Memtata
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 552
- 1,801
Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na rafiki zangu walevi wakakomaa twende kijiwe kimoja cha pombe. Kilikuwa ni kigrocery kidogo lakini kimechangamka hivi, japokuwa pombe nishaacha lakini nilivutiwa sana na hili eneo. Sio kwa uchangamfu bali ni baada ya kumuona muhudumu aliyekuja kutuhudumia, kama utujuavyo wanaume rijali🤣🤣najua wale wenye matatizo yao na kujifichia kwenye uaminifu mtanikebehi hapa 🤣
Huyu dada alikua anaitwa Joyce alikuwa ni mzuri kwakweli, nnaposema mzuri si kwa macho yangu pekee hata rafiki zangu walisema “unadhani kwanini tunakuja kunywa huku kwenye hiki kigrocery mshenzi” 🤣
Mimi nilikuwa sinywi pombe, wenzangu wakiwa wanasubiri wapate starter ya kuondoa aibu ndio wamtongoze mi nikanyanyuka nae faster. Siku hiyo nikakomaa na jamaa hadi saa6 usiku ilimradi wafunge niondoke na Joyce. Hili ni jina lake halisi kabisa na nilimwambia nitaandika kisa chako akasema 'hakuna shida mi nilishavurugwa’🤣
Tumekuwa tukikutana na wanawake wazuri na wengine wazuri sana wakifanya kazi bar ama wakijiuza na maranyingi watu hujiuliza wamekosa nini hawa?! Leo kwa mara ya tatu nipo na Joyce tumejificha kwenye hoteli moja nje ya mji kabisa akigonga lager mi na maji yangu na fegi nikaanza kumuhoji kwanini yuko hapo.
Joyce akilewa ni muongeaji sana, basi akaanza kufunguka. Anasema alikuwa na mume wake mwanajeshi mwenye nafasi yake, jamaa walikutana Kibondo alipokwenda huko kikazi wakati huo Joy alikuwa kidato cha tatu lakini alikuwa mtukutu haswa bar zote za mjini wanamjua. Jamaa akampenda wakapeana namba za simu, baada ya mishe za jamaa kuisha akarudi Dar kituo chake cha kazi.
Mshkaji alivyofika Dar wakawa wanawasiliana na Joy akamwambia anataka aje kutoa mahari kwao, Joy akarahisisha mambo akamwambia wewe nitumie nauli mi nakuja hayo ya ndoa yatafata baadae.
Jamaa akatuma mpunga wa kutosha Joy akatoroka kwao… anasema alitoa taarifa kwao wasisumbuke kumtafuta yeye ameenda kuolewa, wakati huo akiwa ameshafika Kahama!
Joyce akapokelewa na jamaa kwenye gari hadi kwao. Kumbe jamaa alikuwa anaishi Chalinze lakini kituo cha kazi kilikuwa Dar. Lakini jamaa alikuwa vizuri sana, mjengo wa maana na kila kitu ndani cha maana na ndinga la kishua. Mtoto akakaribishwa mjengoni kama maza house. Waliishi yeye na jamaa, beki tatu na kijana wa kazi za nje ambaye alikuwa anahudumia kuku na usafi wa nje.
Kuna mengi Joyce kanielezea kuhusu huyu mwanaume siwezi kuandika yote lakini kifupi jamaa alimpenda sana mke wake yani sana…. Jamaa alimjali kwa kila kitu anasema hadi kumuogesha na kumfulia nguo zake hadi underwear!
Jamaa alikuwa Muislam ila Joyce alikuwa Christian (Mkatoliki). Kila jumapili alimpeleka kanisani na alimsubiri nje akiwa kwenye gari muda wote wa ibada na kisha kumrudisha nyumbani.
Ilifikia wakati mwamba akawa na mawasiliano na wazazi wa Joyce nao wakampa baraka zote. Jamaa akaanza kumpanga Joyce na kumwambia inabidi waoane na ingependeza kama Joyce angebadili dini na kuwa Muislam. Joyce alikubali na akaanza kupata mafunzo ya dini.
Tatizo la huyu jamaa alikuwa na wivu sana nadhani sababu alimpenda sana Joyce, hakutaka atoke nyumbani na kwakuwa home kulikuwa na CCTV camera ambazo zilikuwa linked na simu yake basi kila Joy akitoka jamaa anampigia na kumuuliza alikuwa wapi.
Lakini anasema hakuwahi kumpiga wala kumfokea kwa hasira bali alikuwa analalamika kwa upole na uchungu na kama Joyce angemjibu vibaya basi jamaa huishia kulia, kuacha kula na kulala mbali kitandani bila kumsemesha chochote siku hiyo. Inavyoonekana Joyce alilewa mapenzi akajiona yeye ndo yeye na jamaa hana jeuri kwake sababu anampenda sana.
Mzozo ulianza kuwa mkubwa Joyce akawa hadi anamtamkia kabisa jamaa kwamba hampendi lakini jamaa alikuwa hachoki kumbembeleza na inaonekana aliumia sana maana anasema kila wakati alikuwa hafichi hisia zake kwa Joyce na alikuwa analia sana. Fikiria mwanaume mwanajeshi mwenye kitengo chake kudondosha chozi!😢
Binafsi mimi sikushangaa hili maana Joyce anasema wakati huo alikuwa yuko moto sana hadi nikajikuta namuuliza ‘unamaana ulikuwa mzuri zaidi ya hapa!?’ akajibu ndio hapa ameharibika baada ya kuzaa na kukutana na changamoto za kimaisha. Jamani sitanii Joyce ni mzuri kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia anataka amtongoze Joyce ili aende nae kuuza sura kwenye sherehe ya kampuni ya kufunga mwaka!😁Acheni kabisa naongea haya mjue kabisa uzuri wa Joyce si kwa jicho langu la tamaa tu 😃
Mzozo wa Joyce na jamaa yake ulikuwa zaidi hadi kufikia Joyce kumshurutisha jamaa ampe nauli arudi kwao. Unaambiwa siku hiyo jamaa alilia sana lakini Joyce hakusikia la muadhini wala mtangaza kifo akakomalia arudi kwao. Neno la mwisho la jamaa kwa Joyce “mke wangu unaondoka mimi bado nakupenda nakwambia wazi wanaokudangaya hawatokupenda kama mimi”
Haikusaidia kitu Joyce akakomaa kuondoka, jamaa akamsaidia kukusanya kila anachotaka akampeleka hadi kituoni siku ya safari mrembo Joyce akarudi kwao Kibondo. Kibondo!!! 😀
Wakati naendelea kuandika sehemu ya pili nakaribisha sumu kama sio povu