Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 1,118
- 1,915
Rejelea kichwa cha habari. Kuna haja ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuvujwa kwasababu hauna faida yeyote Tanganyika. Tangu muungano huu Zanzibar ndiyo imekuwa ikinufaika kutoka Tanganyika lakini Tanganyika haijawahi kunufaika kutoka Zanzibar.
Zanzibar wamekuwa wakichota mchanga na mawe kutoka Tanganyika kwasababu ya tatizo la udongo wao, siyo hivyo tu Zanzibar inamiliki eneo lenye ukubwa wa hekta 6000 tangu mwaka 1977 katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Wakazi wa Tanganyika wanapokwenda Zanzibar hawapokelewi mpaka pale wanapokuwa na vitambulisho mbaya zaidi Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar huku Wazanzibari wakimiliki ardhi Tanganyika. Katika nyanja za siasa Watanganyika hawapewi fursa ya kuwa viongozi Zanzibar huku Wazanzibari wakipewa nafasi nyingi kwenye serikali ya Tanganyika.