Kuvaa na maonyesho kwa aina zake ni sehemu ya maburudisho ya mioyo.
Kimsingi kumbi za muziki zimehamia nyumba za ibada.
Tumeshuhudia kanisani watu wakicheza " Mapanga shaaa' ndombolo" reggae na mitindo yote .
Miziki ina code zake za uimbaji uchezaji na uvaaji pia. TWENDENI hivyo akili mu kichwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utkufu wa Mungu ni Individual feeling, kunawanaopenda hiyo melegezo maana wanajiona wapo sehemu ambayo ni sahihi wao kuwapo wakiona wanakwaya wamevaa kama wao.
never uovu hata uupambe vip hauwezi kuwa ukwel

[emoji375][emoji375]
 
Back
Top Bottom