Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,993
Wadau wa JF ningependa kushare nanyi hiki kisa nilichokutana nacho asubuhi hii baada ya kuingia katika bar moja hapa Mbagala Charambe ili kupata supu. Kilichonistua ni kukuta katika hiyo bar zinapigwa nyimbo za injili, na walevi wachache waliokuwa wamepambazua wakijitahidi kufurahia nyimbo hizo kwa kuziimba kwa kuigilizia.
Pamoja na furaha hiyo ya walevi lakini kitu kibaya zaidi walikuwa wanaimba nyimbo hizo kwa kuzi abuse. Wanabadilisha baadhi ya maneno na kuimba matusi.
Kwakweli Jumapili yangu leo nimeianza kwa kustaajabu huu ujasiri wa hawa wamiliki/waendesha vilabu vya pombe kumdhihaki Mungu kwa kiwango hiki.
Nawatakieni jumapili njema raia wote. Msisahau kufanya ibada!