Muziki wa Injili Katika ''Kilabu cha Pombe''...!!!

Kwani ulipo kwenda kunywa supu ulitenda dhambi gani? bar si sehemu ya mahasi ila ni sehemu wanapokutana watu mbalimbali wenye maadili tofauti. Wengine ni sehemu ya kufanyia vikao , appointment n.k. Hakuna dhambi yoyote kuweka muziki huo bar hata kama wahusika hawahudhurii kanisani lakini wanapata ujumbe huko huko bar ambao waweza kuwasaidia wsasitende dhambi au kwa tafakari ya ujumbe uliomo wakaja kubadilika siku za mbeleni
 
Wadau wa JF ningependa kushare nanyi hiki kisa nilichokutana nacho asubuhi hii baada ya kuingia katika bar moja hapa Mbagala Charambe ili kupata supu. Kilichonistua ni kukuta katika hiyo bar zinapigwa nyimbo za injili, na walevi wachache waliokuwa wamepambazua wakijitahidi kufurahia nyimbo hizo kwa kuziimba kwa kuigilizia. Pamoja na furaha hiyo ya walevi lakini kitu kibaya zaidi walikuwa wanaimba nyimbo hizo kwa kuzi abuse. Wanabadilisha baadhi ya maneno na kuimba matusi. Kwakweli Jumapili yangu leo nimeianza kwa kustaajabu huu ujasiri wa hawa wamiliki/waendesha vilabu vya pombe kumdhihaki Mungu kwa kiwango hiki. Nawatakieni jumapili njema raia wote. Msisahau kufanya ibada![/QUOTE

kwanza ifahamike wazi kwamba kutokana na wingi wa makanisa na hali ngumu ya maisha wanaomiliki mabaa hayo na wafanyakazi wao ni watu wanaokwenda makanisani ...tena ni watoaji wazuri wa sadaka na misaada mingine mingi kwa jamii.... wanaoingia katika mabaa kunywa supu sio wote ni walevi kunawanaotoka makanisani na kuingia kwa ajili ya supu na soda na kujiondokea....walevi pia wanakwenda makanisani na hata misikitini.... kwa hali ilivyo mambo ya nyimbo za injili katika mabaa na shoo mbali mbali ni jambo la kawaida..... nadhani utashtuka siku ukiingia ndani ya baa na usikie Qur'an au kasida inaungurumishwa lazima watu watatoka mkuku

Kwa nini watoke mkuku wakati peponi kuna pombe? na madanguro ya kukabiziwa wanawake sabini.
watatoka mkuku kwa kuofiya kuvamiwa na wahuni,
2 watakimbia kwa kuofiya kuongezewa mzingo mwingine wa majini.
 
BIA. Kili awards kumtunza Rose Mhando inaonyesha kuwa shetani naye anaamini kuwa mungu ni zaidi popote pale kwa mataifa na mbinguni
 
Acha waziweke, injili inahubiriwa mpaka kilabuni! Hakuna atakaesema sikusikia siku ya hukumu itakapofika. Isitoshe Mungu hatishwi na dhihaka za wanadamu.
 
Yaani unaenda bar unategemea ukutane na watu wasiokuwa walevi?. Walevi wenyewe wamelewa.
Nakushauri ukaichome hiyo bar.
Akishaichoma kesho atakunywa supu wapi?
Mungu wetu si Mungu wa visirani. Kupitia hizo nyimbo wako ambao wataijua hiyo kweli.
 
Hujaelewa hoja yangu. Rudia kunisoma ili unielewe na utoe comment ya kueleweka ustaadh Mustafa!
Ushauri wako wa kuichoma hiyo bar hauna tija sana kwahiyo ni sawa na kusema hujatoa ushauri.
Hiki ndicho kiwango chake cha kuchangia. Kuchoma moto!
 
...waaaooo ..! What a good news ! Yaani watu tunaumiza vichwa tutafikaje kwenye mabaa, madanguro,vijiwe vya unga,nyumba za wasioamini,wajahidina n.k,kumbe njia nyepesi ni muziki..!, kwa moyo wa dhati kabisa naipongeza hiyo bar.
naziomba bar zote ziige mfano huu bora wa
kuwapa habari njema walevi wote...

Barikiwa!
 
BIA. Kili awards kumtunza Rose Mhando inaonyesha kuwa shetani naye anaamini kuwa mungu ni zaidi popote pale kwa mataifa na mbinguni

Tena ndugu yangu, Shetani anayajua maandiko kuliko hata sisi, na ndiyo sababu alithubutu hata kumjaribu Yesu.

Barikiwa
 
Ussitaajabu Tena nawaomba wenye baa waendelee kutuwekea mziki wa injili kila siku asubuhi,
wenye afya hawaitaji tabibu bali walio hawawezi
sikuja kuwatafuta wenye haki bali wenye dhambi,

injili inapoingia mahala popote si tu inalengo la kubadilisha watu, bali pia kuweka ushaidi kwamba wamesikia, kwa hiyo suala la ziaka lisikusumbue hata wasio walevi wa pombe wanazihaki injili,
Mathayo 24:14
Tena habari NJEMA YA UFALME itahubiriwa katika ulimwengu wote, KUWA HUSHUHUDA kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

Barikiwa!
 
uko sawa kabisa, injili ni kwa walio mbali nayo, haiwezekani samaki ukamfundisha kuogelea, akili ikikaa sawa watajua makosa yao
 
Wacha Injili itangazwe, Injili haikuja kwa walio haki, bali kwa wasio haki ili waongoke.

Kama Bia zinaweza mtunza mwimba injili (Kili Music Awards) kwanini Injili isijipenyeze kwa wanywa bia??

Leo wameimba kwa kuzikejeli, its a good start kwanza kufahamu melody, kesho akiwa sober kidogo akiisikia ataiimba kiukweli na itampenya, atajiuliza mara mbili

Duniani ni mapambano

Samahan wadau mnaoshiriki katika hii mada
Mimi bado nahitaji kujua uhalali wa hizi nyimbo kutumbuizwa bar, night club nk
wanaojua mambo nawaomba mnifafanulie zaidi wandugu ili nipate kujua, kuelewa na kushawishika ili kuepuka kila mtu kujibu kwa utashi wake unampeleka wapi bila kujali Mungu analichukuliaje jambo hili with evidence kutoka kwenye vitabu
 
BIA. Kili awards kumtunza Rose Mhando inaonyesha kuwa shetani naye anaamini kuwa mungu ni zaidi popote pale kwa mataifa na mbinguni

duh nahii nayo Mungu ameelekeza au ni namna moja ya kuwafanya watu tufikie kwenye lengo linalokusudiwa na walimwengu?
 
Ndugu yangu Dar ina mambo mengi sana tena hizo pande za Mbagala ndiyo balaa maana waswahili wengi walikimbilia huko kwa sababu ya unafuu wa maisha
 
Back
Top Bottom